Hivi jamani kuna vya wanawake na vya wanaume?

Hehehe! Vita tena? Kutoka mada ya misosi mpaka vita ya mabox Vs mavumbi! Natafuta taswira kamili.
umeliona hilo mchumba,inabidi tuite kamati ya usuluhishi kati ya Julius na Nguli.Hawa watu wana bifu la kichinichini.
wajumbe ni:
Xpin
Invizibo
Vera
MJ1
Nyamayao
Fidel80
ZD
Geoff
Burn
Semenya
Kaizer
Sipo
Masanilo
FL1
Mamaa Carmel
 
Haya hitimisho la kinywaji:
1.Wachangiaji wamepwaya katika michango maana nilitegemea kusikia background ya unywaji kufuatana na malezi.Hili halikujitokeza kabisa na hasa ukizingatia kila kabila wana pombe zao za kienyeji.
2. Unywaji wa wanawake na wanaume hautofautiani sana japo pombe kali mara nyingi hutumiwa na wanaume.Pombe tamu tamu kama ciders, wines ( hizi kiwango chake cha kilevi wakati mwingine hutisha!) hutumiwa na wanawake.

Swali, ni kwanini wanaume wengi hawanywi wine wakati tunajua kabisa kuwa alcohol content yake ni kubwa kuliko hata beer nyingi?
 
JIBU: Glass moja ya wine = 3500/- hadi 2500/-(baa mshenzi)
Wanawake waliowengi huwa hawalipi wenyewe bili kwa hiyo hawaoni uchungu, hapo kwenye glass moja ni sawa na chui mbili na nusu.
 
Hahaha! Mchumba bana! Angalizo: Kama huyo mwenye red atakuwa participant, then nashauri venue iwe msikitini au kanisani. Lol!
 
Haya hitimisho la kinywaji:
1.Wachangiaji wamepwaya katika michango maana nilitegemea kusikia background ya unywaji kufuatana na malezi.Hili halikujitokeza kabisa na hasa ukizingatia kila kabila wana pombe zao za kienyeji.
2. Unywaji wa wanawake na wanaume hautofautiani sana japo pombe kali mara nyingi hutumiwa na wanaume.Pombe tamu tamu kama ciders, wines ( hizi kiwango chake cha kilevi wakati mwingine hutisha!) hutumiwa na wanawake.

Swali, ni kwanini wanaume wengi hawanywi wine wakati tunajua kabisa kuwa alcohol content yake ni kubwa kuliko hata beer nyingi?

Wengine tupo shalow kwenye vinywaji,Bar naenda kwa bahati mbaya.kinywaji changu ni chai,maji na juice.
 
JIBU: Glass moja ya wine = 3500/- hadi 2500/-(baa mshenzi)
Wanawake waliowengi huwa hawalipi wenyewe bili kwa hiyo hawaoni uchungu, hapo kwenye glass moja ni sawa na chui mbili na nusu.
Asante sana kwa jibu zuri..
na je inakuwaje pale ambapo hakuna mtu anatakiwa kulipa, yaani kwenye sherehe/ ina maana wanaume watakunywa nao?
Akina kaka/baba, hii ni kweli? ndio sababu inayowafanya msinywe wines, cocktails? Au kuna sababu nyingine?
Kama ni swala la bei mbona ni wanawake wachache sana hunywa whyskies, brandies ambazo nazo siyo bei rahisi?..wal wanywaji wa couvoisier, hennessy.. wanaelewa what im talking about...
 
Asante ZD,
Ngoja nikuulize...katika chai na kahawa, soda na juice unadhani wanawake na wanaume wanapenda nini zaidi?
kwenye maziwa fresh na yogourt je?Yogourt plain, flavoured?
 
Kwa upande wangu hakuna hata kimoja nakipenda hapo. Mbadala wake ni supu ya mbuzi au mchemsho wa kuku. Ukisukumiza na serengeti mbili baridi mchana unapita bila kujua. Maziwa fresh huwa nayapiga asubuhi napoamka, si unajua watu wa maulabu lazima tujiwekee ka sekyuriti flani?
 
Suala si nani ananunua ni attitude toward vitu vya bei kali, unajua sina sandals inayofikia laki moja maihanei wangu anamiliki hizo mavitu za hadi laki mbili tena nyingi tu na zote nanunua mimi pamoja na hali yangu ya shida. Kwenye nyekundu umenifurahisha maana jana ulikuwa ka' unapinga hivi na wengi wakakufuata sa sijui leo wataelekea wapi? bendera bwana.
 
Kwa upande wangu hakuna hata kimoja nakipenda hapo. Mbadala wake ni supu ya mbuzi au mchemsho wa kuku. Ukisukumiza na serengeti mbili baridi mchana unapita bila kujua. Maziwa fresh huwa nayapiga asubuhi napoamka, si unajua watu wa maulabu lazima tujiwekee ka sekyuriti flani?
Mbadala wa supu..asante Cris.

Hivi supu ambazo hunywewa na wanywaji asubuhi.... ni kwa wote wanawake na wanaume au?
 
Hahaha! Hapa ofisini kuna mdada mmoja anapiga supu sijapata ona. Lol! Huyu lazima atakuwa anazimimina safari za kutosha! Mashosti wengi naona huwa wanapendela kahawa na visambusa na vitu kama hivyo.
 
Asante ZD,
Ngoja nikuulize...katika chai na kahawa, soda na juice unadhani wanawake na wanaume wanapenda nini zaidi?
kwenye maziwa fresh na yogourt je?Yogourt plain, flavoured?

Wote wanakunywa mchanganyiko wanaume kwa wanawake,lakini wanakunywa zaidi soda kwa vile juice ni gharama na katika mahoteli makubwa juice inanywewa sana na wanawake kuliko wanaume.chai na kahawa sio sana ni kwa wachache hasa asubuhi kwa vile kuna joto sana Dar.
Maziwa ya aina zote hayana wapenzi sana isipokuwa kwa watu waenye asili na maziwa kama wamasai na wasukuma.
 
JIBU: Glass moja ya wine = 3500/- hadi 2500/-(baa mshenzi)
Wanawake waliowengi huwa hawalipi wenyewe bili kwa hiyo hawaoni uchungu, hapo kwenye glass moja ni sawa na chui mbili na nusu.

Nahisi ni kutokana na ''nature'' tu wa kisaikolojia kati ya mwanaume na mwanamke. Mwanaume anaweza kuwa bahili hata kwenye kununua mavazi yake mwenyewe. Lakini mkewe au girlfriend wake akawa anamnunulia chochote anachotaka bila kujali bei.

Mfano, ni vigumu kukuta mwanamke anaendesha ka-gari ka ovyo ovyo mjini au ana simu kimeo. Ila wanaume ni jambo la kawaida tu!

Kwa hiyo hata kwenye vinywaji ni hivyo hivyo tu!
 
Hahaha! Hapa ofisini kuna mdada mmoja anapiga supu sijapata ona. Lol! Huyu lazima atakuwa anazimimina safari za kutosha! Mashosti wengi naona huwa wanapendela kahawa na visambusa na vitu kama hivyo.

Asante...
Supu ni kama tiba ya mning'inio... hivyo supu hunywewa na wale wenye kutumia beer ?..na wanywa wine je?
 
haya tuweke kinywaji pending..
lets move on.
Part 3 UNADHIFU

Siku hizi wanawake na wanaume generally wanajitahidi sana kwenye usafi na utanashati.Kuna hata misemo kuwa cleanliness is Godly....to be clean is to be next to God etc.Lakini suala la usafi lina siasa zake.Je wanawake na wanaume ni wapi wanajali sana usafi wao binafsi - mwili, nywele, nyumba wanamoishi, maofisini, vyooni nakadhalika?
Tuwe wakweli kabisa kwenye hili.
 
Back
Top Bottom