The Boss
Kipaumbele cha tano ni amani, umoja na usalama wa mali na maisha ya Watanzania. Amani na umoja wa nchi yetu ni tunu na urithi tulioachiwa na waasisi wa nchi yetu. Marais wote waliopita wamefanya kazi kubwa ya kuzilinda tunu hizi. Serikali yangu haitakubali urithi huu upotee.
Tutafanya jitihada zote ili kujenga maridhiano mapya na upendo miongoni mwa makundi mbalimbali katika jamii yetu. Nitawahusisha viongozi wa dini zote katika hili. Nitaanzisha Jukwaa la Rais na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Jumuiya ya Wakristo Tanzania (CCT) na Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) litakalokutana kila miezi miwili kujadili na kupanga mikakati ya kuendeleza amani, umoja, upendo na maadili ya jamii.

Last edited by a moderator: