Louis II
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 3,030
- 4,645
Naangalia TBC1 LIVE mkutano wa taifa wa baraza la kitaifa la biashara ikulu-Dar es Salaam, naona mzee Reginald Mengi amepewa nafasi ya kuongea ila nilichogundua ni kwamba huyu mzee hayuko sawa kimwili na kiakili (kisaikolojia) kama yule Mzee Mengi halisi tuliyepata kumfahamu hapo mwanzo, huyu mzee amekosa kabisa momentum hata ya kuongea akaeleweka kwani anaonekana kana kwamba amedata.
Kwa tuliobahatika kumjua huyu mzee tangu zamani alikuwa ni jembe kwelikweli, alikuwa hodari wa kuongea vizuri tena kwa hoja kuntu lakini hapa namuona anasoma hotuba yake kama mgonjwa au kama mtu aliyeshikiwa bunduki au panga.
Wapendwa ni kipi haswa kimemkumba mzee wetu huyu kipenzi cha wengi?
Kwa mwenye uelewa atupe majibu.