Hivi ni Somo la Historia litafundishwa rasmi kwa Kiswahili au kutakuwa na masomo mawili ya Historia huku Somo la Sasa likibaki Kama kawaida?

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,469
Najiuliza swali Hili: Kutakuwa na masomo mawili ya Historia huku somo la Sasa likiendelea kufundishwa kwa kingereza? Je kutakuwa na somo jipya la Historia ya Tanzania litakofundishwa kwa kiswahili kuanzia daraasa la kwanza hadi form six ambalo ni la lazima?

Kimbukeni Rais kasema Historia ya Tanzania iandikwe upya na kufundishwa kwa kiswahili kwa ngazi hizo za elimu. Waziri wa elimu kaagizwa kusimamia hili haraka na lianze kufundishwa January 2022.

Niondoleeni utata ktk hili maana sidhani hata Kama huyu waziri na Rais wameelewana na sidhani Kama Waziri anafahamu Rais anataka nini na pia Rais sidhani Kama ana uhakika ikiwa waziri wa Elimu kamuelewa.
 
Naam masomo yatakuwa mawili, la mwanzo litabaki kama lilivyo na hili jipya litaitwa Historia Tanzania na ndilo litakalo fundishwa kwa kiswahili na litasheheni historia yetu tu kama Taifa.
 
Aisee ukiangaika na Elimu ya Tanzania unaweza kupata uchizi, wekeza kwenye ufugaji unaweza kutoboa maana hakuna kodi huku
Uwekezaji nao inategemea mkuu, jamaa kapanda miti yake ya mbao huko Mafinga umekomaa baada ya miaka dahari kavuna kauza kapata milioni zaidi ya 300. Mara paaa fwedha imedakwa yote huko kwa akaunti.
 
Aisee ukiangaika na Elimu ya Tanzania unaweza kupata uchizi, wekeza kwenye ufugaji unaweza kutoboa maana hakuna kodi huku
Anzisha mada hii, acha kuvuruga uzi wenye mjadala mzuri kwa Taifa letu. Nafuga pia nikujulishe, ila sijigambi.
 
Naam masomo yatakuwa mawili, la mwanzo litabaki kama lilivyo na hili jipya litaitwa Historia Tanzania na ndilo litakalo fundishwa kwa kiswahili na litasheheni historia yetu tu kama Taifa.
Kwa kweli nimechanganyikiwa. Hivi somo la historia lilishafutwa na ndipo sasa inatakiwa lifundishwe? Au Mimi sikumwelewa mfalme?
 
Kwa kweli nimechanganyikiwa. Hivi somo la historia lilishafutwa na ndipo sasa inatakiwa lifundishwe? Au Mimi sikumwelewa mfalme?
Halijafutwa kama nilivyoeleza, lipo pale pale ila lile limebeba mambo mengi ya mataifa tofauti duniani.
Hili la sasa ni kwa ajili ya kujifunza historia yetu kabila mpaka kabila, mazingira yetu, asili yetu na yote ambayo yalipotea bila kufundishwa popote.
 
Anzisha mada hii, acha kuvuruga uzi wenye mjadala mzuri kwa Taifa letu. Nafuga pia nikujulishe, ila sijigambi.
Mkuu subiri watu wengine wasema kama mjadala ni mzuri au sio mzuri, usiseme wewe mwenyewe ulieanzisha uzi.
 
Back
Top Bottom