Hivi inawezekanaje mtu huna kazi bado unasoma Master's Degree?

Elimu na maarifa ndo utajiri wenyewe huo ikiwa MTU utapata chocho la kusoma soma Sana . mambo ya Ajira na Pesa ni mambo madogo Sana kuyapata.
 
Wakuu habari za Jumapili,

Niseme, mwaka huu 2023 nimehitimu Shahada ya Umahiri ama Master's Degree kwenye fani ya uchawi na ushirikina chuo kikuu.

Kwenye kuisoma hiyo fani, kilichonishangaza sana na bado nazidi kushangaa ni kuona vijana wakisoma Shahada za Umahiri huku hawana kazi.

Najiuliza, kwa hapa Tanzania kazi zinazotangazwa zinazotaka mtu awe mahiri ni kazi ambazo lazima uwe na uzoefu usiopungua miaka 8 na kuendelea na mara nyingi kama sio zote hua ni managerial positions.

Sasa kama Shahada ya awali haijakupa kazi, haijakusaidia kupata kazi, unawezaje kwenda kusoma Shahada nyingine ya juu zaidi huku huna kazi?

Kwa mtazamo wangu, wazazi wanapoteza pesa nyingi sana kusomesha watoto wao Master's Degree ambazo wangezitumia kuwafungulia miradi ya ujasiliamali na wakapata pesa.

Leo kukuta kijana yuko mtaani na anaendesha bodaboda na ana Master's Degree ni kitu cha kawaida, unajiuliza hiyo pesa ya Master's Degree zaidi ya 10m na 2+years za kusoma, angeanza kua bodaboda si angekua mbali sana, kwanza angekua na bodaboda 5 ambazo zinamuingizia wastani wa 1.2m kwa mwezi, miaka 2 angekua na 25m+ na bado bodaboda zake ziko pale pale.

Juzi nimeenda na girlfriend wangu mahala kwa tailor, nikakuta tailor katika mazungumzo anasema ana Master's Degree ya Accountancy halafu ni fundi nguo, yeye mwenyewe anajilaumu kusoma Master's Degree bora angeaza ushonaji mapema angekuwa mbali.

Master's Degree bongo zinasomwa kwa kujifurahisha?
mkishashiba na mavitambi yenu mnajijambia tu mnakua motivational speakers.
 
Kama kuna kosa tunalifanya ni kuendelea kuidharau elimu. Someni kama kuna fursa ya kufanya hivyo...ili hata msipoajiliwa muweze kuweka ubora kwenye shughuli zingine mnazozifanya.
Tumekuwa tukidharau kazi za mikono kuwa ni za watu wasio na elimu lakini ukweli ni kwamba ajira nyingi zitapungua hivyo tegemeeni kazi za suluba kuwa kimbilio la wasomi wengi.
Sijui mnautazamaje ujio wa robots and AI technology nyie wasomi.
We waache wambeze mtoa mada.
 
Wakuu habari za Jumapili,

Niseme, mwaka huu 2023 nimehitimu Shahada ya Umahiri ama Master's Degree kwenye fani ya uchawi na ushirikina chuo kikuu.

Kwenye kuisoma hiyo fani, kilichonishangaza sana na bado nazidi kushangaa ni kuona vijana wakisoma Shahada za Umahiri huku hawana kazi.

Najiuliza, kwa hapa Tanzania kazi zinazotangazwa zinazotaka mtu awe mahiri ni kazi ambazo lazima uwe na uzoefu usiopungua miaka 8 na kuendelea na mara nyingi kama sio zote hua ni managerial positions.

Sasa kama Shahada ya awali haijakupa kazi, haijakusaidia kupata kazi, unawezaje kwenda kusoma Shahada nyingine ya juu zaidi huku huna kazi?

Kwa mtazamo wangu, wazazi wanapoteza pesa nyingi sana kusomesha watoto wao Master's Degree ambazo wangezitumia kuwafungulia miradi ya ujasiliamali na wakapata pesa.

Leo kukuta kijana yuko mtaani na anaendesha bodaboda na ana Master's Degree ni kitu cha kawaida, unajiuliza hiyo pesa ya Master's Degree zaidi ya 10m na 2+years za kusoma, angeanza kua bodaboda si angekua mbali sana, kwanza angekua na bodaboda 5 ambazo zinamuingizia wastani wa 1.2m kwa mwezi, miaka 2 angekua na 25m+ na bado bodaboda zake ziko pale pale.

Juzi nimeenda na girlfriend wangu mahala kwa tailor, nikakuta tailor katika mazungumzo anasema ana Master's Degree ya Accountancy halafu ni fundi nguo, yeye mwenyewe anajilaumu kusoma Master's Degree bora angeaza ushonaji mapema angekuwa mbali.

Master's Degree bongo zinasomwa kwa kujifurahisha?

Huwezi kumpangia mtu asome mpaka level gani na wakati gani kwa sababu haulipi ada wewe wala hayo maarifa hayana uhusiano na wewe.
 
Unajua hakuna mtu mwenye uhakika kwamba akifanya nini atafanikiwa. Kila mtu anajaribu. Kuna watu drs la saba wana mafanikio kuna drs la saba ni mafukara wa kutupwa. Kuna mtu masters ndo imempa +advantage akapata kazi nzuri kuna mtu diploma ndo imempa kazi nzuri.

Jamani. KILA MTU APAMBANE KWA LILE AMBALO ANAONA LINAWEZA KUMPA MAISHA ANAYOYATAKA, TUSIWE WACHAWI KUKAA NA KUTAFUTA WANAOKOSEA MAISHA TUWAITE WAJINGA. MAISHA HAYANA NJIA YA UHAKIKA YA MAFANIKIO.
Well spoken
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kwa elimu gani hiihii ya hapa !! Wanasomaga kufaulu mitihani hapo unaelimikia wapi Yani!

Mtoa mada ana hoja
Hapo unakosea ndugu unasema elimu yakufaulu mitihani sio,ngoja nikuulize swali dogo,tu je umewahi tembelea hospitals Kwa shida yoyote yakiafya? ukatibiwa na ukapona? Au ndugu yako? Sasa wale waliokutibu walisoma hizo elimu unazo zizarau za kufaulu mitihani.inawezekana wewe hauna kichwa Cha kubeba material,waache wenzio wasome.
 
Ana hasira na wenye degree
 
Kusoma master's degree wakati huna kazi Wala biashara ni uoga wa maisha tu wala hakuna kingine.Confucius aliwahi kuulizwa ; watu wameongezeka Sana nchini( china) serikali iwafanyie nini? Confucius akajibu,enrich them! Wakamuuliza baada ya kuwapa mali akajibu educate them,wakamuliza what next akajibu security.kumbe mali ni Bora kuliko elimu na hili liko wazi Wewe jaribu kwenda nyumbani na master's yako huna hata Hela ya vocha uone kama hujatumwa na mdogo wako umfatie vocha dukani ili nawewe upate vocha!
 
Wakuu habari za Jumapili,

Niseme, mwaka huu 2023 nimehitimu Shahada ya Umahiri ama Master's Degree kwenye fani ya uchawi na ushirikina chuo kikuu.

Kwenye kuisoma hiyo fani, kilichonishangaza sana na bado nazidi kushangaa ni kuona vijana wakisoma Shahada za Umahiri huku hawana kazi.

Najiuliza, kwa hapa Tanzania kazi zinazotangazwa zinazotaka mtu awe mahiri ni kazi ambazo lazima uwe na uzoefu usiopungua miaka 8 na kuendelea na mara nyingi kama sio zote hua ni managerial positions.

Sasa kama Shahada ya awali haijakupa kazi, haijakusaidia kupata kazi, unawezaje kwenda kusoma Shahada nyingine ya juu zaidi huku huna kazi?

Kwa mtazamo wangu, wazazi wanapoteza pesa nyingi sana kusomesha watoto wao Master's Degree ambazo wangezitumia kuwafungulia miradi ya ujasiliamali na wakapata pesa.

Leo kukuta kijana yuko mtaani na anaendesha bodaboda na ana Master's Degree ni kitu cha kawaida, unajiuliza hiyo pesa ya Master's Degree zaidi ya 10m na 2+years za kusoma, angeanza kua bodaboda si angekua mbali sana, kwanza angekua na bodaboda 5 ambazo zinamuingizia wastani wa 1.2m kwa mwezi, miaka 2 angekua na 25m+ na bado bodaboda zake ziko pale pale.

Juzi nimeenda na girlfriend wangu mahala kwa tailor, nikakuta tailor katika mazungumzo anasema ana Master's Degree ya Accountancy halafu ni fundi nguo, yeye mwenyewe anajilaumu kusoma Master's Degree bora angeaza ushonaji mapema angekuwa mbali.

Master's Degree bongo zinasomwa kwa kujifurahisha?

Lakini kuna wenye masters na wana kazi nzuri?
 
Shahada ya umahiri❌
Shahada ya uzamili✔
Wewe unaye msahihisha ndio umekosea, Master degree ni Shahada ya Umahiri. Shahada ya uzamili ni shahada nyingine unayosoma baada ya Shahada ya kwanza. Mfano mtu mwenye degree ya sheria akasome degree ya Sayansi ya siasa

Shahada za uzamili yani postgraduate degree ina jumuisha Postgraduate diploma (stashahada ya Uzamili, Master degree (Shahada ya Umahiri) na PhD (shahada ya Uzamivu)
 
Kapitie upya nondo zako then urudi tena. Ukishindwa unaweza kugoogle pia.
Asante🙏
 
Shahada ya umahiri❌
Shahada ya uzamili✔
Wewe unayemsahihisha ndio umekosea, Master degree ni Shahada ya Umahiri. Shahada ya uzamili ni shahada nyingine unayosoma baada ya Shahada ya kwanza. Mfano mtu mwenye degree ya sheria akasome degree ya Sayansi ya siasa

Shahada za uzamili ni postgraduates ambazo ina jumuisha bachelor
Kapitie upya nondo zako then urudi tena. Ukishindwa unaweza kugoogle pia.
Asante🙏
Wewe ndio uje na ushahidi kuonesha mimi sitegemei maarifa ya kugoogle kila kitu. Master degree ni Shahada ya Umahiri ndio kiswahili sanifu.
 
Wewe unayemsahihisha ndio umekosea, Master degree ni Shahada ya Umahiri. Shahada ya uzamili ni shahada nyingine unayosoma baada ya Shahada ya kwanza. Mfano mtu mwenye degree ya sheria akasome degree ya Sayansi ya siasa

Shahada za uzamili ni postgraduates ambazo ina jumuisha bachelor

Wewe ndio uje na ushahidi kuonesha mimi sitegemei maarifa ya kugoogle kila kitu. Master degree ni Shahada ya Umahiri ndio kiswahili sanifu.
Sawa mtaalam
 
Back
Top Bottom