Hivi jamani kuna vya wanawake na vya wanaume? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi jamani kuna vya wanawake na vya wanaume?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Nov 11, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ninaleta mada hii ili kujaribu kuelewa zaidi kuhusu wanawake na wanaume katika kupendelea vitu fulani zaidi( preferences).
  Nitaanza na 1.VYAKULA.
  Je ni kweli wanaume wanapenda zaidi kula ugali, wali, viazi ndizi, wakati wanawake hupendelea zaidi soup/mtori,chips, macarroni/spaghetti,mikate, maandazi, chapati,salads?
  Nimewahi kusikia kwa baadhi ya wanaume kuwa wasipokula ugali hawashibi; ugali huwafanya wawe na nguvu zaidi za mwili na hata majukumu yake mengine ya uzazi. Je kuna ukweli?
  Mimi binafsi sioni tofauti katika vyakula na hivyo hakuna ninachopendelea zaidi ya kingine alimradi kimepikwa vizuri.Ugali siupendelei zaidi kwa sababu tangu utotoni sikuupenda.

  Naomba sana michango yenu - wanawake kwa wanaume kwa uwingi wenu iwezekanavyo.
  Asanteni.
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  mimi nikiliona dume zima linakula chocolate hadharani naanza kupata mashaka, halafu nikiona mwanaume anakula chipsi mayai ''uskaushe'' naogopa.Mimi siwezi kabisa kula ice cream cone hadharani wala soseji. nadhani umenisoma.
   
 3. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kaukweli kapo ila kidogo sana.
  mara nyingi sana uchaguzi wa chakula unatokana na mazingira mtu alipozaliwa na kukua,mfano kama ni mtu wa Kyela ,uwe mwanaume au mwanamke lazima utapenda wali.Na kama ni Bukoba lazima wote watapenda ndizi.Na wazungu sio rahisi wapende ugali hata kama ni mwanamume ,wanapenda ma-burger na mapiza.
  kwa hiyo ka ukweli kapo ila kadogo hasa huku mjini tena kutokana na nature ya kazi ya mtu.
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wenzetu dunia ya kwanza kula aiskrim wanaume kawaida kabisa.yani wenyewe wanatembea na lunch box huku anakula.yani wanapenda kulakula.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mh, wewe VC:D:p mchokozi!!
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  si ndio maana ni kawaida pia kwa midume mizima kuolewa, tena hata aibu haina linaweza kumtambulisha dume lenzake kwa wazazi wake eti ''dady this is my boyfriend'' kama toto langu litachezea gobole na hilo dume lake na sambaza ubongo.
   
 7. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hapa inategemea na jinsi ulivyolelewa au makuzi yako tu hakuna vyakula vya mwanaume au mwanamke, mie hubby wangu wala hapendi ugali na vyakula vigumu kabisaaa.
  Mie ugali huwa nakula kwa msimu nikikaa muda mrefu ndio napata hamu ya kula ugali, ila ndizi na vyakula vingine twende tu hivyo havina msimu.

  Ila sema baadhi ya sehemu kuna wanaume kweli bila ugali bado hujamwambia kitu.Kuna sehemu niliwahi kwenda hadi nilishangaa yaani wao asubuhi na mapema wanakula ugali tena mgumuu, ukiwaambia habari za kula snacks na chai asubuhi hata hawakuelewi. Wanasema kwamba wao ndivyo walivyokulia kula ugali asubuhi.

  Hivyo mie naona hii sana sana inategemea malezi na mazingira uliyokulia toka ulivyokuwa mtoto wazazi wako walikuwa wanapendelea kukulisha vitu gani, hivyo ukiwa mkubwa utapendelea hivyo vitu.
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Asante ZD,
  Nakuunga mkono 98% kuwa inategemeana na ulikozaliwa/toka.Ninasema hivi kwa sababu, chukulia wale walaji wa ndizi kwa mfano.Miaka ya zamani ilikuwa ni aibu kubwa kula ugali maana waliona ugali ni chakula cha kimasikini! Siku hizi imani hizi hazipo tena.Unakuta ugali unaliwa na makabila yote.Kadhalika kwa baadhi ya makabila yasiyolima mpunga, wali uliliwa kama chakula cha sikukuu! Siku hizi wali ni chakula maarufu kila mahali na kwa makabila yote bila kujali wanalima mpunga au kuna sherehe .

  Nina marafiki wazungu wanapenda sana ugali na hii imechangiwa na influence ya kuchanganyika na waafrika ( ugali huliwa karibu kila nchi - Zimbabwe huitwa Sadza, Zambia huitwa Millie miliie,huko west africa huitwa fufu n.k.).Kadhalika chips chakula cha kimagharibi kimegeuka cha kawaida mno kiasi utakikuta kila mahali hadi barabarani na huliwa na kila mtu.

  Umegusia ulaji unaozingatia kazi mtu aifanyayo - hapa ndio nataka tujikite zaidi.Kiafya pia tunaambiwa tule kufuatana na mahitaji ya mwili.Kama unafanya kazi laini za ofisini mahitaji yatakuwa kidogo kuliko mbeba mizigo, mkulima nk. Je kwa wanawake na wanaume tunavyochagua vyakula tunajali hili au inatokana na vionjo tu?
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Burn jamani!
  Kuwa muwazi basi ili tuelimike ndugu yangu.
  Ni kwanini? Hutamani ice cream wala chocolate au inakuwaje? Je ukiwa mweyewe nyumbani pia huli?
   
 10. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Hapa mimi nilitegemea tu, jina zuri kama hilo huwezi kuwa unapenda ugali.
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana nanyi kwamba Malezi ya toka utotoni ndiyo yanafanya mtu apende kula aina gani ya chakula, kwa mfano mimi nilivyozoea ni kula ASubuhi chai na maandazi YASIYOZIDI matatu, au HOME MADE bread ambayo tulikuwa tunakatiwa slice moja ukubwa wa km wa chungwa hivi, siagi/blue band halafu mchana piga UA lazima UGALI na mboga yoyote ile ila ya MAJANI haikosi so zinakuwa mboga mbili na matunda pembeni, Usiku lazima WALI Na na matunda. kwa kweli siku my wife wakati wa uchumba alipoanza kunipikia ilikuwa tofauti na yale niliyoyazoea, asubuhi anaweza akakupikia mchemsho sahani nzima km vile lunch, na mie sikuzoea asubuhi kupata breakfast nzito(Mtanisamehe niliishi na step mother toka nna 3yrs na yeye aliweza kupika maandazi hata ndoo nzima lkn asubuhi mtakula maandazi mawili hata matatu na tulikuwa watoto 5 within a week yale mengine utakuta yameoza nusu ndoo inamwagwa) Mchana ndo usiseme ma variety ya msosi mara ndizi mara futari ya mihogo, jioni sometimes ndizi za kukaanga na kachumbari, dah ilinichukua muda kuzoea so hii kitu bana mimi naamini sana ni kule ulikokulia na ulikuwa raised na menu dizaini gani
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Kuna kila kitu cha wanaume na wanawake, michezo, nguo, sherehe--kitchen party, nk
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Ni kitendo cha aibu sana kwa toto la kiume kula ice cream tena ya cone, na kwa malezi ya kwetu mtoto wa kiume kulakula hadharani ni dalili za kuwa weak. Nikiwa peke yangu au na watu wa karibu sana nakula tu chocolate na ice cream ila sio cone pia sili lolipop asilani. Vipi wewe VeraCity ukimuona mtoto wa kike kashikilia mzinga konyagi na mwingine na ana glass ya wine nani atakuwa anaonekana kikekike?
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Nov 11, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Sasa mtoto wa kike na supu ya Paya au supu ya kongoro wapi na wapi bana?
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Nov 11, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Sasa mtoto wa kike na supu ya paya au ya kongoro wapi na wapi bana???!!!
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Nov 11, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa dunia ya sasa ukiona mwanamke amevaa suruali watu hamshangai lakini vijijini lazima watamshangaa lakini ukiona mwanaume amevaa sketi hii naona kama dunia nzima itakushangaa sasa sielewi sielewi hapa wanawake wanapo ingilia maswala ya kiumeni ni shwari lakini mwanaume akiingilia maswala ya ukeni huko inakuwa nongwa kwa nini?
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Nov 11, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahaha Burn iwa unaona wanavyo zishika hizo coni? mm iwa napandwa na mahasira balaa.
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Nov 11, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  au ukute toto la kiume na savanna premium cider.
   
 19. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #19
  Nov 11, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  2. RANGI
  Huwa pia kuna kasumba kwamba rangi ya pinc ni kwa ajili ya wanawake, na hii kasumba si kwetu Tz/Africa hata baadhi ya maeneo ya Mashariki ya Mbali huko Asia nilikutana na kasumba hii nilipokuwa huko. Sasa, ni kitu gani kihalalishe rangi ya pinc ionekane ni ya wanawake tu?
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Nov 11, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ulishazoeshwa pattern fulani toka utotoni, halafu unakuja kuoa unakutana na pattern nyingine... je unadhani adaptation kutoka chai ya maandazi mawili hadi mchemsho sahani tele kama lunch ilikuwa kitu rahisi? Na je ingekuwa wewe ulishazoea mchemsho sahani..halafu ukaoa ukakauta wife anatoka kule ambako wanakunywa chai na maandazi mawili unadhani nini kingetokea?
   
Loading...