Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Elimu gani inayofundisha mungu anatengeneza oksijeni na mvua. Kama wewe hiyo elimu unayo tuelekeze anatengenezaje vitu hivyo.
Simply Science explains how things work! Na vile jinsi vinavyofanya kazi ndivyo yeye aliyeziumba na kuziset ili zifanye kazi anajidhihirisha! Yeye ndiye kaweka hayo madude makubwa angani, Jua nyota zote, galaxies n.k na ye ndiye chanzo cha uhai. Sasa kama umesoma scince sina haja ya kuleza zaidi
 
Meditation haina uhusiano na mambo ya simba wa yuda , wala Meditation haikufanyi uone kuna kiumbe kina kupa nguvu , mkuu bado wewe ni lena ,ila sio kwa ubaya lakini.
😅😅
Mkuu achana naye huyo 😀😀
 
Kwa hiyo vimejitokea tu vyenyewe?

Aliyekuumba na kuprogram akili yako ameiwekea limits kuweza kufahamu mambo yaliyo katika level yake.Sasa unataka ulazimishe wakati akili yako hailingani wala kufikia level yake? Uko na rubberband alafu unataka uvute utanue ukubwa wa mto Nile?!
Wewe umejuaje mambo hayo?
 
Hiyo ni sayansi gani na ya wapi ambayo imefikia hitimisho la kwamba kuna master alieseti kila kitu?
Unahoji kama nani? Mwanasayansi uliyefanya research zako ukaja na alternatives au kama mbulula? Hata BIG BANG theory unaijua? Nini chanzo cha kila kitu?
 
Wataalamu wa bibilia, nakumbuka kuna siku nilisoma hicho kitabu nikaona historia ya mnara wa babeli Mungu aliposhuka na kuwakuta binadamu wanatengeza ule mnara alishtuka na kuwatenganisha kwa lugha pamoja na maeneo ndiyo yakazaliwa mataifa mengine.

Tukio la pili kwenye sura ya mwanzo Mungu baada ya adamu kula ule mti ambao alikatazwa inaonekana ibilisi alikuwa anajua siri ya mti huo wa uzima japo hakuufahamu haswa ni upi ila baada ya Mungu kuona binadamu na jeshi lake watapanga kuutafuta ndiyo akauficha, nimesahau exactly ni wapi.

Case ya tatu, baada ya kuwatoa Wanaisraeli kupitia Mtume wake Musa aliwaambia kuwa yeye ni Mungu mkuu na anawivu hivyo wasiabudu mwengine isipoikuwa yeye.

Je, kwa kauli ya kusema kuna miungu mengine anafahamu kuwa kuna nguvu nyengine tofauti na yeye?

Je, hajiamini na nguvu zake?

Je, Mungu huyu ni tunayemuabudia wakristo na waislamu?

Je, ni binadamu wa mwanzo ambaye aliwahi kutambua siri za ulimwengu na akajitahidi kuzificha na hatimaye akajitolea taji la uungu?

Nawasilisha.
Kama mti ule wenye lile tunda ulikuwa ni mti wa utambuzi wa mema na mabaya na wakala, basi dunia hii kuna wachache wanajua meya ya huu ulimwengu na mabaya yake... Kwamaana hiyi siri zimhusuyo mungu zajulikana
 
what is ngapi? Unazungumziaje dimensions za kibinadamu unapomzungumzia Mungu? What is IQ? Hayo mambo ya kwenye maisha ya mwanadamu ambayo umezaliwa umeyakuta unadhani ndiyo yaliyopo kwenye dimensions za Mungu? Alafu bado unaamini kwa akili hizo ndiyo upate majibu ya akili za Mungu


*Alafu unapoandika neno Mungu anza na herufi kubwa

-Nianze na heri kubwa kwa sababu gani.
-Dimesion za mungu zikoje na wewe umezijua vipi.
 
Bado una ufahamu mdogo sana alafu unataka kutumia akili yako kuhoji akili ya Mungu wakati hata uwezo wa kutambua namna nyepesi ya ufahamu wa viumbe hai hauna! Wewe na Ng'ombe nani mwenye akili? Kwa hiyo hayo maneno angeongea ng'ombe kwamba yeye ndiye mwenye akili zaidi ya binadamu na hana limitation angekuwa sahihi? Hauna hata akili ya kutengeneza uhai wa mdudu, alafu unajidai kuhoji akili zilizotumika kuweka kila kitu mahala pake! Nadhani unahitaji msaada zaidi
Religion's emotions at work.
 
Kila kitu hakipo kwa bahati mbaya! Bali ni mifumo ambayo sayansi inaeleza wazi namna inavyofanya kazi na chanzo cha hayo yote ni Nguvu kubwa iliyopo nyuma yake ambayo ni Mungu.
Ni nini kinakufanya ufanye hitimisho kwamba ni mungu na kwa mantiki hiyohiyo kwamba vitu havijatokea kwa bahati mbaya, je nini kimetengeneza hiyo mungu.
 
Unataka uthibitisho wa mambo wanayoamini wasio na akili. Kazi ipo.
Nilikuwa namanisha hayo ni mahubiri yanayofatwa na vipofu wa akili. Bila kuwa na maneno mengi thibitisha uwepo wa mungu.
 
Simply Science explains how things work! Na vile jinsi vinavyofanya kazi ndivyo yeye aliyeziumba na kuziset ili zifanye kazi anajidhihirisha! Yeye ndiye kaweka hayo madude makubwa angani, Jua nyota zote, galaxies n.k na ye ndiye chanzo cha uhai. Sasa kama umesoma scince sina haja ya kuleza zaidi

-Kwanini unampa personality ya uyeye na si vinginevyo, ina maana ni mtu?
-umejuaje kwamba yeye aliumba vitu hivyo na kuviseti?
-yeye aliumbwa na kitu gani?
 
Nilikuwa namanisha hayo ni mahubiri yanayofatwa na vipofu wa akili. Bila kuwa na maneno mengi thibitisha uwepo wa mungu.
MUNGU yupo sababu unamfahamu na kuulizia habari zake. Kama hayupo usingefahamu lolote kumhusu.
 
Kwa sababu uwepo wake hauthibitishiki kwa namna yoyote ile. Kama mungu yupo thibitisha yupo.
Kumzungumza tu ni uthibitisho wa uwepo wake. Kitu kisichokuwepo popote hakifikiriki. Huwezi kukitaja, hakipo kwenye ulimwengu halisi wala wa fikra. Ndo maana huwa nakuuliza, maana ya kutokuwepo ni nn?
 
Back
Top Bottom