Sintofahamu ya siasa za ndani nchini Marekani ni chanzo kikuu cha wasiwasi wa uhusiano wa China na Marekani katika siku zijazo

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG211278538862.jpg


Mwelekeo wa uhusiano kati ya China na Marekani umewekwa wazi katika masuala ya kulegeza, kutuliza na kurejesha uhusiano huo. Jamii ya kimataifa ina matumaini kuwa, uhusiano kati ya nchi hizi mbili kubwa kiuchumi duniani utatulia, na utasonga mbele badala ya kurudi nyuma, kwani utulivu wa uhusiano kati ya nchi hizi mbili ni matarajio ya dunia nzima.

Mpaka uhusiano huo ulipofikia sasa ni matokeo ya juhudi za pande zote mbili kwa pamoja, lakini licha ya hayo, ili kurejesha uhusiano huu vizuri na kuzuia mvutano wa baadaye, pande zote mbili bado zina kazi kubwa na za muhimu za kufanya, na pia, bado zinatakuwa kushughulikia masuala mbalimbali ambayo hayana uhakika.

Ni wazi kwamba, kipindi kijacho kitakuwa ni muhimu sana katika kufuatilia masuala ya kufanya maamuzi, uongozi, na matarajio ya China na Marekani kwa pamoja. Kwa wakati huu, kutokana na uzoefu uliopita na ukweli wa siasa za Marekani, nchi hiyo inakabiliwa na changamoto ya mazingira magumu ya kisiasa na sintofahamu kubwa.

Mwaka mmoja tu uliopita, viongozi wa China na Marekani walifikia maafikiano mjini Bali, Indonesia, kuhusu kudhibiti uhusiano unaoonekana kwenda mrama kati ya nchi hizi mbili. Hata hivyo, tangu wakati huo, Marekani haikuacha juhudi zake za kuidhibiti China, na badala yake, iliongeza juhudi zaidi, kiasi kwamba kiwango cha uhusiano wa China na Marekani kwa mara nyingine tena kimefikia cha chini zaidi.

Wasiwasi kuhusu uhusiano wa nchi hizo mbili umeongezeka kutokana na mambo kadhaa yanayoashiria kuwa, kiongozi wa sasa wa Marekani hana uwezo wa kuingilia maslahi ya makundi mbalimbali ya nchini humo kama alivyofanya katika siku za nyuma. Ingawa huenda akawa na nia nzuri ya kufanya hivyo, lakini mazingira ya sasa ya kisiasa na mfumo wa uendeshaji nchini Marekani vinazuia uwezo wake. Kiongozi huyu hawezi kukwepa vizuizi vya pande mbalimbali, na kama kauli yake inaweza kuaminika, inategemea na kama ataungwa mkono kikamilifu na Bunge la Marekani.

Hivi sasa Marekani iko katika wakati mgumu wa kabla ya uchaguzi, na wagombea wa vyama vyote Democrat na Republican wanaweka msisitizo mkubwa katika masuala ya uhusiano kati ya Marekani na China. Huenda wanaweza kuendelea kuongeza hatua za kuikandamiza na kuidhibiti China, wakati idara za serikali ya nchi hiyo zikiendelea kutekeleza sera zinazoiona China kama mshindani wake mkuu, na haijulikani ni lini sera hizi zitaondolewa. Mambo haya yanaweka ugumu kwa pendekezo la utawala wa rais wa Marekani Joe Biden la kudhibiti ushindani.

Ni wazi kwamba, uhusiano mzuri kati ya China na Marekani unategemea kwa kiasi kikubwa mazingira ya kisiasa ya nchini Marekani. Kama siasa za ndani ya Marekani zitaendelea kutekelezwa katika mfumo usio na uhakika, sintofahamu ya uhusiano wa baadaye wa China na Marekani unaweza kuwa jambo la kawaida.

Pande hizo mbili hazina jinsi isipokuwa kujitahidi kuwa na mwelekeo mzuri zaidi, lakini wakati huohuo, ni lazima kujiandaa na uwezekano wa kutokea kwa migogoro.
 
Kuvunjika/kudumaa kwa uhusiano/mahusiano kati yao, hili ni hatari kwa mahusiano jamii ya Ulimwengu mzima.

China Ni kiungo/rafiki wa jumiia kubwa katika diplomasia kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom