Jinsi ya Kutoa Madoa Sugu kwenye Nguo Nyeupe

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,965
Nguo nyeupe kuwa na doa kama la nyanya, matope au umejimwagia soda huwa inakera sana. Lakini usiwe na wasiwasi mimi hutumia mbinu hizi kuondoa madoa bila stress. Twende pamoja;

Kwanza epuka kutumia maji ya moto kwenye nguo nyeupe zenye madoa yenye protini ndani yake (kama damu, jasho, maziwa, mayai) au madoa magumu (kama mchuzi wa nyanya na mvinyo) yana tabia ya kugandiana na nyuzi za nguo yakikutana na joto kali. Ukitumia maji ya moto kwenye doa jipya, unakuwa umelipika na kuligandisha moja kwa moja kwenye nguo yako—halitatoka tena! Anza na maji baridi kila wakati.

Unachohitaji:
  1. Baking Soda.
  2. Limao (kama limao kavu, unaweza tumia siki—vinegar).
  3. Nguo yenye doa.
  4. Kijiko cha kuchanganyia na bakuli dogo.
  • Hatua ya 1: Chukua bakuli lako. Weka vijiko viwili vya baking soda. Kamulia limao mpaka utengeneze rojo nzito, inayoweza kutosha kufunika doa. Unaweza ongeza baking soda au limao kidogo kulingana na ukubwa wa doa.

  • Hatua ya 2: Paka rojo hii nzito moja kwa moja kwenye doa lile sugu. Hakikisha umefunika doa lote. Unaweza kutumia kijiko au kidole chako kupaka. Ikiwa doa ni kali, paka kwa pande zote mbili za nguo.

  • Hatua ya 3: Acha nguo ikae na rojo hiyo kwa muda wa dakika kumi na tano (15) hadi nusu saa (30). Kwa madoa sugu zaidi, acha ikae kwa masaa machache. Rojo hii itaendelea kufanya kazi yake na kuvunja chembechembe za doa.

  • Hatua ya 4: Baada ya muda kuisha, fua nguo yako kama kawaida, ukitumia sabuni yako ya unga au ya kioevu. Kisha anika nguo yako juani na sio kwenye air dryer
Pia unaweza kukamulia ndimu moja kwa moja kwenye lile doa, weka chumvi kiasi kwa juu, kisha tumia kidole chako kusugua kwa mwendo wa duara. Iache ikae kwa dakika 10 ili inyonye yale mafuta kabla ya kusuza.

Kama una njia nyingine unaweza kucomment wadau waokote madini
 
Doa la utomvu linatokaje
 
Back
Top Bottom