Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,088
Wadukuaji wanaiba account za wengine kufanyia shughuli ambazo wanaogopa kuzifanyia kwenye account zao au ndugu zao, shughuli hizi ni:
kuposti picha / video za uchi,
kuposti linki kwenye magroup
kuziuza account,
kuweka link na kuwatag marafiki
kutapeli
kutukana / kudhalilisha watu maarufu,
n.k.
Wao kufanya hizo shughuli wanatafuta account za wengine bila kujali madhara yake, watu wanaweza kukuona muhuni kudhani wewe ndie unapost picha za uchi, unaweza stukia defenda zipo mlangoni unaambiwa umetukana waziri, umetapeli wakulima, n.k.
Hizi ndio mbinu zinazotumika.
1. Kukisia password kwa namba za simu - Watanzania wengi hutumia namba za simu kuwa password kwenye email, facebook na mitandao mingine, mfano mtu ana namba ya simu 0711222333 basi na password anaweka namba hio hio au sehemu ya hizo namba mfano namba sita za mwisho mfano 222333, mdukuzi anaweza kukisia kirahisi akipata namba za simu,
kama na wewe ni moja wao nakushauri ubadili password yako haraka, weka password hata ya jina la mtaa wako unganisha na mwaka uliozaliwa mfano kigamboni1998
2. website feki za facebook zenye sehemu ya kuingiza namba ya simu au email pamoja na password yake, namna rahisi ya kugundua hizi link ni kuangalia anwani zake, utaona zinafanana na facebook.com kwa harakaharaka ila ukichunguza unakuja gundua ni facebook1.com, faceboook.com, facebook.blogspot.com, n.k. hizi link huwa zinaitwa chambo, wewe ukiingiza password unakuwa umevuliwa, namna hizi link zinavyosambazwa unakuta kuna link imewekwa kwenye group au tangazo la facebook inaonyesha picha ya tukio linalovutia wanakwambia uminye ili ucheki video yake au uone picha zaidi, ukiingia hio link kuna ukurasa unakuja unaambiwa uingize user na password, ukiingiza tu zinatumwa kwa mdukuaji, wengine huzituma kwa mfumo wa link za kudanganya utashinda zawadi kirahisi, utashinda vocha, utapewa mkopo, n.k.
chukua tahadhari, ukiingia link ina sehemu ya kukuamuru uingize oassword hakikisha mwanzoni inaanza na facebook.com
3. ukitumia simu au laptop ambayo huimiliki ni hatari kuingiza hata password zako za jamii forums,
hakikisha unapotumia kifaa kisicho chako ukiambiwa save password minya "NO", na usisahau kulogout. lakini bado ni hatari kuna watu wanaweza kuweka software/application za kurekodi password unazoingiza, ni vema utumie simu / laptop yako