Hili la January Makamba ni hatari zaidi

Hili la January Makamba ni hatari zaidi

Mkuu The Boss ,nadhani unaufahamu ule msemo unaosema ‘take the bull by the horns''

Kwa mtazamo wa haraka aliyosema Makamba yanonekana kama tatizo.
Suluhu uliyoshauri ni kuwaacha
viongoziwa dini mbali na siasa. Nzuri kabisa!


Je, viongozi wa siasa wafanywe nini? Kwamba ni makosa kuchanganya dini na siasa lakini ni halali kuchanganya siasa na dini. Mpaka upo wapi?

Kama tunakubali viongozi wa dini wabaki kwenye masinagogi,misikiti na makanisa, basi tuwaeleze wanasiasa wabaki katika majukwa ya siasa, wakienda misikitini au Mkanishani waende kama waumini, si viongozi wa dini

Endapo hatutaweza kusema hayo, basi hatuwezi kuepeuka viongozi wa dini kuwa sehemu ya siasa.

Lakini pia tusiishie kuwaambia wakae huko kwenye dini,lazima tuwarudhishie misahafu na bibilia zao ili wakati wanasiasa wanaapa wasitumie kabisa vitabu hivyo.
 
Mkuu The Boss, mgawanyiko wa kidini umepigiwa debe la kimkakati kwa nguvu na awamu hii ya utawala hasa kuelekea uchaguzi wa 2010 baada ya mkulu kugundua kapoteza popular support aliyoingia nayo 2005 huku Dr. Slaa akiwa tishio la uhakika. Ni kipindi hicho ndio kelele za nchi kuongozwa na mfumo kristo zilipofikia peak. Aidha, tukasikia tishio la Vatican kupitia kutaka kuendelea kutawala nchi yetu kupitia kwa "Padre" zikivuma sana.

Hawa jamaa wakaendeleza porojo hizo kipindi chote hiki ili mkulu angalau awe na some credibility kwenye jamii iliyomstukia ulaghai wake. Ukweli ni kuwa Watanzania katika maisha yetu ya kawaida hatuna mgawanyiko wala tatizo la udini. Huo ni mkakati wa kijinga wa wanaosaka madaraka kihuni.
 
The Boss

Dini ibaki kuwa ni jambo la mtu binafsi na viongozi wa dini waachwe huko huko kwenye mimbari za dini zao
Unajua mnachekesha sana kuwasoma wakati mwingine. Nirahisi sana kumuona January Makamba amekosea kusema hivyo wakati kila mkutano niliwahi kuhudhuria wa vyama au sherehe za Kitanzania lazima muanze na Asalaam Aleikum - Asifiwe bwana Yesu Kristo, sasa kama mliona kuna makosa ya matumizi ya dini kwa nini hamkuanza na salaam zenu wenyewe mkaweka maneno jingine badala yake?.

Kumbukeni jamani sisi sote tuna dini zetu ambazo ndio mwongozo wa maisha yetu na hakuna kitu kibaya kama serikali ikipoteza mila na desturi za wale inaowaongoza kwa visingizio vya 'Separation of Church and State" kwa sababu wenzetu walifanya hivyo kwa sababu maalum wakipinga sheria moja tu ya Blasphemy ilowanyima Uhuru wa kutoa maoni. Sisi hatuwezi kuepuka Custom law maana ni sehemu ya jamii yetu na hakuna kitu kizuri kama kuwakutanisha viongozi wa Dini inapohitajika.

Hivi tunavyozungumza hufanyika vikao na mara nyingi vimetoa suluhu ya mambo mengi yalokuwa yakichukuliwa kama chuki baina ya imani zetu jambo ambalo lingeweza kabisa kuleta madhara makubwa kama lingepuuzwa. Isipokuwa nakubaliana na wewe sana tu pale serikali inapowaruhusu viongozi wa dini kutoa mwelekezo kwa kisiasa kwa serikali, kinachotakiwa ni wao kupewa maelekezo na serikali wao ni kama Polisi wetu wana serve na ku protect kwa kufundisha mema na kuonya mabaya.. kazi yao sio kutunga sheria bali wanawajibika kufuata sheria.

Dini haiwezi kubakia kama imani ya mtu binafsi ikiwa sisi wenyewe tunatambulishana juu ya Waislaam/Wakristu kama kwamba ni wafuasi wa ama society fulani. And for that needs to be controlled maana Wayahudi wameweza kudai nchi ni yao kwa kutumia dini na ikahalalishwa dunai nzima na sasa tumeona ISIS wakianza kudai nchi... ni mwanzo wa marudio ya kuhalalisha dini kumiliki nchi - Tujihadhari.[/QUOTE]


Zamani hizi salaam za 'asaalam alaikum' halafu mtu huyo huyo anasema 'bwana yesu asifiwe'
hazikuwepo kabisa
tayari hapo ni dalili tosha kuwa kuendeleza huu utamaduni ni kuwagawa watu

Hivi haiwezekani mtu kusema 'wakubwa shikamooni' wadogo marahaba na akaendelea na hotuba?

kujifanya tunawaheshimu viongozi hawa wa dini ndo tunazidi kuwagawa wananchi....

Nchi zingine zina sababu zao na sisi pia tuna mengi ya kujifunza lakini kuzidi kuwapa nguvu hawa viongozi wa dini ni hatari zaidi
 
The Boss umetoa madini matupu hapa.Idea yako ni sahihi.

Huwezi kufuta kitu kwa kukipa umuhimu bali kwa kukipotezea na kukipunguzia ushawishi.

Umasikini ndo unawapa watu wa kila aina nguvu ya ushawishi
umasikini ukipungua hakuna mtu atakae kesha nyumba za ibada na kugeuzwa 'msukule'
wa kiongozi wa dini.....January alipaswa kutafuta namna ya kupunguza ushawishi wa viongozi wa dini
kwa ku concentrate na kuondoa umasikini zaidi na kuwa ignore hawa watu
 
The Boss

Mkuu hapo unemlenga askofu wa kurudisha misukule haukuwa na lolote la kusema sasa gwajima kaingia kwenye hyo hotuba na ulichokiongea kwikwikwikwikwi......

Gwajima type wako wengi na ni watu hatari wakipewa nguvu zaidi ya ushawishi nchini
 
Well said mkuu. Tusichanganye mambo ya kidini kwenye secular state maana tukifanya hivyo tutaamsha hisia za udini na nchi itakuwa imegawanyika kwa misingi ya udini. Aliyemshauri hivyo january makamba kampotosha na kama january angekuwa muungwana angefuta kauli yake mara moja ili kutuachia nchi yetu iendelee kubaki katika hali ya amani, upendo na utangamano
The Boss
 
Last edited by a moderator:
The Boss

Naunga mokono hoja.
Dini ibaki kama ilivyo... Uhusiano wa mtu binafsi na Mungu wake. Serikali isizipe "promo" dini hizo kwa namna yoyote na serikali yenyewe nayo isipewe "promo" na dini hizo.

Huyu "February" anahitaji kufukiria upya suala hilo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu The Boss ,nadhani unaufahamu ule msemo unaosema ‘take the bull by the horns’’

Kwa mtazamo wa haraka aliyosema Makamba yanonekana kama tatizo.
Suluhu uliyoshauri ni kuwaacha
viongoziwa dini mbali na siasa. Nzuri kabisa!


Je, viongozi wa siasa wafanywe nini? Kwamba ni makosa kuchanganya dini na siasa lakini ni halali kuchanganya siasa na dini. Mpaka upo wapi?

Kama tunakubali viongozi wa dini wabaki kwenye masinagogi,misikiti na makanisa, basi tuwaeleze wanasiasa wabaki katika majukwa ya siasa, wakienda misikitini au Mkanishani waende kama waumini, si viongozi wa dini

Endapo hatutaweza kusema hayo, basi hatuwezi kuepeuka viongozi wa dini kuwa sehemu ya siasa.

Lakini pia tusiishie kuwaambia wakae huko kwenye dini,lazima tuwarudhishie misahafu na bibilia zao ili wakati wanasiasa wanaapa wasitumie kabisa vitabu hivyo.


Heshima kwako mkuu Nguruvi
ulicho ongea kiko kwenye mawazo yangu

Binafsi natama kuwepo sheria inayopiga kiongozi yeyote wa umma kwenda kuhutubia ndani ya makanisa na misikiti
wakienda huko waende kama waumini wengine....na ikibidi wahutubie wahutubie kama waumini wwengine
iwe marufuku kuripotiwa kama 'news' ya kitaifa.....sasa nakubaliana na wewe namna ya kuchora huu mstari bila kuvunja haki za kiraia na haki binafsi za mtu sio rahisi
 
naungana mkono hawa watangaza nia wa ccm wanatoa mawazo bila kutafakari mbeleni .January Makamba katika hili unataka kuliingiza taifa kwenye vita .
 
Mkuu The Boss, bora umeandika kwa lugha nyepesi na isiyoudhi lakini inayoweka wazi madhaifu ya mkusudiwa. Amenishangaza pale anaposema eti hawezi kuongelea gesi kwa maana kuna miaka kama 10 mbele kabla ya kuanza kuichimba huku bosi wake anataka kuzindua mtambo wa Kinyerezi pale bomba la gesi kutoka Mtwara linapopitia kuelekea B'moyo kabla ya Oktoba!
Any way, anaelewa misingi na mbinu viliyomfikisha alipo na ndio maana limesticky akilini mwake!
 
hauwezi kumpuuza January Makamba kwa kiapnde hicho tu ambacho anaweza kusahihishwa kuliko hao viongozi wengine wenye jana nyingi kuliko leo. Kwa jinsi alivyoongea na kujipanga ameonyesha kukomaa kuliko wenzake waliomtangulia kutangaza nia, na taifa au kiongozi atayepata urais anaweza kutumia mawazo mazuri na kuacha yasiyo mazuri.
 
January seems to lack appreciation of the time tested concept of "Separation of Church and State" and the need to maintain a secular state.

I suspect though, this proposal of his, is just a ploy to appease and appeal for the support of all faiths and religions, in his quest for the highest office in the country. Based on what I have seen so-far (e.g the cyber crimes Act that he championed) January is not the kinda person who will seek anybody's input on how to maintain peace in the country.If he becomes President, I bet he won't give a rat's ass about what any religious leader has to say, with regard to maintaining peace in the country. He will do as he sees fit, regardless of the consequences.

This January fellow is one to be wary of, as he clearly habors dictatorial tendencies (again this can be inferred from the cybercrimes ACT he championed). He comes across as a Mr know it all. If he becomes President, he will probably suppress a lot of our civl liberties, and if we complain, he will simply tell us he knows what is best for us, so we should just put up or shut up. January appears to be so full of himself!! He strikes me as a very corky fellow, hot headed and immature. Both not qualities befitting a head of state. In my considered judgement, January is not yet presidential material. Maybe in 10 years time, he might by then be mature enough to run a country.

i support at least one of his proposals though:- empowering the PCCB to institute charges before any court in the country, without having to go thru the DPP. This is long overdue!

I could now confidently describe him in simple two words 'narcissistic politician'deriving it from your description of Mr Makamba.
 
hauwezi kumpuuza January Makamba kwa kiapnde hicho tu ambacho anaweza kusahihishwa kuliko hao viongozi wengine wenye jana nyingi kuliko leo. Kwa jinsi alivyoongea na kujipanga ameonyesha kukomaa kuliko wenzake waliomtangulia kutangaza nia, na taifa au kiongozi atayepata urais anaweza kutumia mawazo mazuri na kuacha yasiyo mazuri.

Sijasema ninamhukumu kwa hili moja
ninachosema hili moja haliko sahihi ...ni hatari zaidi....
 
The Boss

kwa kuijenga tanzania mpya kunahitajika mawazo yetu wote katika hilo , kwahy hata maoni yako yatafanyiwa kazi kwa kila mwananchi kuchangia tanzania mpya anayoitaka ni ipi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom