Hivi ndivyo account za facebook zinavyodukuliwa, chukua tahadhari, chunga account yako

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Wadukuaji wanaiba account za wengine kufanyia shughuli ambazo wanaogopa kuzifanyia kwenye account zao au ndugu zao, shughuli hizi ni:

kuposti picha / video za uchi,
kuposti linki kwenye magroup
kuziuza account,
kuweka link na kuwatag marafiki
kutapeli
kutukana / kudhalilisha watu maarufu,
n.k.

Wao kufanya hizo shughuli wanatafuta account za wengine bila kujali madhara yake, watu wanaweza kukuona muhuni kudhani wewe ndie unapost picha za uchi, unaweza stukia defenda zipo mlangoni unaambiwa umetukana waziri, umetapeli wakulima, n.k.

Hizi ndio mbinu zinazotumika.

1. Kukisia password kwa namba za simu - Watanzania wengi hutumia namba za simu kuwa password kwenye email, facebook na mitandao mingine, mfano mtu ana namba ya simu 0711222333 basi na password anaweka namba hio hio au sehemu ya hizo namba mfano namba sita za mwisho mfano 222333, mdukuzi anaweza kukisia kirahisi akipata namba za simu,

kama na wewe ni moja wao nakushauri ubadili password yako haraka, weka password hata ya jina la mtaa wako unganisha na mwaka uliozaliwa mfano kigamboni1998

2. website feki za facebook zenye sehemu ya kuingiza namba ya simu au email pamoja na password yake, namna rahisi ya kugundua hizi link ni kuangalia anwani zake, utaona zinafanana na facebook.com kwa harakaharaka ila ukichunguza unakuja gundua ni facebook1.com, faceboook.com, facebook.blogspot.com, n.k. hizi link huwa zinaitwa chambo, wewe ukiingiza password unakuwa umevuliwa, namna hizi link zinavyosambazwa unakuta kuna link imewekwa kwenye group au tangazo la facebook inaonyesha picha ya tukio linalovutia wanakwambia uminye ili ucheki video yake au uone picha zaidi, ukiingia hio link kuna ukurasa unakuja unaambiwa uingize user na password, ukiingiza tu zinatumwa kwa mdukuaji, wengine huzituma kwa mfumo wa link za kudanganya utashinda zawadi kirahisi, utashinda vocha, utapewa mkopo, n.k.

chukua tahadhari, ukiingia link ina sehemu ya kukuamuru uingize oassword hakikisha mwanzoni inaanza na facebook.com

3. ukitumia simu au laptop ambayo huimiliki ni hatari kuingiza hata password zako za jamii forums,

hakikisha unapotumia kifaa kisicho chako ukiambiwa save password minya "NO", na usisahau kulogout. lakini bado ni hatari kuna watu wanaweza kuweka software/application za kurekodi password unazoingiza, ni vema utumie simu / laptop yako
 
Jamaa wa UNICEF wamekomba accounta kibao na kufanya utapeli..

Bado unakuta account yako inasambaza pornos bila ya kujijua , mtandao ni dhaifu sana kwa kweli
Screenshot_20240211-132053.png
 
Sasa ni Kwa namna gani tunaweza kuepuka huo udukuaji
1. Usi-download ma-file ambayo huyajui kwani yata-install malware kwenye kifaa chako eg computer au simu, na hiyo malware itaiba password na username zako.
2. email zote zinaonekana kama zimetoka facebook, zichunguze kwa makini na usiweka datails zako. Tumia website au app ya Facebook tu.
Kwa kifupi unatakiwa uwe makini muda wote kwani hakuna kuna njia nyingi za kuweza kukudanganya. Ni kama kuishi mjini. Je, unawezaje kujilinda na matapeli na wezi? Jibu ni kuwa hakuna kanuni moja bali unatakiwa uwe mwangalifu. Pia kadiri unavyoishi mjini ndivyo unavyopata uzoefu wa kujua matapeli na wezi na kujilinda. Hivyo hivyo kadiri unavyotumia Internet na kusoma mambo mbalimbali, ndivyo unavyopata uzoefu wa kujikinga na hao hackers.
 
Facebook, Instagram embu tuwaachie watoto wa 2000. Watu wazima tubaki na JF, twitter, Watsup n.k
Watu wengi maarufu waliokuzidi akili, pesa, umaarufu, connection, dhambi n.k wapo huko.

Ila wewe kuwepo hapa kwenye kamtandao kavilaza mnapiga umbea tena kanajulikana Dar na Mwanza unajiona mjanja😂😂😂😂😂

Nikisikia hapa wanapatikana great thinker huwa nacheka sana, Jf ni kundi kubwa la wapiga umbea mtandaoni.
 
UMEPIGA KWENYE PUA MKUU
 
Facebook, Instagram embu tuwaachie watoto wa 2000. Watu wazima tubaki na JF, twitter, Watsup n.k
Dhana potofu hizi

Hivi nani aliyewaambia mitandao fulani ni kwaajili ya umri fulani au watu fulani?

Ushamba tu wa waTanzania kutojua umuhimu na matumizi sahihi ya hii mitandao ndio huko kujifanya mnabagua baadhi ya mitandao.

Facebook&instagram ndio sehemu pekee ambako unaweza kupata marafiki wa kwel, huko ndiko mahala pekee kwa wafanyabiashara na wajasiriamali unaweza kukuza biashara zako na kazi zako, bila kuwasahau wale mafreelancers wanaohusika na baishara za matangazo, programmers, Networking, huko ndiko kuna uhalisia wa maisha na sio hii mitandao ambayo mnajipa upekee na sifa zisizo zenu.

Narudia tena, Tanzania ndio nchi pekee baadhi ya raia wanadhani sifa kutomiliki account Facebook, tiktok, insta, huo ni ushamba wa hali ya juu, njoeni tuwafunze umuhimu wa hii mitandao ikiwezekana tuwape na Pages, accounts, zinazopost habari ambazo huwezi kuzikuta katika hii mitandao mnayoipa sifa.

Badirikeni enyi washamba.
 
Wadukuaji wanaiba account za wengine kufanyia shughuli ambazo wanaogopa kuzifanyia kwenye account zao au ndugu zao, shughuli hizi ni:

kuposti picha / video za uchi,
kuposti linki kwenye magroup
kuziuza account,
kuweka link na kuwatag marafiki
kutapeli
kutukana / kudhalilisha watu maarufu,
n.k.

Wao kufanya hizo shughuli wanatafuta account za wengine bila kujali madhara yake, watu wanaweza kukuona muhuni kudhani wewe ndie unapost picha za uchi, unaweza stukia defenda zipo mlangoni unaambiwa umetukana waziri, umetapeli wakulima, n.k.

Hizi ndio mbinu zinazotumika.

1. Kukisia password kwa namba za simu - Watanzania wengi hutumia namba za simu kuwa password kwenye email, facebook na mitandao mingine, mfano mtu ana namba ya simu 0711222333 basi na password anaweka namba hio hio au sehemu ya hizo namba mfano namba sita za mwisho mfano 222333, mdukuzi anaweza kukisia kirahisi akipata namba za simu,

kama na wewe ni moja wao nakushauri ubadili password yako haraka, weka password hata ya jina la mtaa wako unganisha na mwaka uliozaliwa mfano kigamboni1998

2. website feki za facebook zenye sehemu ya kuingiza namba ya simu au email pamoja na password yake, namna rahisi ya kugundua hizi link ni kuangalia anwani zake, utaona zinafanana na facebook.com kwa harakaharaka ila ukichunguza unakuja gundua ni facebook1.com, faceboook.com, facebook.blogspot.com, n.k. hizi link huwa zinaitwa chambo, wewe ukiingiza password unakuwa umevuliwa, namna hizi link zinavyosambazwa unakuta kuna link imewekwa kwenye group au tangazo la facebook inaonyesha picha ya tukio linalovutia wanakwambia uminye ili ucheki video yake au uone picha zaidi, ukiingia hio link kuna ukurasa unakuja unaambiwa uingize user na password, ukiingiza tu zinatumwa kwa mdukuaji, wengine huzituma kwa mfumo wa link za kudanganya utashinda zawadi kirahisi, utashinda vocha, utapewa mkopo, n.k.

chukua tahadhari, ukiingia link ina sehemu ya kukuamuru uingize oassword hakikisha mwanzoni inaanza na facebook.com

3. ukitumia simu au laptop ambayo huimiliki ni hatari kuingiza hata password zako za jamii forums,

hakikisha unapotumia kifaa kisicho chako ukiambiwa save password minya "NO", na usisahau kulogout. lakini bado ni hatari kuna watu wanaweza kuweka software/application za kurekodi password unazoingiza, ni vema utumie simu / laptop yako
Me yangu ya instagram ishawai kuhakiwa alafu huyo jambazi kaanza kupost picha za wanawake wenye makalio makubwa 🙆🙆🙆🙆
 
Dhana potofu hizi

Hivi nani aliyewaambia mitandao fulani ni kwaajili ya umri fulani au watu fulani?

Ushamba tu wa waTanzania kutojua umuhimu na matumizi sahihi ya hii mitandao ndio huko kujifanya mnabagua baadhi ya mitandao.

Facebook&instagram ndio sehemu pekee ambako unaweza kupata marafiki wa kwel, huko ndiko mahala pekee kwa wafanyabiashara na wajasiriamali unaweza kukuza biashara zako na kazi zako, bila kuwasahau wale mafreelancers wanaohusika na baishara za matangazo, programmers, Networking, huko ndiko kuna uhalisia wa maisha na sio hii mitandao ambayo mnajipa upekee na sifa zisizo zenu.

Narudia tena, Tanzania ndio nchi pekee baadhi ya raia wanadhani sifa kutomiliki account Facebook, tiktok, insta, huo ni ushamba wa hali ya juu, njoeni tuwafunze umuhimu wa hii mitandao ikiwezekana tuwape na Pages, accounts, zinazopost habari ambazo huwezi kuzikuta katika hii mitandao mnayoipa sifa.

Badirikeni enyi washamba.
Well said mkuu
 
Akaunti yangu ya IG imeibiwa mwaka jana...nimejaribu kuirudisha nimeshindwa 😔😔
 
Back
Top Bottom