Hivi maisha bila kuvaa nguo ingekuwaje?

Hivi maisha bila kuvaa nguo ingekuwaje?

Hawa hua hawaogi?
Mbona miili sio safi

Mambo yetu ya kujipulizia manukato kuonga mara mbili kwa siku, kuvisha wake zetu mzigo wa maguo, kuficha nyuso n.k watu hawa huru kabisa kifikra hawana, maana na bado wanazaana na kutengeneza familia huku wakiheshimiana wakubwa kwa wadogo, vijana kwa wazee na wanaishi fresh kabisa bila kesi za kubaka wala nini na hakuna tamaa za kimwili nje ya ndoa
 
Mambo yetu ya kujipulizia manukato kuonga mara mbili kwa siku n.k watu hawa huru hayana maana na bado wanazaana na kutengeneza familia huku wakiheshimiana wakubwa kwa wadogo, vijana kwa wazee na wanaishi fresh kabisa bila kesi za kubaka wala nini
Aiseee sema kwa vile wamezoeana hakuna tofauti hapo duh
 
Mkuu huu sio unyanyapaa kweli
Mbona kama unazidisha?
Siyo unyanyapaa mkuu
Nguo ziheshimiwe, unajua zinawafinyanga sana ma female...unaweza kuta mwanamke nguo zimemkaa, mkiingia ndani kuna vitu vinaporomoka kifuani mara kwenye matumbo howaaa paraaa

Ukianza kuvunja amri ile, unavuta hisia kama vile unavuta sigara dawa!
 
Nimetoka kuoga wakati napaka Lotion nilikua mbele ya kioo gafla nikajiona kwenye kio nikiwa mtupu

Hapo hapo nikajiuliza hivi ingekuaje kama tungekua tunatembea utupu bila nguo hivi maisha yangekuaje?

Nikajiuliza pia hivi ni nani alipata wazo la kuvaa nguo

Aliwaza nini ?
Ni baridi kali ilimsukuma?
Au jua kali kupita kiasi?
Au aibu ?
Kama ni aibu alijuaje hii ni aibu ?

Maana kwa viumbe hai nadhani mwanadamu ndio anavaa nguo

Mada yangu naigawanya sehemu mbili wewe mdau utajibu upande unaopenda
👇

Mtazamo wa kidini

Kwa mujibu wa Biblia, baada ya Adamu na Hawa kula tunda walilokatazwa, wakafumbuliwa macho wote wawili, wakajua kuwa wako uchi wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo (Mwanzo 3:7)

Baadaye Adamu akasema:

Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha (Mwanzo 3:10)

Hapo tunaona Adamu alikua akiishi mtupu na hakuwahi kugundua kua alikua mtupu alikua kawaida

Baada ya kula hilo tunda ndio akagundua kua yupo uchi yeye na Hawa

Swali la kujiuliza kama Adam aligundua kua yupo uchi baada ya kula tunda

Hii ina maana mwanzo hakujua chochote na alikua akiishi mtupu

Je huko kwenye bustani ya Edeni hakukua na baridi?
Kama lilikuepo mbona hakusikia?
Je hakukua na jua kali ?
Kama lilikuepo mbona hakulisikia?

Au kulikua na mazingira rafika kwa kuishi mtupu?

Je, simulizi hili linaonyesha kwamba desturi ya kujisitiri ilianza hapo, au ni fundisho la kiroho kuhusu dhamiri ya mwanadamu?


Mtazamo wa kifalsafa 👇

JE , nguo ni matokeo ya akili ya mwanadamu kutafuta ulinzi dhidi ya baridi, jua na mazingira, au ni makubaliano ya kijamii kuhusu staha na utambulisho?

Leo utasikia mtu wa kwanza kugundua simu ni fulani

Aliegungua radio ni fulani

Hivi ni nani wa kwanza aligundua kwamba watu wavae nguo badala ya kutembea watupu?

Kama tungekuwa kama wanyama wengine wasiovaa nguo, je, maadili na maisha ya jamii yangekuwaje?

Yaani tuwe kama ng'ombe , Mbuzi ,
Au wanyama wa mwituni

Yaani tungekua tunapeta naked ingekuaje😅🙌

ShesRise_1 ✋️
Tungekua kama wanyama wengine tu, kusingekua na jipya....
 
Umesema uchumi kwenye sekta ya nguo
Na mi nikauliza uchumi utaporomoka vipi na wakati haujawahi kuwepo

Ni kama kusema kwamba uchumi kwa ufugaji panya umeteteleka na wakati haujawahi kuwepo

Au wewe ulikua na maana gani?
Mkuu nilimaanisha kuwa disrupted nikiwa na maana kwamba mabadiliko makubwa ya allocation of resources (Ugawaji wa Rasilimali).

Sasa hivi, asilimia kubwa ya ubunifu wa binadamu na mtaji umekwama kwenye fashion & textiles kama tusingekuwa na hivyo viwanda, hiyo mental energy na capital ambayo sasa hivi inaenda kwenye kushona nguo, ingeenda wapi?

Hii ndio tunaita opportunity cost, kutokuwepo kwake uchumi usingesimama, lakini hali ingekuwa tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom