Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Habari za Leo wakuu,

Leo nilikua najaribu kuiuliza akili yangu swali lifutalo.

Yaani kwamba mwanadamu unafanya kazi za watu ambazo sio zako.

Yaani hapo ndio najiuliza, wakuu.

Wakuu hebu tujadili hii mada. Inakuwaje unaishi kwa kutumwa kwa miaka mitano?

Waajiriwa mlio maofisini hapa mtajibaraguza sana lakini hii mada inawahusu njooni mtolee maelezo huku.

Kwanini mnakaa kwenye ofisi za watu kwa zaidi ya miaka mitano.

Mkistaafu au kutumbuliwa ndio mnaanza kukumbuka shuka la kujiajiri na huku muda wenu wote, nguvu yenu yote na akili yenu yote mmemalizia kwenye ofisi za watu.
Pale akili ndogo inapojaribu kuwaza kwa akili ndogo zaidi
 
Kwanza kabisa, hakuna mtu anayefanya kazi zake.

Hata ukiwa na biashara yako, utafanya kazi za wateja wako.

Hivyo, na wewe pia umeajiriwa na hao wateja wako.

Tusiangalie mambo kwa tafsiri finyu ya juu juu tu.

Pia, watu wasingekaa ofisini kufanya kazi za watu wengine, hata wewe usingeweza kupost kitu hapa JF kujifaragua.

Kwa sababu JF inaendeshwa na watu wengi tu walioajiriwa wakakaa ofisini kufanya kazi za watu.
Huu uzi ulitakiwa uishie hapa baada ya hii comment.
Ila kwa kiwango cha ujinga alicho post acha atandikwe
 
Huyu watakua ni vijana waliotoka au bado wako shuleni bado anahisi kila kitu ni rahisi yaani akiona boom imeingia, akala chipsi yai, akanywa na pepsi, akaenda kufanya presentation akifanya na test akiwa anaongea na wenzake wanadanganyana anaona kila kitu rahisi uandishi wake unaonekana bado mchanga kwenye hustle za mtaa
Nasema uongo ndg zanguuuuuuuuuu?
Screenshot_20210614-145531.jpg
 
Unakuta mtu anapokea mshahara wa milion 4 , halafu mke wake Yuko mkoa mwingine abafanya kazi ya mshahara wa laki 9. Halafu familia Yao inaishi na house girl.

Unawauliza hivi mnashindwa kujiajiri mkae na familia. Wanajibu kazi kwanza. Huwa nashangaa Sana mentality za namna hii.
 
Kujiajiri sii kila mtu anaweza. Tuko huku mtaani tunasota ila hizo ajira tunazitolea udenda
 
Kwanza kabisa, hakuna mtu anayefanya kazi zake.

Hata ukiwa na biashara yako, utafanya kazi za wateja wako.

Hivyo, na wewe pia umeajiriwa na hao wateja wako.

Tusiangalie mambo kwa tafsiri finyu ya juu juu tu.

Pia, watu wasingekaa ofisini kufanya kazi za watu wengine, hata wewe usingeweza kupost kitu hapa JF kujifaragua.

Kwa sababu JF inaendeshwa na watu wengi tu walioajiriwa wakakaa ofisini kufanya kazi za watu.
Umemaliza mkuu!
 
Mleta mada watu wote wakifuata ushauri wako wakaacha kuajiriwa - mambo yatakwenda kweli?

Hata wewe utakwama.
 
Waajiriwa leo mtajieleza sana.
Nasema uongo ndg zanguuuuuuuuuu?View attachment 1819526
Habari za Leo wakuu,

Leo nilikua najaribu kuiuliza akili yangu swali lifutalo.

Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Yaani kwamba mwanadamu unafanya kazi za watu ambazo sio zako.

Yaani hapo ndio najiuliza, wakuu.

Wakuu hebu tujadili hii mada. Inakuwaje unaishi kwa kutumwa kwa miaka mitano?

Waajiriwa mlio maofisini hapa mtajibaraguza sana lakini hii mada inawahusu njooni mtolee maelezo huku.

Kwanini mnakaa kwenye ofisi za watu kwa zaidi ya miaka mitano.

Mkistaafu au kutumbuliwa ndio mnaanza kukumbuka shuka la kujiajiri na huku muda wenu wote, nguvu yenu yote na akili yenu yote mmemalizia kwenye ofisi za watu.
Kama nimekuelewa vizuri unatamani watu waajiriwe na wafanye kazi muda kifupi then watche ili na ww na wengine mpate kuajiri.
 
Sasa kwanini hao walioajiriwa wakifukuzwa kazi au kustaafu wanaanza kuhaha kujiajiri tena, zile hela walizopata kule kwenye kuajiria hazitoshi au hizi za kuja kujiajiri ndio zitatosha.
Kwa reasoning hizi we unaonekana bado mtoto. Ngoja watu wakujibu kitoto pia wasije wakakukomaza bure
 
Ukitaka kufanya kazi zako tu subiri uzikwe maana hata biashara akija mteja hapo ofisin kwako atakutuma vilevile acha watu wainjoy maisha yenyewe mafupi
 
Ushauri wa bure 'inspirational speaker uliyemsikiliza ukapata hayo mawazo, siku nyingine ukimuoma mkimbie sanaaaaaaa........ '
 
Watoto wa chuo hawa, waliotoka form six kwa BRN. Wakikaa kwa youtube wakiangalia videos za akina elon musk, na pesa za boom wanakimbilia kuja andika wanachojiskia humu. Huwa tunawaacha kwanza.....
 
Habari za Leo wakuu,

Leo nilikua najaribu kuiuliza akili yangu swali lifutalo.

Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Yaani kwamba mwanadamu unafanya kazi za watu ambazo sio zako.

Yaani hapo ndio najiuliza, wakuu.

Wakuu hebu tujadili hii mada. Inakuwaje unaishi kwa kutumwa kwa miaka mitano?

Waajiriwa mlio maofisini hapa mtajibaraguza sana lakini hii mada inawahusu njooni mtolee maelezo huku.

Kwanini mnakaa kwenye ofisi za watu kwa zaidi ya miaka mitano.

Mkistaafu au kutumbuliwa ndio mnaanza kukumbuka shuka la kujiajiri na huku muda wenu wote, nguvu yenu yote na akili yenu yote mmemalizia kwenye ofisi za watu.
Society imedilika na shuguli zote za muhimu zinafanywa na organization/taasisi na siyo mtu mmoja mmoja au familia. Ulinzi,elimu ,afya,uzalishaji mali,ujenzi wa infrastructure ni jukumu la organization ama public au private. Organization ndio chanzo kikuu cha ajira . Bila organization wasomi hawezi kutumia elimu yao inavyostahili watabaki kufanya vijishuguli vidogo vidogo visivyo na tija kwake wala taifa.
 
kwani ukijiajiri lazima nawewe uajili watu wa kukusaidia kazi yako kwa bila wataalamu walio ajiliwa kwa jili ya insu zako za kujiajili huwezi piga kazi
 
Watu wakijiajiri wakianza kupata mia mbili wanaanza kudharau walioajiriwa. Kwanini kuajiriwa ni kitu kibaya na kujiajiri ndio kizuri? Nchi itaendaje kama watu wote watajiajiri hivi huwa mna akili au shingo zenu zimebeba uvimbe juu yake.

Mtu anashindwa hata kuwaza kwamba kuna kazi ni lazima watu wawe waajiriwa. Na aliye ajiriwa amechagua kuajiriwa na ndio sehemu anayo jiona bora kuliko kujiajiri.
 
Tofautisha Kati ya kuajiriwa na kujiajiri, vinginevyo rudia tena kusoma uzi,kina maeneo hujayaelewa.
Kwanza kabisa, hakuna mtu anayefanya kazi zake.

Hata ukiwa na biashara yako, utafanya kazi za wateja wako.

Hivyo, na wewe pia umeajiriwa na hao wateja wako.

Tusiangalie mambo kwa tafsiri finyu ya juu juu tu.

Pia, watu wasingekaa ofisini kufanya kazi za watu wengine, hata wewe usingeweza kupost kitu hapa JF kujifaragua.

Kwa sababu JF inaendeshwa na watu wengi tu walioajiriwa wakakaa ofisini kufanya kazi za watu.
 
Watu wakijiajiri wakianza kupata mia mbili wanaanza kudharau walioajiriwa. Kwanini kuajiriwa ni kitu kibaya na kujiajiri ndio kizuri? Nchi itaendaje kama watu wote watajiajiri hivi huwa mna akili au shingo zenu zimebeba uvimbe juu yake.

Mtu anashindwa hata kuwaza kwamba kuna kazi ni lazima watu wawe waajiriwa. Na aliye ajiriwa amechagua kuajiriwa na ndio sehemu anayo jiona bora kuliko kujiajiri.
Mbona hata wewe kuna mahali umejiajiri mkuu
 
Back
Top Bottom