Msingi wa siasa za Tanzania uko kidini, kamwe haiwezekani ukatenganisha dini na siasa za Tanzania

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,153
Baada ya Serikali na CCM kubanwa kona zote kuhusu mkataba wa bandari na DP world, watawala na wapambe wao wakaona njia rahisi ni kuwagawa watanzania kidini mpango ambao nao umegonga mwamba.

Hoja iliyobakia kwa watawala ikawa ni kuzifunga mikono na midomo taasisi za kidini zisijadili mkataba wa bandari kwa hoja kuwa siasa na dini hazipaswi kuchangamana.

Hapa chini ni uchambuzi rahisi na makini kueleza ni kwa namna gani siasa za Tanzania msingi wake uko kidini na kamwe haziwezi kutenganishwa.

1. Katiba ya Tanzania
Mwanzo kabisa katika utangulizi wake inatamka, Tanzania ni nchi isiyofuata imani ya dini yoyote lakini yenye kutambua na kuziheshimu imani/dini zote zilizopo kwa watu wake. (Hivyo tamko la TEC (la kiimani!) kupinga mkataba wa bandari linapaswa kutambuliwa na kuheshimiwa (hata kama serikali haiko tayari kulifuata) na mamlaka zote za kiutawala hapa Tanzania kwa mujibu wa katiba)

2. Hakuna sheria yoyote inayozuia wala kukataza imani/dini zisishiriki kwenye mambo ya kisiasa
Ndio maana;

(i)Viongozi wote wa serikali huapa na kuapishwa wakiwa wameshika vitabu vya dini wanazoziamini.

(ii)Mahakamani watu huapa kwa kushika vitabu vya dini.

(iii)Bungeni huapa kwa kushika vitabu vya dini

(iv)Vikao vya bunge havianzi mpaka sala na dua za kidini kufanyika

(v)Wimbo wa taifa wa Tanzania umejaa maneno na vionjo vyote vya kidini

(vi)Maombolezo na mazishi ya viongozi wa juu wa kiserikali kitaifa hufanyika katika misingi ya kiimani/kidini kwa 100%.

(vii)Maadhimisho ya sherehe za kidini ya kikristo na kiislamu hapa Tanzania kila mwaka kisheria ni siku rasmi za mapumziko. (Siku rasmi ya kuadhimishwa kwa sikukuu za Eid kila mwaka kitaifa husubiria na kutegemea tamko la kiongozi wa kidini (kiislamu) na serikali huridhia automatically)


3. Uhuru wa kila mtanzania kushiriki kwenye siasa na dini
Hakuna sheria yoyote inayokataza viongozi wa kidini kushiriki kwenye siasa au viongozi wa kisiasa kushiriki kwenye harakati za dini. Ndio maana

(i)Bungeni, mahakamani na serikalini kuna utitiri wa viongozi wa dini na kwenye taasisi za kidini kumejaa wanasiasa kibao.

(ii)Ni jambo la kawaida sana kuona viongozi wa kisiasa (kuanzia Rais wa Tanzania) kualikwa na kuhutubia kwenye matukio muhimu ya kidini hata kama yeye sio muumini wa dini/imani hiyo, na huko kwa 100% hutoa hotuba za kisiasa!

(iii)Viongozi wa kidini kualikwa ili kuhubiri na kuomba kwenye matukio ya kisiasa ya kiserikali tena kitaifa.

(iv)Viongozi wa kisiasa wa kiserikali kuwaasa watu washike na kufuata vyema mafundisho ya kiimani/kidini.

(v)Mambo muhimu ya kisiasa (kiserikali) kusisitizwa kwenye nyumba za ibada (yaani serikali inaomba taasisi za kidini zitumie pia madhabahau zao kwa mambo mengine yasiyo ya kidini), mfano ni mambo ya uchaguzi, sensa na makazi, Kupinga rushwa, kutunza mazingira, Uzalendo, Elimu, Uwekezaji, Ulipaji kodi, ulinzi na usalama, Afya nk)


Tukitaka siasa na dini zisichangamane hapa Tanzania itabidi kwanza tubomoe misingi iliyopo sasa, na hakuna namna tunaweza tukabomoa misingi hiyo halafu tukaendelea kuwepo kama taifa.
 
Tukitaka siasa na dini zisichangamane hapa Tanzania itabidi kwanza tubomoe misingi iliyopo sasa, na hakuna namna tunaweza tukabomoa misingi hiyo halafu tukaendelea kuwepo kama taifa.
Asante kwa andiko hili, naunga mkono, ila kutumia mimbarini na madhabahuni ya Mungu kwa mambo ya Kaisari .
P
 
Haya majamaa yamechanganyikiwa. Yanasahau hata yanapoapishwa hayashiki katiba bali vitabu vya kanisa na msikiti.
 
Waache kuongoza kwa mazoea, KAZI ya dini ni kukemea mabaya, mbona wakiwa wanasifiwa huwa hawasemi hivyo, mwendazake walikuwa Hadi wanataka kumpa utakatifu . Madhara yatakayo letwa na hii mikataba mibovu itaathiri watu wadini zote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom