Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,318
- 5,990
Leo nimekaa na kujiuliza. Kwa wakristo tunaambiwa baada ya Yesu kurudi na kuwachukua wateule wake hao wateule watakaa mbinguni kwa miaka 1,000 wakijifunza hukumu ya wenye dhambi. Hiyo miaka 1,000 ni sawa na masaa 8,760,000. Na katika kujifunza hiyo hukumu hao wateule watakuwa wanaangalia "video" ya matendo ya kidhambi kwa kila mwanadamu ikiwa ni moja ya kazi kubwa watakazofanya wakiwa huko mbinguni. Hoja yangu ipo kwenye kuangalia hizo "video" za dhambi walizotenda watu.
Kwa sasa watu tulio hai duniani ni wastani wa watu 8,000,000,000. Hiyo idadi ni bila kuhesabu waliokwisha kufa miaka yote nenda rudi huko nyuma. Tukikadiria walio hai na waliokwisha kufa jumla wawe mara mbili ya tuliopo leo hii jumla tunakuwa 16,000,000,000 (bilioni 16). Ukisema dhambi za kila mmoja zionyeshwe japo kwa saa moja tu itahitaji masaa bilioni 16 ambazo ni sawa na miaka 1,826,484! Ukisema hizo dhambi za kila mmoja zionyeshe japo ndani ya dakika moja tu bado itachukua miaka 30,441 kuangalia video za hao watu wote.
Kumbuka hiyo hesabu niliyoandika hapo juu ni kwamba muda wote, kila siku kwa miaka yote hiyo ni watu kukaa macho na kuangalia video tu bila kazi nyingine kama kuimba/kumsifu Mungu, watu kuuliza maswali kwa yale mapya na ya kustaajabisha watakayokutana nayo huko mbinguni, kuongea na wapendwa wao ambao walikufa duniani na kuagana kwa maneno kama "R.I.P.", "tutaonana baadae", n.k. ambayo kwa pamoja ukiyajumlisha ni wazi itachukua miaka mingi zaidi ya ile niliyotaja awali ambayo ni zaidi ya miaka 1,000 iliyotajwa kwenye biblia.
Kwa mwenye uelewa zaidi naomba ufafanuzi wake.