Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Wataalamu wa bibilia, nakumbuka kuna siku nilisoma hicho kitabu nikaona historia ya mnara wa babeli Mungu aliposhuka na kuwakuta binadamu wanatengeza ule mnara alishtuka na kuwatenganisha kwa lugha pamoja na maeneo ndiyo yakazaliwa mataifa mengine.

Tukio la pili kwenye sura ya mwanzo Mungu baada ya adamu kula ule mti ambao alikatazwa inaonekana ibilisi alikuwa anajua siri ya mti huo wa uzima japo hakuufahamu haswa ni upi ila baada ya Mungu kuona binadamu na jeshi lake watapanga kuutafuta ndiyo akauficha, nimesahau exactly ni wapi.

Case ya tatu, baada ya kuwatoa Wanaisraeli kupitia Mtume wake Musa aliwaambia kuwa yeye ni Mungu mkuu na anawivu hivyo wasiabudu mwengine isipoikuwa yeye.

Je, kwa kauli ya kusema kuna miungu mengine anafahamu kuwa kuna nguvu nyengine tofauti na yeye?

Je, hajiamini na nguvu zake?

Je, Mungu huyu ni tunayemuabudia wakristo na waislamu?

Je, ni binadamu wa mwanzo ambaye aliwahi kutambua siri za ulimwengu na akajitahidi kuzificha na hatimaye akajitolea taji la uungu?

Nawasilisha.
Kwa kibinadamu 'wivu' ni hisia zinazozalishwa baada ya kupigwa tukio, kwa mfano utakapokiona kinyago ulichokifinyanga ama kinyago cha mpapure ulichokichonga kwa mikono yako kinaanza kuvimba ndani ya nyumba na kukuletea za kuleta.

Kinyago ulichokifinyanga kwa madhumuni let say ya mapambo ya sebule, leo unakuta kimeshuka na kwenda jikoni kula misosi ambayo mama alikuwekea.

Wakati kinyago hicho haujashea na mtu kukifinyanga, ulikibhumba mwenyewe peke yako na kwa utashi wako.

Je utapoanza kuona kimeanza kujitambua na kukusumbua ama kujilinganisha na wewe, si utakivunja vunja kirudi kwa udongo na habari iishie hapo?
 
Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Mungu wa kwenye Biblia na maandiko yote ya kidini ni Fictional character sawa na Abunuwasi wa kwenye Hekaya.

Mungu ana ongelewa na binadamu kwa vile Hayupo kujiongelea mwenyewe..
 
Kwa kibinadamu 'wivu' ni hisia zinazozalishwa baada ya kupigwa tukio, kwa mfano utakapokiona kinyago ulichokifinyanga ama kinyago cha mpapure ulichokichonga kwa mikono yako kinaanza kuvimba ndani ya nyumba na kukuletea za kuleta.

Kinyago ulichokifinyanga kwa madhumuni let say ya mapambo ya sebule, leo unakuta kimeshuka na kwenda jikoni kula misosi ambayo mama alikuwekea.

Wakati kinyago hicho haujashea na mtu kukifinyanga, ulikibhumba mwenyewe peke yako na kwa utashi wako.

Je utapoanza kuona kimeanza kujitambua na kukusumbua ama kujilinganisha na wewe, si utakivunja vunja na habari iishie hapo?
nimesema wivu sio kinyongo na mtu mpaka awe na hicho kinyongo huwa akili yake haipo katika kufanya kazi.
 
kwani ukichukua sura yangu,yako na wengineo unaweza kujua au kufahamu ukubwa,rangi,nafasi,idadi ya SURA yake?

me najua kuwa kasema hivyo kwa sababu hafananii kwa mfano wetu wa sura wala tabia ila mungu labda tuawmw ni nguvu untouchable,invisible,unseen but you can feel it by your subconscious mind.
Uko sawa, naposema mtu aliumbwa kwa mfano wa mungu namaanisha mtu(nishati).
Huu mwili wa nyama ni chombo tu sio mtu, hivyo alivyosema alimuumba mtu kwa sura na mfano wake ni hiyo nishati.(hata biblia imeeleza tunaona baada ya kumfanya mtu kwa mfano wake kisha aliwekwa katika mwili, Adam).

Asili ya mtu ni Mungu, na asili ya mwili ni ardhi(earth), hizi sura zetu za kimwili ni matokeo ya vizazi na vizazi toka mtu wa kwanza kuepo hadi sasa na zinatofautiana kulingana na mabadiliko ya genes zinazosababishwa na mazingira.
Mazingira yanapelekea kuundwa kwa asili fulani lakini haimaanishi yanabadili uhalisi, hivyo tuna miili ya mifano na sura tofauti kulingana na asili zetu ila kiuhalisi tuko mtu mmoja ambaye ametokana na chanzo kimoja (God).
 
Hakuna mungu aliyeumba binadamu.

Binadamu ndio wameumba dhana ya kufikirika na kuiita mungu.
Je neno Mungu linamaana gani kwako?

Chanzo cha mtu ni nini?

Muundo wa mtu ni upi?

Naomba unisaidie nielewe majibu ya hayo maswali mkuu.
 
Kutokuwepo kwake ni uthibitisho tosha kwamba hayupo.

Na hawezi kuthibitishika kwa namna yoyote ile kwamba yupo.

Huu ni uthibitisho tosha kwamba Mungu hayupo.
Nimeomba unithibitishie kuwa hayupo, wewe unasema hawezi kuthibitika na kwamba huo ni uthibitisho tosha. Sasa hapo mbona bado hijaeleweka mkuu.
 
Nimeomba unithibitishie kuwa hayupo, wewe unasema hawezi kuthibitika na kwamba huo ni uthibitisho tosha. Sasa hapo mbona bado hijaeleweka mkuu.
Unataka uthibitisho wa kitu ambacho hakipo?

Labda unataka uthibitisho wa namna gani?

Maana kitu chenyewe unachotaka nikupe uthibitisho hakipo.

Kisichokuwepo hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika kwamba kipo.

Una elewa hilo?
 
Nimeomba unithibitishie kuwa hayupo, wewe unasema hawezi kuthibitika na kwamba huo ni uthibitisho tosha. Sasa hapo mbona bado hijaeleweka mkuu.
kitu hakipo unakithibitishaje?ebu wacha ujinga basi.
 
Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Mungu wa kwenye Biblia na maandiko yote ya kidini ni Fictional character sawa na Abunuwasi wa kwenye Hekaya.

Mungu ana ongelewa na binadamu kwa vile Hayupo kujiongelea mwenyewe..
Fictional character maana yake ni kutokuwepo?
 
Back
Top Bottom