Kuna uhusiano gani kati ya kua na mawazo ya kimasikini na kutokuwa na vipaumbele katika maisha au ni elimu ndogo katika jamii?

VINICIOUS JR

Member
Dec 29, 2022
60
196
Kwema wakuu. Kama mada inavyojieleza, umekuwa na tabia ya watu katika jamii zetu kufanya maamuzi flani bila kujua ni maamuzi sahihi kwa wakati sahihi au kipi kianze au kipi kifate.

Mfano unakuta mwanaume anaoa wakati hajejipanga vizuri (kiuchumu) kimaisha matokeo yake kipato kinachopatikana ni hand to mouth, anakua na watoto wengi ambao kimsingi hawatimizii mahitaji yao muhimu ipasavyo sababu ikiwa ni kipato duni ukilinganisha na uhitaji wa familia.

Pia kuna mfano wa kweli kabisa ambapo kuna graduate wa chuo x mwaka 22 baada ya kuhitimu masomo kaja mtaani akaoa wakati hajejipanga vizuri mwisho wa siku kamtelekeza binti akiwa na mimba yemwenyew kaenda kuishi mkoa mngne kwa madai anaenda kutafuta hela wakati kwa mke wake hela hatumi na mke karudi kwa wazazi.

Je ni muhimu kuzingatia vipaumbele katika maamuzi tunayofanya bila kukurupuka? Karibu kwa maoni.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom