Pasi ya maji hulinda nguo zako na kuzitoa smart kuliko pasi kavu, pasi za maji sio mbovu, zitumie kwa namna hii na hutafikiria tena kutumia pasi kavu

Pasi ya maji hulinda nguo zako na kuzitoa smart kuliko pasi kavu, pasi za maji sio mbovu, zitumie kwa namna hii na hutafikiria tena kutumia pasi kavu

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
2,495
Reaction score
7,506
Watu wengi wamekariri kutumia pasi kavu bila kujua zinachangia pakubwa kuharibu nguo zao

Pasi kavu huchosha kitambaa, huchosha nyuzi na fabrics, huondoa mwonekano mzuri wa nguo na kufanya zifubae mapema. Ndio maana mara nyingi utaona nguo za mtumba zimetumika miaka mingi huko zilipotoka lakini bado zinaonekana nadhifu na zenye ubora mkubwa. Lakini zikifika huku baada ya muda mfupi zinabadilika haraka na kupoteza mvuto wake.

Sababu kubwa ni kwamba wenzetu hutumia zaidi pasi za maji ambazo hulinda kitambaa, huhifadhi rangi na kufanya nguo zidumu muda mrefu zaidi. Kama unataka nguo zako zidumu, zibaki smart na zionekane mpya kwa muda mrefu, anza kutumia pasi za maji badala ya pasi kavu. (pia tumia sabuni nzuri kama omo na pendelea kuloweka kwanza)

Watu wengi wanaogopa kutumia steam iron kwasababu ya kuogopa zinavyovuja, kuziba, n.k. Kumbe ni rahisi sana ukijua hatua zake.

Hakikisha pasi haijachomekwa kwenye umeme

Weka maji hadi kwenye alama ya FULLau MAX

Hakikisha kitufe cha mvuke kimezimwa ili pasi isitowe mvuke kwanza

Zungusha kidude cha joto mpaka juu kabisa mwanzo. Hii husaidia maji yachemke vizuri. kwasababu Maji yasipochemka vizuri, pasi nyingi huanza kuvuja maji badala ya kutoa mvuke.

Baada ya hapo:
Chomeka pasi kwenye soketi

Subiri taa nyekundu izime - taa ikiwa imewaka maana yake bado inapasha moto. Ikizima au kwa pasi nyingine kubadilika rangi ndiyo pasi ipo tayari kutumika.

Sasa unaweza kupunguza joto kulingana na nguo mfano mashati laini utapunguza kidogo, ila vitambaa vigumu acha joto la juu

Hapo unaweza kuwasha sasa kitufe cha kutoa mvuke kwa mtiririko pamoja na kutumia steam burst ambayo huwa inapiga chafya ya mvuke


Ukimaliza mwaga maji yote, Usibakize maji kwa muda mrefu maana maji hasa ya bomba yana kemikali zinazoweza kuganda ndani ya pasi na kuziba sehemu za mvuke.

zima kitufe cha mvuke mtiririko, Acha pasi ipoe ikiwa imesimama vizuri

Steam iron ukijua kuitumia vizuri, nguo zinatoka smart sana kuliko dry iron ya kawaida 🔥
 
Uziri wa pasi ya maji inanyoosha nguo ya aina yoyote,hata zile zisizonyoosheka kwa pasi kavu, pia unatumia muda mchache sana kunyoosha nguo,ukipitisha mara moja upande unaoonyosha unakuwa umeshakaa sawa,haina kurudia rudia kama pasi kavu,hainguzi nguo,ina save umeme kutoka a na kutumia muda mchache kunyoosha nguo ,pia haipashu nguo
 
Back
Top Bottom