Hivi jamani kuna vya wanawake na vya wanaume?

Watu wa ofisini wote (wanaume na wanawake) wanatakiwa kula mara mbili kwa siku,asubuhi na jioni saa 11 au saa 12.
Asubuhi kula kitu hevi kama chai na kiporo au mihogo,viazi na hata mabumunda.usisahau matunda.
Mchana kula matunda au kunywa juice.
Jioni kula chips na kachumbari,au wali nyama kidogo sana.
usisahau kuywa maji angalau lita 2 kwa siku nzima.

Na wale wa zege hao wale chakula hevi hata mara 3 kwa siku ugali na wali au ndizi na mboga nyingi.

Wagonjwa,wajawazito na watoto na wazee wanaratiba yao special wataalamu wanajua.

NB.Jinsi unavyolizoesha tumbo lako ndivyo linavyokuwa.ukila sna linatanuka na utakuwa unasikia sana njaa na hushibi haraka.ukila kiasi ukizoea utakuwa unakula kiduchu.
 
Ninaleta mada hii ili kujaribu kuelewa zaidi kuhusu wanawake na wanaume katika kupendelea vitu fulani zaidi( preferences).
Nitaanza na 1.VYAKULA.
Je ni kweli wanaume wanapenda zaidi kula ugali, wali, viazi ndizi, wakati wanawake hupendelea zaidi soup/mtori,chips, macarroni/spaghetti,mikate, maandazi, chapati,salads?
Nimewahi kusikia kwa baadhi ya wanaume kuwa wasipokula ugali hawashibi; ugali huwafanya wawe na nguvu zaidi za mwili na hata majukumu yake mengine ya uzazi. Je kuna ukweli?
Mimi binafsi sioni tofauti katika vyakula na hivyo hakuna ninachopendelea zaidi ya kingine alimradi kimepikwa vizuri.Ugali siupendelei zaidi kwa sababu tangu utotoni sikuupenda.

Naomba sana michango yenu - wanawake kwa wanaume kwa uwingi wenu iwezekanavyo.
Asanteni.

Mimi navyo dhani, wanawake wanapenda kula vyakula vya kigeni, vyakula ambavyo hawavipiki wenyewe (they like to try new foods) lakini wanaume wanakula vyakula vyote (doesn't metter for them)
 
Hahahaha Burn iwa unaona wanavyo zishika hizo coni? mm iwa napandwa na mahasira balaa.

hapo huwa ni mzuka zaidi umkute mtoto ana lipsi za maana halafu hiyo ice cream imebakibaki unaweza pandwa na wazimu, sasa picture that ni lidume linaramba hiyo koni unaweza tapika.
 
Ni kitendo cha aibu sana kwa toto la kiume kula ice cream tena ya cone, na kwa malezi ya kwetu mtoto wa kiume kulakula hadharani ni dalili za kuwa weak. Nikiwa peke yangu au na watu wa karibu sana nakula tu chocolate na ice cream ila sio cone pia sili lolipop asilani. Vipi wewe VeraCity ukimuona mtoto wa kike kashikilia mzinga konyagi na mwingine na ana glass ya wine nani atakuwa anaonekana kikekike?

Hapa kwenye bold ndipo napataka.
Kabla ya yote nadhani kwenye hivyo vimiminika sitakuwa na mshangao wowote.Nitashangaa pale nitakapoona bibie mrembo kashikilia liglass ambalo linaonyesha ni lizito ( beer glass zile nzito!)..kama ni konyagi ikiwa kwenye proper glass wala sina tatizo...hili ni somo lingine tutalijadili baadae kwenye mada hii hii.

kuhusu kula icecream iwe ni ball cone au sugar cone sioni tatizo kabisa kwa mwanaume kula maana kila mtu ana haki na uhuru kula ile kitu roho inataka.
 
Kwa dunia ya sasa ukiona mwanamke amevaa suruali watu hamshangai lakini vijijini lazima watamshangaa lakini ukiona mwanaume amevaa sketi hii naona kama dunia nzima itakushangaa sasa sielewi sielewi hapa wanawake wanapo ingilia maswala ya kiumeni ni shwari lakini
Wapendwa...naomba twende taratibu basi..sasa hivi tunazungumzia makulaji..mbona mnaruka mpangilio? TUKO KWENYE1.VYAKULA
Hii mada ina malengo yake wakuu wangu samahani sana naomba uvumilivu wenu tu..kama mchango wako uko kwenye mavazi naona vuta subira tutakuja huko.
 
ni ulivyolelewa tu.............mwanamme anaweza akalamba icecrem cone na akaonekana dume kuliko wewe unaekula ugali

ni unvyojiweka tu........

vyakula havin gender........yoyote anaweza kula chochote
 
Mimi navyo dhani, wanawake wanapenda kula vyakula vya kigeni, vyakula ambavyo hawavipiki wenyewe (they like to try new foods) lakini wanaume wanakula vyakula vyote (doesn't metter for them)
Mkuu asante sana kwa kuleta dimension nyingine kwenye PART 1 ya mada -VYAKULA.

Kwanini unadhani wanawake wanapenda kula vyakula vile ambavyo huwa hawavipiki wenyewe? Nadhani assumption hapa ni kuwa mnapotoka kula out ndiyo choice waifanyayo wanawake. Je wewe kwa mfano, ukitoka kula restaurant, unapendelea zaidi kula vyakula gani/ ni vile ulivyovizoea au vile ambavyo mara nyingi haviko kwenye menu nyumbani?
 
Hii nayo inategemea,nijuavyo mimi wanawake wengi wanafanya dayati na vyakula vingi vya kigeni vinakuwa na mafuta.Mimi mwenyewe huwa napendelea kula nilichopika mwenyewe ,vingine naviona vibaya.Sijui lakini pegine watu tunatofautiana.
 
hapo huwa ni mzuka zaidi umkute mtoto ana lipsi za maana halafu hiyo ice cream imebakibaki unaweza pandwa na wazimu, sasa picture that ni lidume linaramba hiyo koni unaweza tapika.

Hahahaha kwa shori mm kwangu nywele iwa zinasimama na mwili kusisimka ila kwa dume dah ebwaneee iwa naona kinyaa utaona dume zima na midevu linailamba lamba na kuizungusha dah
 
Hii nayo inategemea,nijuavyo mimi wanawake wengi wanafanya dayati na vyakula vingi vya kigeni vinakuwa na mafuta.Mimi mwenyewe huwa napendelea kula nilichopika mwenyewe ,vingine naviona vibaya.Sijui lakini pegine watu tunatofautiana.

Wewe kama FL unapenda zaidi vyakula gani kama hutajali kushirikisha wengine kujua hili?
 
Hahahaha kwa shori mm kwangu nywele iwa zinasimama na mwili kusisimka ila kwa dume dah ebwaneee iwa naona kinyaa utaona dume zima na midevu linailamba lamba na kuizungusha dah

Ina maana Fidel, unaangalia mtu anavyokula na wewe kuanza kutoa tafsiri? Hii inatokea kwanini?
 
kwa nafsi yangu nikila nje.....nakula zaidi vyakula vya kigeni hasa itlian food au spanish.

nikiwa ndani kwangu napata tabu sana kwa kuwa sina mapenzi na chakula kihivyo na mr wangu anapenda kula mno!

nnachoweza kusema huwa hachagui chakula, na hula icecream cone tukiwa nje wote
 
Yatakushinda besti!
Haya hebu tuambie wewe unapendelea vyakula gani na kwanini?

Kwani wewe yamekushinda?
Mimi napendelea mdudu wa kuchoma, Ugali samaki, Mchemsho wa kuku wakienyeji au mchemsho wa ng'ombe, supu ya mbuzi na supu ya pweza...kisha nateremshia na Ndovu
 
kwa nafsi yangu nikila nje.....nakula zaidi vyakula vya kigeni hasa itlian food au spanish.

nikiwa ndani kwangu napata tabu sana kwa kuwa sina mapenzi na chakula kihivyo na mr wangu anapenda kula mno!

nnachoweza kusema huwa hachagui chakula, na hula icecream cone tukiwa nje wote

Asante ndugu yangu..
kuhusu cone hata mie Mr wangu haoni noma kula cone kabisa..... sote tunafurahia icecream na mawazo kama aliyotoa Fidel au Burn wala hayajawahi kutuingia akilini kabisa!

Je wenzangu, mnaona ubaya wowote kula hadharani? Mfano una haraka au uko kwenye traffic jam, ukawa umenunua may be a snack - chocolate, a fruit kama ndizi , crisps, cashewnuts etc, utasubiri hadi ufike nyumbani au unaweza kula tu huku ukiendelea na safari??
 
Je wenzangu, mnaona ubaya wowote kula hadharani?

Kuna vitu vya kula hadharani lakini sio ice cream maana unatengeneza tention kwa watu wengine tunamifadhaiko ya ajabu sasa unalamba lamba kiustadi mbele za watu unajenga taswira mbaya ingawa wewe unafrahia na mm pembeni nafrahia kitaswira
 
Wewe kama FL unapenda zaidi vyakula gani kama hutajali kushirikisha wengine kujua hili?

Kwa nature mimi sio mlaji sana.na sina favourite dish lakini sipendi makande wala ugali au nyama.Vyakula vingine vyote naviona kawaida especially vya kiafrika kwani sipendelei vya kizungu.Ila vya kizungu huwa nakula mara mojamoja sana nikialikwa mahali nikavikuta.
Mara nyingine najikuta nikila mayai au chipsi kwa sababu ni rahisi kupika na sio kwa vile napenda
ujumbe: jinsi ulivyo ni matokeo ya chakula unachokula.
 
Asante ndugu yangu..
kuhusu cone hata mie Mr wangu haoni noma kula cone kabisa..... sote tunafurahia icecream na mawazo kama aliyotoa Fidel au Burn wala hayajawahi kutuingia akilini kabisa!

Je wenzangu, mnaona ubaya wowote kula hadharani? Mfano una haraka au uko kwenye traffic jam, ukawa umenunua may be a snack - chocolate, a fruit kama ndizi , crisps, cashewnuts etc, utasubiri hadi ufike nyumbani au unaweza kula tu huku ukiendelea na safari??

Kwa suala la aibu kwangu sina,mie naweza kula.Ila huwa sili kwa ajili ya afya,sio vizuri kulakula in between major meals,kwanza kwa ajili ya colesterol na pia kipindupindu(unawezza kuwa unakula embe njiani na michuzi inakuchuruzikia yani noma kweli na mainzi wanakufuata)
 
acheniubishoo nyie watoto wa kiume, mwanaume kama sijala ugali na nyama choma (...mhhh mate yanajaa mdomoni!) pilipili na limao kwa mbaali, msiseme hamtamani!!! hakyamungu sili piza labda niwe mazingira ambayo ugali na nyama choma au samaki wa kuchoma havipatikani!!!! KWELI KABISA WAZEE, ila kuramba koni barabarani bado!!! soseji kila siku kwenye breakfast (tena soseji ya mdudu) asubuhi kula ugali noma mwanangu, ila shangaa mke wangu asubuhi yeye anagonga uporo wa ugali niliobakiza jana (AMESHINDWA KABISA KUACHA TABIA HII) ANAPENDA MATEMBELE KAMA MBUZI
 
Back
Top Bottom