Viongozi wa juu wa serikali wamulikie vitendo vya baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri kukataa kusaini barua zinazofika ofisini kwa utekelezaji

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,177
2,281
Tumeshaongea sn hapa juu ya baadhi ya viongozi wa serikali wanaolipwa mshahara wa Watanzania wanyonge kuona km ofisi wanazokalia ni mali Yao. Hili limekuwa likitokea ktk idara mbalimbali za serikali. Unakuta mtu kapewa dhamana kusimamia kundi flani la watu kwa kufuata sheria, utaratibu, na miongozo iliyopo lakini kwa makusudi anaamua kuinajisi ofisi yake kwa maslahi binafisi.

Siku moja tulijadili hapa kuhusu Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) ikaonekana kuna baadhi ya Viongozi wa serikali wanakikigia kifua kwa maslahi binafisi hasa pale wanachama wake wanapoamua kuhamia chama kingine. Ikasemekana kuwa Kuna baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri Wana manufaa binafsi na hiki chama (CWT) kwamba wamekuwa wakiwatisha Walimu kuhamia vyama vingine km CHAKUHAWATA kinachotambuliwa hadi hivi sasa na bodi ya usajili wa vyama vya Wafanyakazi nchini.

Kwa vile tuna watu wanaofanya kazi hii ya Ualimu huko ktk Halmashauri kuna taarifa zinasambaa kuwa baadhi ya Wakurugenzi wanapoandikiwa barua ya kuwataarufu kusitisha makato ya 2% kwenda CWT wamekuwa viziwi, hawasaini hizo barua kwa makusudi either kwa sababu za rushwa kutoka CWT au kwa kutojua sheria za vyama vya Wafanyakazi.

Nijuavyo mimi, barua yoyote inayofika ktk ofisi ya umma na inahitaji kusainiwa na kiongozi husika ni sharti isainiwe vyovyote vile pasipo masharti yoyote Yale. Sasa hawa Wakurugenzi wa Halmashauri wanapata wapi uhalali wa kulalia barua za Walimu wanaotaka kujitoa kwenye mateso ya CWT, chama ambacho kwa miaka mingi kimekuwa kikilalamikiwa na Walimu. Hawaoni kuendelea kukaa na hizo barua ni kutengeneza mazingira ya rushwa?

Nyie Wakurugenzi mnaokataa kusaini barua za Walimu tambueni CWT ilikuwepo kabla yenu na mtaiacha na mkiendelea kushupaza shingo ipo siku zitavunjika. Tena Wengine ni Waislam na Wakristu kabisa na wamefundishwa kutenda haki lakini kwa makusudi wanadharau maandiko ya dini zao. Imani na maadili yenu yako wapi hapo. Taarifa za hao Wakurugenzi zipo na muda ukifika majina yao na Hamashauri zao zitawekwa hapa.

Walimu wamekuwa wakinyanyasika sn kupitia hawa Wakurugenzi wanaovunja sheria kwa makusudi. Walimu wakitaka kwenda masomoni shida, kuanzia kwa wakuu wa Shule wanakataa kusaini barua zao, Walimu wakiwa na shida za kifamilia kupewa ruhusa hadi wawapigie magoti, Walimu wamekuwa wakilazimishwa hadi kutoa pesa za kukimbiza Mwenge. Ukiwauliza hao Wakurugenzi wanatumia sheria ipi au kifungu kipi Cha sheria au muongozo upi kunya hayo yote wanabaki hawana majibu. Mwishowe Walimu wamekuwa watu wa kukata tamaa na kufundisha watoto wetu ilimradi wapate mishahara tu siyo kwa sababu ni Walimu wasomi na walezi wa watoto wetu.

NB:
Km kuna kiongozi yeyote wa serikali hajui, basi kuanzia leo ajue kuwa barua yoyote inapofika ofisini kwako na kuhitaj kusainiwa hakikisha unafanya hivyo pasina masharti yoyote kwani sheria,na taratibu za ofisi ya umma zinakutaka kufanya hivyo na Wala siyo hisani. Tunataka hawa Walimu watufundishie watoto wetu pasipo na stress za mwanadamu.
 
daah.......babu yangu hajawahi pitia haya mambo .., aliamua kuvua samak tu baharini, circle yake ilikuwa Nyumbani baharini na msikitini....
 
Mimi nawashauri tu kama mambo yapo hivyo acha kazi Fata mishe zingine
Tatizo huwa halitatuliwi kwa kutengeneza tatizo. Uzuri ujumbe umewafikia walengwa na wamo humu, hata mheshimiwa hupitia nyuzi zetu humu anatukubali sn wana jamii forum.
 
Back
Top Bottom