Njia 17 za kujilinda na udukuzi wa mtandaoni

Psiteshio72

JF-Expert Member
Nov 13, 2016
634
441
Usije ukalia baadae, useme hukujua.

1. Kama umepokea ujumbe kutoka Kwa mtu unayemuamini sana

Mfano anakwambia Kuna site ya kuinvest na unapata faida kubwa

Cha kwanza FIKIRI.

Pili: usiingie Kwa wakati huohuo

Tatu: fanyia tafiti at least miezi 3

Nne: akuonyeshe yeye kufaulu kwake, kama hakuonyeshi kimbia

2. Strong password

Hakikisha unatumia password strong kama mwamba, Wacha kufanya siku ya Kuzaliwa ndio password

Au 123456

Andika password ndefu, changanya number, herufi na symbols

Hata ikiwezekana weka na emoji


3. Two-Factor Authentication (2FA)

Hii husaidia kuongeza ulinzi. Kwahiyo itabidi uweke password mara 2 kulogin

Pakua app ya 2FA,

Mfano unawekea X app account Yako 2FA nenda settings - password - 2FA

weka password kutoka kwenye hiyo app

Pia backup keys, Incase utapoteza sim

4. Hakikisha una update softwares

Kama anti virus, applications nk ziwe updated

5. Kuwa makini na phishing

Kwanza ogopa kubonyeza links ambazo anayekutumia humjui,

Utalia na kusaga meno.

Unaweza tumiwa pia email inakaa tamutamu,

Hakikisha kabla hujatembelea website husika ni yenyewe na verified

6. Tumia VPN

Epuka kutumia public WiFi, unaweza ibiwa pesa zako.

Hakikisha unatumia VPN kama
• Nord VPN
• Yoga VPN
• HMA VPN

Pale inapobidi.

7. Backup data

Mara Kwa mara uwe una backups taarifa zako Kwa external drive,

Incase taarifa zako zimevuja uweze kuwa nazo Kwa external.

8. Antivirus

Kwenye PC Yako usisahau kuweka antivirus pia ku activate firewall

Kuzuia malware.

(Napendekeza utumie paid antivirus)

9. Monitor accounts

Kwa jicho la karibu fuatilia accounts zako hasa za fedha zetu

Kama hufanyi trading online hakuna mtu ata ku hack bana

Sasa atadukua Nini?

10. Hapa weka passwords Kwa vifaa vyako kama
• Tablets
• Simu
• Laptop

Pia weka tracking apps Kwa vifaa hivyo Incase ilipotea uipate

Find My iPhone Kwa iphone
Find my device Kwa android

11. Downloads

Hakikisha unadownload vitu kutoka official sites

Kuwa makini na cracked softwares, hizo Mimi Huwa naweka humo virus

Kisha narudisha google, achana na vitu vya Bure.

12. Nyumba ikiungua itakuwaje?

Simu na Kila kitu vitakwisha....

Backup photos zako Kwa kutumia google photos

Au tumia telegram ku backup Kila kitu.

13. Tumia private browser kama
• Duckduck go
• Brave nk

14. Communication

Kama unawasiliana na watu na hutaki hata mitandao wajue au Serikali tumia VPN pia tumia apps kama
• Telegram
• Signal nk

15. Turn off location.

Pia cards za banks unazofanya nazo manunuzi online

Hakikisha pesa haitoki mpaka uingize OTP lasivyo itakuwa ni siku ya kiama

16. Je, unapost Nini online?

Kwanza punguza au acha kupost taarifa zako za chumbani online kama Asha,

Huwa hazifutiki, hakikisha unaandika taarifa ambazo hazina uhusiano na mienendo yako

17. Acha kushare taarifa zako sahihi online kama picha upoishi, NIDA, license nk.

Nasemaje, njia nzuri ya kujilinda online ni kutoka online.

Na Kwa bahati mbaya umeshachelewa,

Chukua risk 50% Kwa 50% kuwa makini
png_20240102_130327_0000.jpg
 
Back
Top Bottom