Hivi CCM huwapa nini Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na kupelekea wao kukaa kimya hata pasipobidi!?

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,193
Hilo ndilo swali huwa najiuliza siku zote.

Wazi huwa yapo mambo mengi ambayo kwa macho ya kawaida kabisa, huhitaji Vyombo vya Dola viikemee Serikali inayoongozwa na CCM kwa kuhatarisha usalama wa Taifa. Ajabu wala hawajishughulishi!

Mbaya zaidi, CCM hutumia sababu ya machafuko kama silaha ya kuwatisha wapenda haki eti Nchi itasambaratika.

Shime wana usalama, wakati umefika muwe upande wa Wananchi wa kawaida. Kuendelea kuilea CCM kama mtoto pendwa ipo siku ulezi huo utazaa haramu.
 
Jeshi halifanyi siasa. Wa kuwaadhibu wanasiasa ni wananchi. 40% tu ya raia katika mikoa yote wakiamua kuiondoa ccm kwa kuingia barabarani ccm inatoka. Sasa walio tayari kwa hili % ni ndogo sana kulinganisha na ambao wanaona bora hali tuliyo nayo iendelee kuliko mbadala wake.
 
Mbaya zaidi, CCM hutumia sababu ya machafuko kama siraha ya kuwatisha wapenda haki eti Nchi itasambaratika.

Huwezi kuteuliwa kwenye hivyo vyeo kama siyo Kada wa ccm
 
Jeshi lipo kwa ajili ya kulinda raia, amani, mipaka ya ardhi na mali za raia na si jambo lingine.

Uchaguzi u karibu mnoo, Tupe mbadala wa CCM tujipime na kama hatutoshi raia wataamua.

2025-2030 CCM ITAPEWA TENA NAFASI YA KUIONGOZA NCHI YETU.
 
Hilo ndilo swali huwa najiuliza siku zote.

Wazi huwa yapo mambo mengi ambayo kwa macho ya kawaida kabisa, huhitaji Vyombo vya Dola viikemee Serikali inayoongozwa na CCM kwa kuhatarisha usalama wa Taifa. Ajabu wala hawajishughulishi!

Mbaya zaidi, CCM hutumia sababu ya machafuko kama siraha ya kuwatisha wapenda haki eti Nchi itasambaratika.

Shime wana usalama, wakati umefika muwe upande wa Wananchi wa kawaida. Kuendelea kuilea CCM kama mtoto pendwa ipo siku ulezi huo utazaa haramu.
Siraha = silaha. Wewe hadi unaandika huu uzi ukiwa unajamba hapo kwa hawara yako unadhani unadhani imetokea tu kwa bahati mbaya? Acha kuwaza upumbavu. Hamia mashariki mwa Congo ili ujue kazi nzuri inayofanywa na serikali ya CCM kulinda raia wake ukiwemo wewe.
 
Jeshi halifanyi siasa. Wa kuwaadhibu wanasiasa ni wananchi. 40% tu ya raia katika mikoa yote wakiamua kuiondoa ccm kwa kuingia barabarani ccm inatoka. Sasa walio tayari kwa hili % ni ndogo sana kulinganisha na ambao wanaona bora hali tuliyo nayo iendelee kuliko mbadala wake.
Sio kweli kuwa jeshi halifanyi siasa.

Hii ni nchi yenye chembechembe za ukomunisti na katiba yetu ipo wazi kuwa ni nchi ya kijamaa pasipo kujali tunaufuata kama inavyo takiwa au laaah.

Nchi za kikomunisti jeshi linakuwa na kitengo ndani ya chama na hivyo siasa jeshini zinakuwepo.

Moja ya jukumu la jeshi ndani ya nchi za kikomunisti ni kulinda chama na nchi.

Chini ya utawala wa Mwl. Nyerere siasa majeshini official kabisa zilikuwepo na kitengo kilikuwepo bila kificho.

Jeshi la JWTZ moja ya majukumu yake ni pamoja na kuhakikisha usalama wa chama namaanisha CCM na taifa hii hatakama sio official ila moja ya kazi yake.

Ndani ya mfumo wa kikomunisti jeshi linakuwa chini ya chama hivyo jeshi linakuwa sio independent bali maamuzi yake yana tegemewa na utashi wa chama na amri jeshi mkuu ndio mwenyekiti wa chama cha mapinduzi.

Nitakupa mifano wa nchi za kikomunisti zilizo hai sasa China, Vietnam, North Korea majeshi yao yote yapo chini ya vyama vyao vya kikomunisti.

Remember sisi ni wakomunisti uchwara ( wajamaa ) kwa mujibu wa katiba ya JMT na kukumbusha pia wakati wa Mwalimu kauli mbiu ya zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM majeshini zilitumika sana ni sasa tu wanajificha kidogo.

Sisi tulihama mfumo wa chama kimoja kwa maneno sio kwa matendo na ndio maana hata katiba haikubadilika kukidhi mfumo wa vyama vingi kwetu serikali na chama ni kitu kimoja na serikali ipo chini ya chama.
 
Hilo ndilo swali huwa najiuliza siku zote.

Wazi huwa yapo mambo mengi ambayo kwa macho ya kawaida kabisa, huhitaji Vyombo vya Dola viikemee Serikali inayoongozwa na CCM kwa kuhatarisha usalama wa Taifa. Ajabu wala hawajishughulishi!

Mbaya zaidi, CCM hutumia sababu ya machafuko kama siraha ya kuwatisha wapenda haki eti Nchi itasambaratika.

Shime wana usalama, wakati umefika muwe upande wa Wananchi wa kawaida. Kuendelea kuilea CCM kama mtoto pendwa ipo siku ulezi huo utazaa haramu.
Ni swali zuri,ila jibu lipo wazi.Wao wanashibishwa na familia zao, so hakuja haja ya kuwajali wananchi.Halafu it seems vetting yao ina lenga kupata watu ambao ni easy to manipulate,kwa hiyo wakishibishwa hawatajali welfare ya wananchi,ila the "status quo."
 
Sio kweli kuwa jeshi halifanyi siasa.

Hii ni nchi yenye chembechembe za ukomunisti na katiba yetu ipo wazi kuwa ni nchi ya kijamaa pasipo kujali tunaufuata kama inavyo takiwa au laaah.

Nchi za kikomunisti jeshi linakuwa na kitengo ndani ya chama na hivyo siasa jeshini zinakuwepo.

Moja ya jukumu la jeshi ndani ya nchi za kikomunisti ni kulinda chama na nchi.

Chini ya utawala wa Mwl. Nyerere siasa majeshini official kabisa zilikuwepo na kitengo kilikuwepo bila kificho.

Jeshi la JWTZ moja ya majukumu yake ni pamoja na kuhakikisha usalama chama namaanisha CCM na taifa hii hatakama sio official ila moja ya kazi yake.

Ndani ya mfumo wa kikomunisti jeshi linakuwa chini ya chama hivyo jeshi linakuwa sio independent bali maamuzi yake yana tegemewa na utashi wa chama na amri jeshi mkuu ndio mwenyekiti wa chama cha mapinduzi.

Nitakupa mifano wa nchi za kikomunisti zilizo hai sasa China, Vietnam, North Korea majeshi yao yote yapo chini ya vyama vyao vya kikomunisti.

Remember sisi ni wakomunisti uchwara ( wajamaa ) kwa mujibu wa katiba ya JMT na kukumbusha pia wakati wa Mwalimu kauli mbiu ya zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM majeshini zilitumika sana ni sasa tu wanajificha kidogo.

Sisi tulihama mfumo wa chama kimoja kwa maneno sio kwa matendo na ndio maana hata katiba haikubaliki kukidhi mfumo wa vyama vingi kwetu serikali na chama ni kitu kimoja na serikali ipo chini ya chama.
Maelezo mazuri boss.
 
Siraha = silaha. Wewe hadi unaandika huu uzi ukiwa unajamba hapo kwa hawara yako unadhani unadhani imetokea tu kwa bahati mbaya? Acha kuwaza upumbavu. Hamia mashariki mwa Congo ili ujue kazi nzuri inayofanywa na serikali ya CCM kulinda raia wake ukiwemo wewe.
....mashariki ipi ya Congo, maana, hata huu mda nipo kwa hawara yangu hapa Bukavu. Ama unamaanisha Kamanyor/la, Butembo, Benii ama Goma!?
 
Bashiru alisema ukiwa na Dola hutakiwi kushindwa 'Elewa kwanza hiyo'.
Wananchi shupavu wakiamua jambolao hawazuiliki hata na haowatu tatizo watu waoga hawana chakujivunia bali kulaumu wengine! Tuliache jeshi
 
Jeshi halifanyi siasa. Wa kuwaadhibu wanasiasa ni wananchi. 40% tu ya raia katika mikoa yote wakiamua kuiondoa ccm kwa kuingia barabarani ccm inatoka. Sasa walio tayari kwa hili % ni ndogo sana kulinganisha na ambao wanaona bora hali tuliyo nayo iendelee kuliko mbadala wake.
Wananchi wapo tayari.

Tatizo wamekosa mtu/chama chakuwaunganisha ili kwa pamoja wadai iwe ni katiba, maisha bora, umeme, maji safi, elimu nk.

Wananchi wengi waTz wanaishi kwa shida sana.

Mbaya zaidi hawafahamu nini chakufanya au kama wanafahamu basi haoni namna yakutia bidii ili haki zake zipatikane.

Ni mtego huo.

Unakumbuka miaka kuanzia 2010 -2015 Chadema ilivyokuwa imeweza kuwaunganisha watanzania hasa vijana kwa kutumia changamoto wanazopitia na Tanzania kwa kiasi kikubwa waliwaamini.

Nini kilitokea baada ya hapo?

Well, nilitaka kukuonyesha watanzania wamepigika na wapo tayari. Imekosekana njia bora yakuwaunganisha.
 
Hilo ndilo swali huwa najiuliza siku zote.

Wazi huwa yapo mambo mengi ambayo kwa macho ya kawaida kabisa, huhitaji Vyombo vya Dola viikemee Serikali inayoongozwa na CCM kwa kuhatarisha usalama wa Taifa. Ajabu wala hawajishughulishi!

Mbaya zaidi, CCM hutumia sababu ya machafuko kama silaha ya kuwatisha wapenda haki eti Nchi itasambaratika.

Shime wana usalama, wakati umefika muwe upande wa Wananchi wa kawaida. Kuendelea kuilea CCM kama mtoto pendwa ipo siku ulezi huo utazaa haramu.
Uko shallow

Wao sio kama wewe mwenye mihemuko
 
Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Yaani hakuna mbadala wa kuwaongoza. Upo sawa mkuu.
 
Kwa kuwa wao sio wapumbavu kama nyie nyumbu wa Chadema.

Yaani wawaachie mvuruge Nchi kisa uroho wenu wa madaraka? Shubaamit
 
Yaani hakuna mbadala wa kuwaongoza. Upo sawa mkuu.
Makosa yalifanywa uchaguzi wa 2015.

Watu wakagawanyika.

Hiyo ni upande wa Chadema chama kikuu cha upinzani.

Sasa hapa kiwe chama kingine chochote kipya au cha zamani kikiweza kuweka strategy nzuri yakuwafikia vijana na kuwaunganisha kupitia changamoto wanazopitia hakika hakuna wakuzuia mabadiliko Tanzania.

Kufanikisha hili inabidi zitumike mbinu mpya hasa na hapa mtandao wa internet utumike kama moja ya nyenzo kufanikisha hili.

Vijana wengi Tz wanalala njaa.

Wamepigika haswaa.

Halafu kila siku wanasikia billions of dollars zinakiwa misused.

Lakini pia vijana wengi wa Tz hawajawahi kupata nafasi iwe kujaribu kuisaidia nchi yao au nchi yao kuwasidia.

Kifupi wametengwa.

Na mtaa unatufahamisha haya.

Ila kwasababu watu wengi wanatembea wakiwa wamefunga macho basi kamwe hawatoona.
 
2015 EL angesema tu watu waingie barabarani sijui ingekuaje.
 
Na vipi ingekuwa Chadema bila EL kupata nafasi yakugombea, Chadema ikasimamisha mtu wao toka ndani ya chama?

Vyovyote vile, kwa hakika matatizo lukuki ya kiuchumi na kijamii, uchumi ikiwa sababu kuu ndiyo inafaa kutumika kuwaunganisha watanzania ili tuondoe mifumo dhaifu iliyopo sasa.

Tukitumia uchama, udini, ukabila, ukanda tutakuwa tunazunguka duara tu.

Mimi binafsi napenda sana kuona sheria ya mgombea binafsi inakuwepo ili viongozi wa kweli bila kuwa na mfungamano na chama anaweza kuwapatia watu wake plan ya maendeleo iwe ngazi ya mtaa, wilaya, jiji au nchi.

Kudhani watu wanaotoka katika vyama vya siasa pekee ndiyo wanastahili kuwa viongozi si sahihi.
 
Back
Top Bottom