Hivi maisha bila kuvaa nguo ingekuwaje?

Hivi maisha bila kuvaa nguo ingekuwaje?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
17,748
Reaction score
42,222
Nimetoka kuoga wakati napaka Lotion nilikua mbele ya kioo gafla nikajiona kwenye kio nikiwa mtupu

Hapo hapo nikajiuliza hivi ingekuaje kama tungekua tunatembea utupu bila nguo hivi maisha yangekuaje?

Nikajiuliza pia hivi ni nani alipata wazo la kuvaa nguo

Aliwaza nini ?
Ni baridi kali ilimsukuma?
Au jua kali kupita kiasi?
Au aibu ?
Kama ni aibu alijuaje hii ni aibu ?

Maana kwa viumbe hai nadhani mwanadamu ndio anavaa nguo

Mada yangu naigawanya sehemu mbili wewe mdau utajibu upande unaopenda
👇

Mtazamo wa kidini

Kwa mujibu wa Biblia, baada ya Adamu na Hawa kula tunda walilokatazwa, wakafumbuliwa macho wote wawili, wakajua kuwa wako uchi wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo (Mwanzo 3:7)

Baadaye Adamu akasema:

Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha (Mwanzo 3:10)

Hapo tunaona Adamu alikua akiishi mtupu na hakuwahi kugundua kua alikua mtupu alikua kawaida

Baada ya kula hilo tunda ndio akagundua kua yupo uchi yeye na Hawa

Swali la kujiuliza kama Adam aligundua kua yupo uchi baada ya kula tunda

Hii ina maana mwanzo hakujua chochote na alikua akiishi mtupu

Je huko kwenye bustani ya Edeni hakukua na baridi?
Kama lilikuepo mbona hakusikia?
Je hakukua na jua kali ?
Kama lilikuepo mbona hakulisikia?

Au kulikua na mazingira rafika kwa kuishi mtupu?

Je, simulizi hili linaonyesha kwamba desturi ya kujisitiri ilianza hapo, au ni fundisho la kiroho kuhusu dhamiri ya mwanadamu?

Mtazamo wa kifalsafa 👇

JE , nguo ni matokeo ya akili ya mwanadamu kutafuta ulinzi dhidi ya baridi, jua na mazingira, au ni makubaliano ya kijamii kuhusu staha na utambulisho?

Leo utasikia mtu wa kwanza kugundua simu ni fulani

Aliegungua radio ni fulani

Hivi ni nani wa kwanza aligundua kwamba watu wavae nguo badala ya kutembea watupu?

Kama tungekuwa kama wanyama wengine wasiovaa nguo, je, maadili na maisha ya jamii yangekuwaje?

Yaani tuwe kama ng'ombe , Mbuzi ,
Au wanyama wa mwituni

Yaani tungekua tunapeta naked ingekuaje😅🙌

ShesRise_1 ✋️
 
Moral of the story;
Screenshot_20260705-191432~2.jpg
 
mwanamke wangu hapendi kuvaa nguo, angekuwa ana enjoy sana, hhaha
 
Back
Top Bottom