Hivi ni sahihi mtoto kufukuzwa shule ya msingi kisa hajui kusoma na kuandika?

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,253
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule ya Serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya Serikali.

Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.

Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani.

Je ni sahihi?
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule. Ya serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya serikali.
Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani. Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani. Je ni sahihi?
Hapana. Pamoja na kwamba ni maajabu na siyo sawa mtoto kufika darasa la 3 na hajui kusoma wala kuandika. Hao walimu wanatakiwa wampe special programme ya kumfundisha na siyo kumrudisha nyumbani.

Sasa kama ni hivyo shule ziko kwa ajili gani? Hao wazazi wangeweza kumfundisha nyumbani wangeshafanya hivyo lakini inavyoonekana hawana uwezo huo.
 
Rip JPM, walimu walikuwa wanafanya kazi yao vyema si sasa, wamekaa kiupigaji na kimichongo.
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule. Ya serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya serikali.
Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani. Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani. Je ni sahihi?
Ni sahihi 100% huyohuyo mzazi ndiye baadae atakaye wasema hao walimu pale mtoto wake atakapo shindwa kupita darasa la 4.

Mtoto yuko darasa la 3, halafu hana sifa za kuwa MBUNGE?
 
Hapana. Pamoja na kwamba ni maajabu na siyo sawa mtoto kufika darasa la 3 na hajui kusoma wala kuandika. Hao walimu wanatakiwa wampe special programme ya kumfundisha na siyo kumrudisha nyumbani. Sasa kama ni hivyo shule ziko kwa ajili gani? Hao wazazi wangeweza kumfundisha nyumbani wangeshafanya hivyo lakini inavyoonekana hawana uwezo huo.
Kwenye hiyo special program akizidisha kiburi akachapwa viboko vi3 utakuja na kauli hizi tena?
 
Darasa la tatu hajui kusoma? Na umeeleza alitoka "shule ya English medium"? Hideous! Yawezekana walimu walitaka asome kwa Kiswahili ndipo mwanafunzi akashindwa "sababu kazoea kusoma kwa kiinglish"! Natania.

Hawezi kweli kusoma au anadekadeka/poutings za kitoto?Arudishwe darasa la kwanza na mzazi akadai ada alizotoa kule "Saint Masokola" haraka. Namuamuru!
 
Inawezekana wala sababu sio kutokujua kusoma na kuandika, kuna uwezekano dogo anagonga ngeli waalimu wa kayumba hawamwelewi, hebu hili nalo lichunguzwe, huko kayumba watoto kibao wanamaliza la saba hawajui kusoma wala kuandika.
 
Kwenye hiyo special program akizidisha kiburi akachapwa viboko vi3 utakuja na kauli hizi tena?
Kwenye hiyo special program akizidisha kiburi akachapwa viboko vi3 utakuja na kauli hizi tena?
Tatizo wewe siyo mwalimu. Viboko havifanyi mtoto ajue kusoma na kuandika na ni makosa kumchapa mtoto kwa kushindwa kusoma na kuandika. Ndiyo sababu huwa kuna mafunzo maalumu kwa walimu wanao-deal na watoto wadogo. Siyo watu tu kama Mnafiki Wa Kujitegemea wanapewa kufundisha watoto wadogo.
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule. Ya serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya serikali.
Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.
Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani. Je ni sahihi?
Darasa la tatu hajui kusoma na kuandika, sasa huko shule za kulipia alikuwa analipia nini!?
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule. Ya serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya serikali.
Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.
Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani. Je ni sahihi?
Ni sahihi kabisa.

Na wazazi hamfahamu kama huyo mtoto hajuwi kusoma wala kuandika?

Mpelekeni shule ya watoto wenye matatizo.
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule. Ya serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya serikali.
Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.
Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani. Je ni sahihi?
Jina la shule na jina la Mwalimu Mkuu tafadhali.
Dkt. Gwajima D tupe muongozo
 
Tatizo wewe siyo mwalimu. Viboko havifanyi mtoto ajue kusoma na kuandika na ni makosa kumchapa mtoto kwa kushindwa kusoma na kuandika. Ndiyo sababu huwa kuna mafunzo maalumu kwa walimu wanao-deal na watoto wadogo. Siyo watu tu kama Mnafiki Wa Kujitegemea wanapewa kufundisha watoto wadogo.
Kumbe huko aliko pitia mpaka hapo walipo mkacha hakuna hao walimu maalumu?

Ukweli ni kwambaaaaa huko waliko mfukuza na pia waliko mkataa wamegundua kuwa tatizo ni MZAZI na siyo mtoto. Kuna mtoto ambaye ujifunzaji wake ni wa taratibu na mwingine ana uwezo mdogo ktk kutunza kumbukumbu, hawa walimu huenda nao vivyohivyo.

Mpaka walimu wamkatae mtoto lazima wamegundua kuwa mtoto ana uwezo wa kufuata na kuelewa maelekezo wampayo ila mzazi ni kikwazo kikubwa,sasa walimu waendelee kulea tatizo wakati na wao ni binadamu, wana hisia?
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule. Ya serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya serikali.
Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.
Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani. Je ni sahihi?
Shule za kulipia walivyokuwa wanamuibia huyo mzazi ukute mtoto alikuwa anapata A's na B's kwa mbaaaaali C. Alafu wasimuonee huyo mtoto amerithi akili za baba yake, kupunguzwa kazini ni ishara ya uwezo mdogo
 
Back
Top Bottom