Mungu amejibu swali lako kupitia kitabu cha Quran kwa kusema kuwa lau kama angelitaka basi angelituumba sote kuwa umma mmoja.
Ila hakutaka liwe hivyo kwasababu ameyafanya maisha haya ya duniani kuwa ni mtihani kwa kila mwanadamu ili aone ni nani atakayemuamini kikweli na kisha akatenda mema.
Pia ni sawa useme kwanini Mungu hajatuumba wanaadamu wote kuwa na sura moja,urefu sawa,akili sawa,lugha moja,rangi moja ,jinsia moja,umri sawa wa kuishi hapa duniani n.k?! Jibu ni kuwa hakutaka iwe hivyo lau angelitaka basi angelifanya kuwa hivyo.
Ila ameyaweka maisha ya duniani kuwa ni mithili ya chumba cha mtihani. Kila mtu anapewa mtihani wake, atajaza majibu yake anayoyataka kupitia imani atakayoichagua pamoja na vitendo vyake atakavyoamua kuvitenda....mwisho wa siku huu mtihani huwa na muda maalumu ambao ni uhai. .ukiisha ndio Kifo huwa kimefika, unakusanywa kwa ajili ya kwenda kusahihishwa na kisha mwisho washindi na waliofeli watatangazwa siku ya Hukumu