Hili la January Makamba ni hatari zaidi

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,906
Niseme kuwa katika wagombea wa CCM angalau January katoa 'picha' atakuwa Rais wa namna gani akiweza kufika.....wengine wengi hatujui misimamo yao ya mambo mengi.

Sasa leo katika hotuba yake ya kutangaza nia January kazungumzia 'ufa wa kidini'na kwa mawazo yake akipewa Urais basi ataunda 'baraza maalum la viongozi wa dini'eti kazi yao iwe kukutana kila baada ya miezi miwili na kujadili namna 'ya kutunza amani'na kuondoa huo mgawanyiko wa kidini.

Binafsi naona likifanyika hilo ndio nchi itaingia kwenye mgawanyiko mkubwa zaidi wa kidini umoja wa watanzania, amani upendo na mshikamano haupo sababu ya viongozi wa kidini.

Watanzania wengi wamechanganya dini kwenye familia zao na wanashirikiana vizuri tu kuanzisha Taasisi zitakazo wapa sauti viongozi wa kidini ndio itakuwa 'platform' ya wao ku manipulate 'their influences' na ku gain more voice za kuwagawa wananchi.

Kinachohitajika ni kuwaacha na kuwa na serikali ambayo haiwapi sauti yoyote ile kwenye masuala ya kitaiifa.....'Dini ibaki kuwa ni jambo la mtu binafsi' na viongozi wa dini waondolewe kwenye 'National Affairs' completely.

Tuache kabisa kushirikisha shughuli za kidini na za viongozi wa kitaifa...Sherehe zote za kidini zibaki kuwa za kidini na viongozi wa kitaifa hasa wa serikali.

Wasihusike na wala wasiende kwenda kuhutubbia masuala ya kitaifa ndani ya misikiti na makanisa.

Kama tuko serious na kutenganisha dini na siasa....basi tusiruhusu hizi idea za January kupewa nafasi.

Mawazo ya January kwa juu yanaonekana mazuri sana lakini kiukweli ni mawazo hatari sana sababu yatazidi kuwapa nguvu isiyo ya lazima viongozi wa kidini.

Watu kama Gwajima watajikuta wanapewa 'umuhimu wa kitaifa' usio na lazima kwa kupitia vyombo kama hivyo ambavyo January anataka kushawishi viwepo.

Dini ibaki kuwa ni jambo la mtu binafsi na viongozi wa dini waachwe huko huko kwenye mimbari za dini zao.
 
The Boss ndani ya ccm kwa sasa hakuna mawazo mapya yanayoweza kuipeleka nchi mbele zaidi ya kupiga mbinje tu. Yeye anadhani dini na siasa ni kaka na dada ndiyo maana katoa hilo wazo lakini kiuhalisia ni wazo hatari kuliko kawaida hilo baraza akilianzisha litakaa vikao viwili tu cha tatu mgawanyikko utatokea ndipo tutajua ubaya wa dini kuchanganywa na siasa
 
Last edited by a moderator:
The Boss ndani ya ccm kwa sasa hakuna mawazo mapya yanayoweza kuipeleka nchi mbele zaidi ya kupiga mbinje tu. Yeye anadhani dini na siasa ni kaka na dada ndiyo maana katoa hilo wazo lakini kiuhalisia ni wazo hatari kuliko kawaida hilo baraza akilianzisha litakaa vikao viwili tu cha tatu mgawanyikko utatokea ndipo tutajua ubaya wa dini kuchanganywa na siasa

This guy is a human being. Bare that in mind
 
Last edited by a moderator:
January seems to lack appreciation of the time tested concept of "Separation of Church and State" and the need to maintain a secular state.

I suspect though, this proposal of his, is just a ploy to appease and appeal for the support of all faiths and religions, in his quest for the highest office in the country. Based on what I have seen so-far (e.g the cyber crimes Act that he championed) January is not the kinda person who will seek anybody's input on how to maintain peace in the country.If he becomes President, I bet he won't give a rat's ass about what any religious leader has to say, with regard to maintaining peace in the country. He will do as he sees fit, regardless of the consequences.

This January fellow is one to be wary of, as he clearly habors dictatorial tendencies (again this can be inferred from the cybercrimes ACT he championed). He comes across as a Mr know it all. If he becomes President, he will probably suppress a lot of our civl liberties, and if we complain, he will simply tell us he knows what is best for us, so we should just put up or shut up. January appears to be so full of himself!! He strikes me as a very corky fellow, hot headed and immature. Both not qualities befitting a head of state. In my considered judgement, January is not yet presidential material. Maybe in 10 years time, he might by then be mature enough to run a country.

i support at least one of his proposals though:- empowering the PCCB to institute charges before any court in the country, without having to go thru the DPP. This is long overdue!
 
The Boss

Mkuu hapo unemlenga askofu wa kurudisha misukule haukuwa na lolote la kusema sasa gwajima kaingia kwenye hyo hotuba na ulichokiongea kwikwikwikwikwi......
 
Last edited by a moderator:
The Boss

Dini ibaki kuwa ni jambo la mtu binafsi na viongozi wa dini waachwe huko huko kwenye mimbari za dini zao[/QUOTE] Unajua mnachekesha sana kuwasoma wakati mwingine. Nirahisi sana kumuona January Makamba amekosea kusema hivyo wakati kila mkutano niliwahi kuhudhuria wa vyama au sherehe za Kitanzania lazima muanze na Asalaam Aleikum - Asifiwe bwana Yesu Kristo, sasa kama mliona kuna makosa ya matumizi ya dini kwa nini hamkuanza na salaam zenu wenyewe mkaweka maneno jingine badala yake?.

Kumbukeni jamani sisi sote tuna dini zetu ambazo ndio mwongozo wa maisha yetu na hakuna kitu kibaya kama serikali ikipoteza mila na desturi za wale inaowaongoza kwa visingizio vya 'Separation of Church and State" kwa sababu wenzetu walifanya hivyo kwa sababu maalum wakipinga sheria moja tu ya Blasphemy ilowanyima Uhuru wa kutoa maoni. Sisi hatuwezi kuepuka Custom law maana ni sehemu ya jamii yetu na hakuna kitu kizuri kama kuwakutanisha viongozi wa Dini inapohitajika.

Hivi tunavyozungumza hufanyika vikao na mara nyingi vimetoa suluhu ya mambo mengi yalokuwa yakichukuliwa kama chuki baina ya imani zetu jambo ambalo lingeweza kabisa kuleta madhara makubwa kama lingepuuzwa. Isipokuwa nakubaliana na wewe sana tu pale serikali inapowaruhusu viongozi wa dini kutoa mwelekezo kwa kisiasa kwa serikali, kinachotakiwa ni wao kupewa maelekezo na serikali wao ni kama Polisi wetu wana serve na ku protect kwa kufundisha mema na kuonya mabaya.. kazi yao sio kutunga sheria bali wanawajibika kufuata sheria.

Dini haiwezi kubakia kama imani ya mtu binafsi ikiwa sisi wenyewe tunatambulishana juu ya Waislaam/Wakristu kama kwamba ni wafuasi wa ama society fulani. And for that needs to be controlled maana Wayahudi wameweza kudai nchi ni yao kwa kutumia dini na ikahalalishwa dunai nzima na sasa tumeona ISIS wakianza kudai nchi... ni mwanzo wa marudio ya kuhalalisha dini kumiliki nchi - Tujihadhari.
 
Last edited by a moderator:
Mtu akitoa wazo kumpinga inabidi uwe na wazo mbadala unachokizungumza ndio tayari kipo ila tayari kuna nyufa thus why makamba kaja na option nyingine badala ya kutafakari hoja ya makamba imesimamia wapi umekomalia mawazo mgando kweli watanzania wengi vilaza siasa kwanza mambo ya msingi baadae.
 
It is too late, viongozi wa dini siku hizi lazima wapige politics, so it is just important for them to have a platform huwezi kuwaminya Tena... They like it Kama Asali.

Kufuata mfumo wako ni Kama kufumbia macho tatizo ambalo lipo.

To to my opinion wakipewa platform watapunguza hate speaches.

Ila pia alisema anawatumia kujadili maadili ya jamii in general.
 
Back
Top Bottom