Angalizo la CDF Lituamshe Kama Nchi na Turudi kwenye Misingi ya Ulinzi na Usalama

MINENE BOY

Member
Jun 3, 2017
17
14
Kheri za mwaka mpya wanajukwaa!

Nimeona na mimi kama mtanzania niungane na CDF kutafakari kwa kina hali ya ulinzi na usalama nchini.

Naomba niingie moja kwa moja kwenye mada yangu kama inavyojieleza. Ulinzi na usalama wa taifa ni jambo la muhimu kuliko kingine chochote kwenye taifa letu, na suala la ulinzi na usalama ni jukumu la kila mtu kwenye taifa letu.

Lakini kwa umuhimu wake mataifa mengi huunda vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kuondoa dhana ya kutegeana, kwahiyo jambo mahususi hupewa watu mahususi kuliangalia na kuwa sehemu ya majukumu yao ya kila siku pindi sisi tukiendelea na shughuli zingine za kujenga taifa.

Siku ya jana CDF alitoa angalizo kuhusu hali ya usalama wa taifa letu kuwa na matishio kadhaa, ikiwemo vijana wetu kuchukuliwa na kujiunga na makundi ya kigaidi na raia wa kigeni kupenya kwenye mifumo ya nchi na kuteuliwa kwenye nafasi nyeti za maamuzi.

Hii ni ishara tosha kutuonesha kwamba kama taifa kunasehemu tumeanguka kwenye ulinzi na usalama. Anguko hili mimi nalitazama kusababishwa na mambo mengi, lakini manne ya muhimu ni:-
1. Kushuka kwa uzalendo miongoni mwa watanzania
2. Kupungua kwa uwezo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama
3. Viongozi wa kisiasa kupoka mamlaka ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama
4. Ulinzi na usalama siyo kipaumbele tena kwa viongozi wetu.

Naomba nianze kuangalia hoja moja baada ya nyingine.
1. Uzalendo
uzalendo kwa taifa umeonekana siyo kitu cha muhimu tena miongoni mwa watanzania, kizazi cha leo hakioni thamani ya kuwa mtanzania tena na ndio maana kuna watanzania leo wako tayari kulihujumu taifa lao kwa hongo ya vipande vya fedha. Kunawatanzania leo wanashiriki kuficha waharifu tena wanaohujumu taifa lao.

Hii la kushuka kwa uzalendo linasababishwa na viongozi wa taifa letu kwa kutokutoa haki kwa usawa na mgawanyo wa keki ya taifa kwa upendeleo. Hivyo kupelekea makundi mengine kujihisi siyo sehemu ya taifa na kuamua kufanya lolote pasina uchungu kwa nchi yake.

Pia, elimu yetu leo haiwaandai watoto na kizazi kuipenda nchi yao, sambamba na hilo viongozi wa taifa letu wametengeneza mazingira ya kufundisha watanzania kuwapenda wao badala ya kupenda nchi. Hutosikia tena raia, wasanii, viongozi wa dini, wanahabari na wanamichezo wakiisifu nchi bali wanatumia muda mwingi kuwasifu viongozi na vikundi vya viongozi, na kwa kufanya hivyo viongozi nao huwapongeza kwa kuwapa teuzi.

2. Uwezo wa vyombo vya ulinzi na Usalama

Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimepoteza uwezo wake wa kunusa hatari zinazo athiri taifa letu kwa baadaye (madhara ya baadaye). Hapa siyo kwamba watu walio kwenye vyombo hivi hawanauwezo wa kufanya kazi zao kwa weledi, hapana wamewekewa mfumo ambao hauwaruhusu kutumia taaluma zao, na baadala yake wanalazimika kufuata maagizo ya watu nje ya taaluma zao.

Mfumo wa kuwapata viongozi wa vyombo vyetu vya ulinzi siyo rafiki, viongozi wengi wa vyombo hivi wanapatikana kutokana na mahusiano na kiongozi aliyoko madarakani na siyo uwezo wa viongozi hao. Aina hii ya kupata viongozi kwenye vyombo vyetu vya ulinzi itaendelea kutugharimu siku hadi siku kwani vyombo hivi vitazidi kudumaa na kuhatarisha usalama wa taifa letu.

Sheria zinazounda vyombo vyetu vya ulinzi na usalama zimepitwa na wakati, kuna mambo mengi yamebadilika ikiwemo mabadiliko ya sayansi na teknolojia na mabadiliko mengine ya kijamii. Hivyo tunatakiwa kuzitizama upya sheria zinazounda vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Vyombo vyetu vinatakiwa kuwa huru na kufanya mambo yake kwa mujibu wa sheria na kanuni zake na siyo maelekezo.

Vyombo vyetu vya ulinzi vimejikita kwenye kulinda dola, viongozi walioko madarakani na vitu vingine vyepesi ambavyo havina athari kubwa kwa taifa letu. Vimeacha jukumu kubwa la kulinda raia na nchi yetu. Ndio maana ni kawaida kusikia mapandikizi yameteuliwa kwenye nafasi nyeti za maamuzi.

3.0 Viongozi wa Kisiasa kupoka mamlaka ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimeanza kuchangamana na siasa, hili limepelekea kudhofisha vyombo hivi kuanzia kwenye kufikiri mpaka kiutendaji, siyo ajabu tena kuona watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakifanya maagizo (kiki) iliwapate teuzi.

Wanasiasa wametengeneza mazingira ya kuabudiwa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na vyombo hivyo vimeingia kwenye mtego huo. Hapo zamani viongozi wa vyombo vyetu vya ulinzi wahudumu kwenye nafasi zao kwa muda mrefu kidogo, lakini siku hizi wamekuwa wakibadilika mara kwa mara pale tu kiongozi wa kisiasa anapobadilika au kutokuendana.

Viongozi wenye misimamo na wenye uwezo ndani ya vyombo vyetu wanatengwa na kubaki chini mpaka wanastafu, hili huchangia pakubwa kudumaza vyombo vyetu. Hivyo kupelekea kushindwa kutimiza wajibu wao.

4.0 Ulinzi na usalama ni kipaumbele kwa viongozi?

Ulinzi na usalama siyo kipaumbele tena kwa viongozi wetu leo. Viongozi wa kisiasa wametengeneza mazingira ya vyombo vyetu kutumia rasilimali na muda mwingi kulinda vyeo vyao badala ya nchi. Ndio maana ni kawaida kwa kiongozi wa nchi kuvikumbusha vyombo vya ulinzi kukaa mguu sawa kila uchaguzi unapokaribia, kwani ndo muda wao wao wahofu juu ya nafasi zao.

Vyombo vyetu vinatumika waziwazi kulinda maslahi ya kikundi kidogo cha watu, mfano CDM wameitisha maandamo kidogo tu na wito ukatolewa kwa jeshi kuingia mtaani kufanya usafi na hii siyo mara ya kwanza jeshi kutumika kutuliza hoja za kisiasa. Hii siyo salama kwa afya ya ustawi wa jeshi letu, kwa maoni yangu jeshi letu limambo mengi sana ya kufanya kulinda mipaka ya nchi yetu.

Hitimisho:
Angalizo la CDF Lituamshe kama nchi na tujitathimini, kwani haiwezekani nchi jirani zinaingiza mapandikizi ndani ya mifumo ya nchi bila sisi kujua. Vyombo vyetu vinatakiwa kufanya kazi kwa uhuru pasi kuingilia na mtu yoyote, pia, vyombo vyetu vinatakiwa virudi kwenye misingi yake.

Umakini unatakiwa kuongezeka kwenye teuzi za nchi, hususani kwenye nafasi nyeti za maamuzi. Hapa kuna tatizo kubwa sana, Siku hizi vetting haifanyiki kwa umakini ndio maana tunapata viongozi ambao uwezo wao unatia mashaka kwenye jamii. Naomba kuwasilisha.
 
Ukiachana na wanyarwanda , waburundi na wamalawi wamepenetrate mno kwenye system yetu.

Halafu hawapendi tawala zinazosimamia sheria.

Wanapenda tawala zinazuruhusu upigaji maana inakua rahisi kwao kufanya mambo yao.

Utawala kama wa Magufuli na Mkapa hawa jamaa hawakuwahi kuupenda.

Zile kelele za kumpinga Magufuli pia walizianzisha hata wao.
 
CCM wako tayari kufanya KAZI na MTU yoyote maadam atawahakikishia USHINDI WA KISHINDO
 
Sio Kwa KIZIMKAZI yy anawaza kusafiri tu.on to Vatican Soon. Kisha wateule wake wanajipigia Tanganyika
 
Hii nchi iko hatarini kutoweka.
**Mhutu alipata urais.
**Mtusi amepewa unaibu waziri mkuu.
**Msomali amepewa uwaziri wa kilimo.
**Msomali amepewa umakamu mwenyekiti bara wa chama fulani.
** N.k.

Asante CDF kwa kutuamsha!!
 
Back
Top Bottom