Hivi ni nini kimemkumba mzee wa IPP Media?

Louis II

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
3,030
4,645
Naangalia TBC1 LIVE mkutano wa taifa wa baraza la kitaifa la biashara ikulu-Dar es Salaam, naona mzee Reginald Mengi amepewa nafasi ya kuongea ila nilichogundua ni kwamba huyu mzee hayuko sawa kimwili na kiakili (kisaikolojia) kama yule Mzee Mengi halisi tuliyepata kumfahamu hapo mwanzo, huyu mzee amekosa kabisa momentum hata ya kuongea akaeleweka kwani anaonekana kana kwamba amedata.

Kwa tuliobahatika kumjua huyu mzee tangu zamani alikuwa ni jembe kwelikweli, alikuwa hodari wa kuongea vizuri tena kwa hoja kuntu lakini hapa namuona anasoma hotuba yake kama mgonjwa au kama mtu aliyeshikiwa bunduki au panga.

Wapendwa ni kipi haswa kimemkumba mzee wetu huyu kipenzi cha wengi?

Kwa mwenye uelewa atupe majibu.
 
Nadhani huwa huku anatuma vijana kumsomea na atamtuma JAQC au atakuja kutoa jibu nini kimemsibu japo yawezekana hukumwelewa wewe tu!
 
Pole Mtoa mada. Mimi nimeanza kumfahamu mzee Mengi toka 1987 akiwa anaitwa Mzee mengi nafikiri alikuwa kama 40s na sasa ni miaka 30 bado tunamtaka mengi awe vilevile. Alimaliza CPA 1971 UK. sasa ana umri zaidi miaka 70. Ungetaka aweje sasa.
 
Umeongea kitu mkuu malisoka, tumekuwa watu wa kuwategemea wengine ndio wawepo milele na hii inatuponza.
Mfano utakuta wanasema JPM milele, ukiongelea mpinzani tunadhani ni Mbowe tu milele, ukiongelea muziki unadhani ni ottu jazi na ddc mlimani tu, ukiwaza chama unadhani ni ccm au chadema tu huku tukisahau kuwa muda wa mawanadamu kudeliver na kuwa on top sana sana ni miaka 5 - 10!
Bada;a ya kumshangaa Mengi ni bora tukawaza mbadala kwa nia njema kabisa, mtu mmoja hawezi kuwepo daima.
 
Sure mkuu!! Mimi nilikuwa namsikiliza nikiwa ndani ya gari through TBC Taifa...nilipata na mshangao kwa sauti yake na namna alivyokuwa anaongea. Mimi nilidhani ni mgonjwa, labda nyie mliomuona through TV mnaweza kusema zaidi. Lakini kweli anaonekana leo hakuwa timamu sana.
 
Jua kua huyo ni binaadam na sio samaki kama kila akiwa mkubwa na nguvu zinaongezeka , binaadan kadri umri unavokua mkubwa bas na nguvu zko hupungua
 
Pole Mtoa mada. Mimi nimeanza kumfahamu mzee Mengi toka 1987 akiwa anaitwa Mzee mengi nafikiri alikuwa kama 40s na sasa ni miaka 30 bado tunamtaka mengi awe vilevile. Alimaliza CPA 1971 UK. sasa ana umri zaidi miaka 70. Ungetaka aweje sasa.
Umri sio hoja mkuu.....
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom