Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,295
8,205
Habari za Leo wakuu,

Leo nilikua najaribu kuiuliza akili yangu swali lifutalo.

Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Yaani kwamba mwanadamu unafanya kazi za watu ambazo sio zako.

Yaani hapo ndio najiuliza, wakuu.

Wakuu hebu tujadili hii mada. Inakuwaje unaishi kwa kutumwa kwa miaka mitano?

Waajiriwa mlio maofisini hapa mtajibaraguza sana lakini hii mada inawahusu njooni mtolee maelezo huku.

Kwanini mnakaa kwenye ofisi za watu kwa zaidi ya miaka mitano.

Mkistaafu au kutumbuliwa ndio mnaanza kukumbuka shuka la kujiajiri na huku muda wenu wote, nguvu yenu yote na akili yenu yote mmemalizia kwenye ofisi za watu.
 
Kwanza kabisa, hakuna mtu anayefanya kazi zake.

Hata ukiwa na biashara yako, utafanya kazi za wateja wako.

Hivyo, na wewe pia umeajiriwa na hao wateja wako.

Tusiangalie mambo kwa tafsiri finyu ya juu juu tu.

Pia, watu wasingekaa ofisini kufanya kazi za watu wengine, hata wewe usingeweza kupost kitu hapa JF kujifaragua.

Kwa sababu JF inaendeshwa na watu wengi tu walioajiriwa wakakaa ofisini kufanya kazi za watu.
 
Naona kuna notion kwamba kuajiriwa ni jambo baya, hili jambo nalipinga. Kuajiriwa bila maslahi yanayoridhisha ndiyo jambo baya. Hata CEOs wa Apple, Google, Microsoft, Alibaba, Toyota and the list goes on and on nao pia ni waajiriwa na wanakunja pesa ndefu kuliko mkaanga viazi wa Tandahimba aliyejiajiri.

Aidha kujiajiri/ujasiliamali ni kuwa muajiriwa wa wateja wako. Wateja wako ndio mabosi wako. Utatenda vile watakavyo na kucheza mziki wao. Kifupi kukimbia kuajiriwa ni kuacha shughuli zote na kulala tu nyumbani.

Wewe unayepinga kuajiriwa siku ukianza ujasiliamali wako utahitaji hao hao waajiriwa. Kila mtu akiwa na mawazo kama yako sijui mtatoa wapi nguvu kazi.

Cha msingi ni kulipa watumishi maslahi stahiki.
 
Kwanza kabisa, hakuna mtu anayefanya kazi zake.

Hata ukiwa na biashara yako, utafanya kazi za wateja wako.

Hivyo, na wewe pia umeajiriwa na hao wateja wako.

Tusiangalie mambo kwa tafsiri finyu ya juu juu tu.

Pia, watu wasingekaa ofisini kufanya kazi za watu wengine, hata wewe usingeweza kupost kitu hapa JF kujifaragua.

Kwa sababu JF inaendeshwa na watu wengi tu walioajiriwa wakakaa ofisini kufanya kazi za watu.

You beat me to it.
 
Mdogo wangu acha kufuata mkumbo. Usipoteze muda kujiuliza maswali ya kijinga. Wewe na elimu yako ya social work hiyo tafuta mahali ajiriwa fanya kazi. Ukiajiriwa Muhimbili pale kama agent wa social works unakuwa unafanya kazi za watu au za wale unaowasaidia?

Hivi huwa mnawaza kuajiriwa ni kubaya kwa hiyo mnatakaje yaani, kila mtu ajiajiri?

Labda nikuulize swali, hussein pamba kali kajiajiri unahisi yeye ni bora na nafuu kuliko Kasimu Majaliwa ambaye kaajiriwa?
 
Kwa sisi tuliojiajiri, wewe umekosea kwani watu hutegemeana kwenye haya maisha, haina maana kuajiriwa ni kubaya labda uwe mwalimu wa chekechea, lakini kuna waajiriwa wanakunja pesa ambayo wewe kajiajiri kwenye mpunga miaka kumi bado huwezi kumfikia, tujifunze kuheshimiana na kuvumiliana maisha bila kutegemeana hayajawa maisha labda useme ajira isiyo na maslahi haifai tena ajira za dunia ya tatu au nchi maskini ndio changamoto lakini walikoendelea huko ajira ni bingo tu
 
Sasa kwanini hao walioajiriwa wakifukuzwa kazi au kustaafu wanaanza kuhaha kujiajiri tena, zile hela walizopata kule kwenye kuajiria hazitoshi au hizi za kuja kujiajiri ndio zitatosha.

Sasa jiajiri au ajiriwa bado unafanya kazi na watu lazima ujifunze kuheshimu kada nyingine utafika mbali kwa mfano una kampuni yako binafsi, ndio ni yako lakini ili upate tenda lazima ufanye kazi na makampuni mengine yaliyoajiri watu na wewe pia utakua umeajiri watu ili kazi ziende ukianza kudharau wale uliowaajiri na kuwanyima stahiki zao hesabu kampuni yako inakufa muda wowote,
 
Sasa kwanini hao walioajiriwa wakifukuzwa kazi au kustaafu wanaanza kuhaha kujiajiri tena, zile hela walizopata kule kwenye kuajiria hazitoshi au hizi za kuja kujiajiri ndio zitatosha.

Acha kua na akili kama za mbunge musukuma anaedharau wasomi huku yeye akiwa hana impact yoyote zaidi ya kutegemea wasomi haohao hata kufunga hesabu kwenye kampuni zake, jifunze sana kuheshimu kila kada na ukumbuke kujiajiri pekee sio kufanikiwa ndio maana waliojiajiri nao hufilisika vilevile kama walioajiriwa wanavofukuzwa kazi jifunze kuheshimu sana watu wengine
 
Habari za Leo wakuu,

Leo nilikua najaribu kuiuliza akili yangu swali lifutalo.

Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Yaani kwamba mwanadamu unafanya kazi za watu ambazo sio zako.

Yaani hapo ndio najiuliza, wakuu.

Wakuu hebu tujadili hii mada. Inakuwaje unaishi kwa kutumwa kwa miaka mitano?
Ww unafanya shuhuli gani?
 
Maisha ni harakati kama umejiajiri nakusihi sana heshimu wale unaofanya nao kazi utafika mbali, unless otherwise utakuja kuona hali sio maana unaleta kiburi, unadhani kwa nini tukiita kikao na wafanyakazi wanaokusaidia kazi unawaeleza maneno kama hii kampuni bila ninyi haiwezi kufika mbali, ninyi ndio wamiliki wa hii biashara tuitunze kwa pamoja hapo unajaribu kubuni na ufanisi wa kiutendaji ili mambo yaende mbele
 
Ww unafanya shuhuli gani?

Huyu watakua ni vijana waliotoka au bado wako shuleni bado anahisi kila kitu ni rahisi yaani akiona boom imeingia, akala chipsi yai, akanywa na pepsi, akaenda kufanya presentation akifanya na test akiwa anaongea na wenzake wanadanganyana anaona kila kitu rahisi uandishi wake unaonekana bado mchanga kwenye hustle za mtaa
 
Back
Top Bottom