Hivi duniani kuna mdudu msumbufu kama KUNGUNI?

Hivi duniani kuna mdudu msumbufu kama KUNGUNI?

Hao kuwaua ni simple tu. Nunua petrol hata robo lita na uchanganye na sabuni ya unga sana sana omo, au ukipata aerial afu uwanyunyizie kaz kwisha. Afu ulete mrejesho hapa. Na ukumbuke sabun ya unga unaweka kiasi hata ndan ya chupa ya maji unatikisa then unatoboa mfuniko kwa juu unanyunyizia zile nafasi unazojua wanaish ndan afu lala kesho tena hivo hivo coz kuna wengne unakuta wamesafiri kidogo sa wakirud uwasambaratishe kwa style hiyo hiyo. Utanishukuru baadae
 
Shuleni walitutesa sana hawa jamaa.

Nilikuwa naosha hadi chaga na kuimwagia maji ya moto na dawa.

Lakini usiku kwenye neti unawaona wajuba wanapanda.

Tena mida yao ni ile usiku mnene. Ndio wanapanda kwenye neti.
Kwa boarding school inawezekana kwa kuwa tabia za wanafunzi zinaeleweka.

Niliwahi kusoma shule moja moshi bweni moja kwa wanaume kuna form 1 hadi 4 kila aina ya ujinga unapatikana humo ndani.

Ila kwa mtu mzima na familia yako au bachelor kukutana na huyu ni dalili za uchafu.
 
Aisee,sijawahi kuona kunguni Wala chawa.
Usikute ulipo yupo na hujui hilo sababu anajua kujificha kama nyoka. Ukiona madoa ya damu yasiyo ya kawaida kwenye shuka, madoa meusi kwenye godoro , neti au chaga. Basi jua hizi ni dalili za huyu kiumbe.

Unaweza kuwapata kwenye siti za daladala, makochi au vyumbani ukiwa ugenini au kijijini. Wakatulia tulj ukarudi naye nyumbani kwako, wakifika hawajioneshi wanatafuta mahali mbali wanazaliana vya kutosha. Ukija kumwona mmoja jua kuna jeshi. Wanakaa kwenye nguo, viatu, godoro kitandani, vifaa vya umeme..
 
Kunguni nimewajulia CIVE Aiseeee
Ila secondary shule zilizopo sehemu ya bard haya mambo hakuna kabisa.

Cive kuna kunguni sijui sasa hvi nahisi wamebiresha naskia wameweka magodoro mapya.

Ile ishu ya kunguni ilifanya mpaka nikapata wazo la kuwa naua kunguni kama kuna watu wa CIVE hapa nazani watanijua .

Nilikua najiita mr cleaner nilikua napiga hawa wadudu kiasi ambacho nikifika room tuu wadudu wanajua kumbiana "" Amekuja the punisher amekuja jamani kimbieni""

Dawa nilizokua natumia aiseee ni hatare an mpaka wakaniamini yaan mpaka uongozi wa madom wakaniamini nikawa sasa natambilika mpaka na ma waden.

Na hapa ndo nitakuja kutoa kisa cha kuanza kupenda mashangazi baada ya kutoka chuo....
Mwanetu ulikuwa na mahusiano na Warden nini?
 
Uwezo wa kifedha wa kununulia dawa ya kuwaangamiza, muda wa kuchemsha maji ya kuwaangamiza i.e. mtu anakuwa saa zote huko anabangaiza, kuwepo kwa mazingira rafiki kwa hao wadudu (uchafu).
kwenye maduka ya pembejeo za kilimo utakutana na sumu kibao za kuwaua kunguni...Ukipata sumu kama Dudu accelamectin (yenye kiambata cha Abamectin na Acetamiprid) changanya na maji kisha wapulizie...wanakufa wao na mayai yao.. kichupa cha Robo hakizidi sh 8000
 
Kunguni ukimuua huwa ana harufu kali mithili ya Corriander aka Kotmir au cilantro..!!

Wanaitwa Bedbug..kwasababu wanapenda sana kunificha sehemu za karibu na kitanda. Mchana wanajificha na usiku hutoka kuvamia kitanda kwa ajili ya kufyonza damu ya binadamu.
 
Shuleni walitutesa sana hawa jamaa.

Nilikuwa naosha hadi chaga na kuimwagia maji ya moto na dawa.

Lakini usiku kwenye neti unawaona wajuba wanapanda.

Tena mida yao ni ile usiku mnene. Ndio wanapanda kwenye neti.
Hao hata usipokilalia kitanda chako kwa miezi sita ukirudi utawakuta wapo wanakusubiri.

Maji ya moto unakomaza mayai yao tu
 
Usikute ulipo yupo na hujui hilo sababu anajua kujificha kama nyoka. Ukiona madoa ya damu yasiyo ya kawaida kwenye shuka, madoa meusi kwenye godoro , neti au chaga. Basi jua hizi ni dalili za huyu kiumbe.

Unaweza kuwapata kwenye siti za daladala, makochi au vyumbani ukiwa ugenini au kijijini. Wakatulia tulj ukarudi naye nyumbani kwako, wakifika hawajioneshi wanatafuta mahali mbali wanazaliana vya kutosha. Ukija kumwona mmoja jua kuna jeshi. Wanakaa kwenye nguo, viatu, godoro kitandani, vifaa vya umeme..
Aisee,basi wasumbufu,,,Niepushwe nao hivyo,,waendelee tu kujificha😐🙌
 
Back
Top Bottom