Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Kwa hivyo unakubali kwamba ulikuwa umedandia treni kwa mbele kufikiri napinga uwepo wa Mungu kwa sababu siwezi kumgusa wakati hata huelewi sababu zangu za kupinga uwepo wa Mungu?
Hakuna mtu mwenye akili timamu na mwenye macho ya kuuona ulimwengu na yale yaliyomo na masikio ya kusikia akaja na hoja ya aina yoyote ile ya kupinga uwepo wa Mungu. Ndiyo maana nadhani unahitaji msaada zaidi
 
Hapa ndipo shida inapoanzia. Kwa hiyo swala ni milango mitano ya fahamu? Kama aliyekutengeneza aliamua kuopt kukuacha na milango mitano ya fahamu, vipi kama kuna mlango wa sita, saba, nane..... hiyo mingine iliyopo unaifahamu? Sasa kama issue kama hiyo hauna majibu yake, unathubutu vipi kumhoji huyo aliyeamua iwe hivyo? Wewe unajua yeye amebaki na milango mingapi?
Sijasema swala ni milango ya fahamu , soma kwa ufahamu, kulingana na nilichokujibu ama kukuuliza , Mimi nakuambia Mungu ni dhana tu hayupo na wala hawezi kuwepo , kutokana na mikanganyiko ndani ya vitabu vya dini na utofauti wa tabia za Mungu ndani ya jamii mbalimbali ,inathibitisha Mungu ni nadharia ya kimapokeo tu , yani kila jamii iliposhindwa kupata majibu ya maswali yao walitengeneza hii nadharia kulingana na Mila zao na tamaduni zao.
 
Ukifungua tu macho na kutazama wala hauna haja ya kuhoji kama yupo au hayupo! Jibu lipo wazi kabisa! Kuhusu utendaji wake hizo na akili na makusudi yake ambayo siwezi kuhoji!
Maneno hayo ni ya kiimani tu hakuna hata dalili ya uwepo wa Mungu muweza wa yote.
 
Iko hivi mkuu mimi naipenda sayansi na ninaijua kiasi chake, mapungufu ya sayansi ni kwamba bado kuna vitu vingi haijavigundua.

Hivyo, sayansi haiwezi kuthibitisha kutokuwepo kwa Mungu ila haikubaliani na uwepo wake lakini weka kwenye akili kwamba science sio absolute ni bado ina safari ndefu ya kugundua vitu vingi.
Sayansi haiwezi kuthibitisha uwepo wa Pazi aliyebebwa na jogoo, Superman, Spiderman, Unicorn, Hulk nk.

Lakini haina maana Sayansi kushindwa kwake kuthibitisha kunahitimisha kuwa hao character wapo in reality.

Hata wewe huwezi kuthibitisha kuwa kijana wa miaka 20 ana mama yake mzazi mwenye miaka 2. Yani mtoto kuwa na umri mkubwa kuliko mama yake mzazi.

Kushindwa kwako kuthibitisha hakuna maana mtoto huyo pamoja na mama yake wapo.
 
Mkuu hapo unapoteza muda wako bure tu
Huyu ni KIPOFU wa imani, logic haina nafasi kabisa kwenye akili yake anapojadili habari za Mungu wake

Hawa wana kelele nyingi sana lakini mara paap, ukimchomekea mtu kiswali kidogo tu kama hicho, mtu anapotea.

Kama ni mtupu hivyo, na huo nao ni ushahidi kwamba Mungu hayupo.

Angekuwapo asingeumba kiumbe mwenye fikra dhaifu hivyo.
 
Maneno hayo ni ya kiimani tu hakuna hata dalili ya uwepo wa Mungu muweza wa yote.
Hii dunia unayoishi ipo kiimani? Hizo nyota zipo kiimani? Jua na mwezi vipo kiimani? Mifumo yote ya ecolojia na uhai ipo kiimani?
Au unadhani vilitokea tokea tu?
 
Hii dunia unayoishi ipo kiimani? Hizo nyota zipo kiimani? Jua na mwezi vipo kiimani? Mifumo yote ya ecolojia na uhai ipo kiimani?
Au unadhani vilitokea tokea tu?
Kama huyo Mungu anaweza kuwepo tu hata vyote hivyo vinaweza kuwepo tu bila chanzo .
 
Ni sawa na wewe na mke wako then aanzishe uhusiano uliosawa na wa kwako kwa mwanaume mwingine.

Tafsiri utayoipata moyoni mwako ndio hiyo iliyomaanishwa kwenye hayo maandiko, halafu upime mwenyewe kama ni sawa au si sawa.
Word
 
Kiufupi: mtu akikwambia nakupenda ila sina wivu na wewe ujue umepigwa
 
Waislam wao Mungu wao ni MMOJA TU, hana mshirika, hajazaa wala hajazaliwa na Hafanani na kitu chochote.
Kwa maana hiyo, Wakristo Mungu wao ni mwingine kwani hana sifa hizo
 
Ulimwengu wa roho hautumii fact na logic za kisayansi. Unatumia fikra, hisia na mambo yasiyoweza thibitishwa kwa kutumia logic.

Kuna logic ya maria kupata ujauzito bila mbegu za mwanaume? Ndo maana nakuambia FIKIRI. Ukifikiri hutotutumia nguvu na kamwe hutojadili kuhusu uwepo wa MUNGU nje ya masuala ya imani.
Unazidi kupanua wigo wa mambo ambayo huwezi kuyathibitisha kivyovyote vile , kama unakataa thibitisha uwepo wa roho na mwanamke kujifungua mtoto bila kufanya ngono kwa kutumia hizo fikira na hisia ambazo hazifuati logic.
 
Hiyo Oksijeni tu unayovuta ni kithibitisho tosha
Oksijeni ipo.

Thibitisha Mungu yupo.

Sio kuunganisha vitu vilivyopo na kutaka kuvi husishanisha na Mungu asiyekuwepo.

Oksijeni haina uhusiano wowote ule na uwepo wa Mungu.
 
Sasa kama ww kiumbe ulieumbwa kwa mfano wake una wivu, huoni kama na yeye lazima awe na wivu, tena alisema mwenyewe kuwa ana wivu
 
Back
Top Bottom