The problem solutionist
Member
- Jan 28, 2024
- 13
- 9
Mimi kama mdau wa jamii forum nimeona hoja na kero nyingi zikipatiwa ufumbuzi mbali mbali hivyo naomba kuwasilisha hoja yangu ya msingi hapa!
Ni kuhusu wizara ya elimu hapa nchini ninaomba waliangalie hili kwa umakini!
Mimi ni miongoni mwa watu waliohitimu mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Tabora mwaka 2015 lakini ndani ya mwaka huo na miaka mingine yote vyuo vya ualimu vyote vilikuwa chini ya NECTA yani baraza la mitihani lakini badae waliofuata waliwekwa chini ya NACTE na ndani ya mwaka huo kuliambatana na mabadliko mengi sana ikiwemo ya BRN nakumbuka tuko likizo ya Mwezi wa kumi na mbili tunapigiwa simu tukiwa majimbani kuwa vyuo vikifunguliwa kutakuwa na mitihani ya BRN
Ila hoja ya msingi hapa ni kwamba navoelewa mimi vyuo vya ualimu kwa kipindi hicho vilikuwa chini ya NECTA manake mitihani yetu yote ilisahishwa na baraza la mitihani yani hakuna utaofauti na shule za msingi na secondary yani O-levels na A-levels kwani wale mtu anapopata alama zile kuanzia alama A,B,C,D na F matokeo yake yanaoneshwa na alama alizozipata lakini wale wa O-level na A-levels na shule za msingi huwa wanapewa vyeti vyao hata kama kapata mfano alama F mbili anapata cheti lakini kwa vyuo vya ualimu kwa kipindi kile mtu hapewi cheti na unakuta amefeli somo moja tena basi sio masomo ya kufundishia lakini hapewi cheti chake.
Kwanini mtu huyu asipewe cheti kikionesha kuwa amefaulu masomo haya na haya na amefeli somo hili moja ili hicho cheti kimsadie mtaani kutafuta kazi hata shule za binafsi kwani serikali haiwez kuajiri wahitimu wote lakini kitendo cha kuwanyima vyeti kwa kufeli somo moja mimi kwangu naona sio haki sidhani kama somo moja linaweza kumfanya mtu asiwe na ufanisi na sio kweli kwamba kwa miaka miwili yote aliyokaa chuoni na kusoma mtu huyo hajatoka na chochote kisa somo Moja!
Kwangu sio haki mimi nilijaribu kuwasilisha maoni yangu kwa wizara husika bila mafanikio tena kipindi hiko mama Ndalichako ndo alikuwa waziri wa elimu nilipompigia simu alinijibu vibaya nikajaribu kumtumia ambae sasa ni waziri wa Kilimo mheshimiwa Hussein Bashe nae aka kaa kimya sikukata tamaa nikaamua kutuma maoni yangu ikulu bahati nzuri ikulu walinijibu barua pepe yangu wakanielekeza kupeleka maoni yangu kwa aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya elimu mheshimiwa Leonard Akwilapo alinitumia barua pepe akiniomba niandike maoni yangu kwa lugha ya kiswahili ili apate kunielewa vizuri nikafanya ivyo lakini mpka leo hajawahi kunijibu toka mwaka 2016 mpka leo
kwahiyo unakuta vijana wengi ambao walikuwa na tatizo kama langu au wenye tatizo kama langu! Wako mtaani wanakosa ajira kwasababu ya somo moja kuwaangusha mimi siamini na sitoamini kwamba somo moja linaweza kumfanya mtu asiwe na ufanisi! Sio kweli hivyo ninaomba kwa kuwa mabadiliko yale yalijua ghafla tunaomba waziri wa elimu aliangalie hili kwa jicho la tatu ili nasisi tupate vyeti vyetu ili vitusaidie kufanya maisha mengine huku mtaani!
Mimi kwa upande wangu nimeshajitolea mpka kuwasaidia au kufundisha shule za serikali bila malipo hivyo naomba jamii forum mkombozi wa fikra za jamii iweze kufikisha hoja hizi kwa wizara husika