Hili la January Makamba ni hatari zaidi

Hata waislam watapata pa kusemea...matamko elekezi wenzao ndo hutoa na kufuatwa...na hii itasaidia sana waislm waswenkwe lupango... anyway basi tu
 
January, hii sasa ndo bom linawezeza kuharibu amani nchini. Sijui team yako ilikagua speech yako before you presented it, au ndo yaleyale yanayoseka kwenye team yako unajifanya unaakili kuliko wote?
Think before you say.
 
Only in JAMIIFORUMS

Whats wrong with kiongozi wa kitaifa kukutanisha viongozi wa dini mbali mbali kuangalia namna ya kuboresha amani na utulivu au ku address any issues walizo nazo?

Hivi inamaana hupendi JK au Mkapa au Nyerere alivyokuwa anakutana na viongozi wa dini?

acha hizo
 
Hivi unafahamu kuwa Chama cha kiongozi wa Ujerumani, Angela Markel ni kinaitwa Christian Democratic Union (CDU) na chama dada ni Christian Social Union? Ideology ya chama ni Social Conservatism, Christian Democtacy an European Unionism. Na hata siku moja hujasikia Wajerumani wamechapana sababu ya udini.

La msingi hapa ni kuepuka ubaguzi wa aina yoyote ile nchini, na kujua Functions of Religion in Society. Dini inasehemu kubwa sana ktk jamii yoyote.

Mwisho, labda ukipata muda jifunze hizi terms mbili: Social Cohesion na Social Stability. Nadhani zitakupa muangaza kidogo wa kujua umuhimu wa dini ktk jamii.
 
It is too late, viongozi wa dini siku hizi lazima wapige politics, so it is just important for them to have a platform huwezi kuwaminya Tena... They like it Kama Asali.

Kufuata mfumo wako ni Kama kufumbia macho tatizo ambalo lipo.

To to my opinion wakipewa platform watapunguza hate speaches.

Ila pia alisema anawatumia kujadili maadili ya jamii in general.
Tatizo la watu wa JF ni pale Muislaam anapozungumzia Dini tu ujue wanaanza kushtuka kuna nini? huyu anataka kufanya nini yaani hata siwaelewi watanzania japo viongozi kibao sio tu wanasema bali wanashauriwa na viongozi wa dini..

Nadhani January amezungumza hotuba nzuri kabisa, japo mimi sikuona kama pale ni mahala pake kwa sababu kawalenga zaidi wananchi badala ya kulenga wanachama wa CCM, wajumbe wa Halmashauri, Baraza kuu na Kamati kuu ambao ndio anawaomba ridhaa yao. Ni kama msg sent waswahili wanasema!

Kila mgombea kaelekeza NIA yake kwa wananchi kama kwamba uchaguzi unaanza na watu wote hao kuiwakilisha CCM, na kibaya zaidi wameshindwa kubomoana wenyewe,, kwa nini uwe wewe sio January, Membe au Lowassa, wengine wanamlaumu rais aliyepo madarakani badala ya kuonyesha kwamba yeye ndiye aayefaa kupokea kijiti sii ndio msemo wao?..Sasa utapokeaje Kijiti ikiwa timu ilodumu miaka 10 ya utawala unaiponda ilihali wewe ulikuwa waziri wa serikali hiyo?. kama mcheza mpira sii ndio unauzwa kesho yake tu.

Watia nia kusema kweli hawaku focus na Chama kama kwamba makundi yao ni bora zaidi ya chama hivyo wametaka kuridhisha wananchi wengine wamekwenda Kulia na kushoto, wajamaa sii wajamaa mabepari sii mabepari. Hivyo miminadhani wagombea wana kazi kubwa sana kupita NEC na CC kutokana na nia zao. na ikibaya zaidi UADILIFU aloonyesha Membe kwa chama kuwepo toka mwaka 1977 miaka 20 baadaye ndio anapewa uongozi wa juu watu wamekashifu wakati hii ni Plus Plus kuonyesha UADILIFU kwa chama.
 
Mbaya zaidi upande wa waislam atachukua bakwata wakati kuna jumuia kibao na bakwata gains mandate ya kuwawakilisha waislam wote.
 
Mtusi hasa banya milenge machafuko kwake ndio deal,
huyu jamaa ni mdini sana anajificha kwenye siasa tu sio mtu mzuri hata kidogo ataliingiza Taifa kwenye matatizo zaidi.
 
Naomba nami kupata update, je baba Mtu (Mzee Makamba) alikuwepo? Je dada mtu (Mwanvita) alikuwepo?
Walikuwepo wote hao plus Mama mzazi wa January na babu mtu, yaani baba yake mzazi mzee Yusufu.

Kwa kifupi ingawa tukio hilo la utangazaji nia, katika hali ya kawaida ni very minor, familia ya Makamba ililichukulia kuwa very big issue kwao, pengine wameliona kama tukio la karne!
 
Mtusi hasa banya milenge machafuko kwake ndio deal,
huyu jamaa ni mdini sana anajificha kwenye siasa tu sio mtu mzuri hata kidogo ataliingiza Taifa kwenye matatizo zaidi.
Hata ukiingalia wahudhuriaji wa tukio lile, wavaa 'barghashia' walionekana kwa wingi.
 
Viongozi wa dini ni akina nani?
Kwa upande wa wakristo ni wakatoliki na walutheri? Je wapentekoste?
Kwa upande wa Waislamu ni BAKWATA? Je hao wengine?
Kuunda baraza peke yake itakuwa tabu sana.

Huyu January anayetaka urais ni yule aliyekuwa anapata pesa ili kuwawezesha watu kumwona rais? Je akiwa ndio rais mwenyewe itakuwa vipi?

Kwamba January anaweza kufikiria kugombea urais ni kielelezo cha jinsi taasisi ya urais ilivyokosa heshima Tanzania. Tumekuwa nchi ya wafu wanaongoja kuzikwa.
 
Umenena, dogo hatumii akili. Ila bado sijaona mgombea serious zaidi ya edo
Kilichonishangaza zaidi katika hotuba yake huyo dogo ni 'kuwakandia' vikali wagombea wenzake wote waliodai kuwa nchi yetu itakuwa inaingia kwenye uchumi wa gesi kwa siku za karibuni, akidai kuwa expectations hizo ni sawasawa na day dreams!

Kwa maelezo yake yeye mwenyewe January ni kuwa Tanzania tusitegemee kuona matunda ya gesi iliyogunduliwa kwa wingi sana kusini mwa nchi yetu, ambapo hadi sasa gesi ambayo ishagunduliwa inafikia 56 trillion cubic feets ambayo ni equavalent na 10 billions crude oil barrels.

Akadai kuwa muda wa awali kabisa kutegemea uchumi huo wa gesi ni sio chini.ya miaka 10 toka sasa.

Swali kubwa la kumuuliza January, hivi lile bomba ambalo tunaambiwa na watawala wetu kuwa lishakamilika kutandazwa toka Mtwara kuja Dar, ambalo ujenzi wake tumepata mkopo wa Exim bank ya China ya more than 1.5 billion US dollars, hivi hilo bomba litakuwa linatuletea matope?!

Nina wasiwasi kuwa huyo jamaa pengine ana mpango katika kipindi chote cha miaka 10 atakayotawala (iwapo atapata ridhaa ya waTz) basi pesa hizo za gesi 'wazipige' yeye na wapambe wake!
 
Kumbukeni jamani sisi sote tuna dini zetu ambazo ndio mwongozo wa maisha yetu na hakuna kitu kibaya kama serikali ikipoteza mila na desturi za wale inaowaongoza kwa visingizio vya 'Separation of Church and State" kwa sababu wenzetu walifanya hivyo kwa sababu maalum wakipinga sheria moja tu ya Blasphemy ilowanyima Uhuru wa kutoa maoni. Sisi hatuwezi kuepuka Custom law maana ni sehemu ya jamii yetu na hakuna kitu kizuri kama kuwakutanisha viongozi wa Dini inapohitajika.



Dini haiwezi kubakia kama imani ya mtu binafsi ikiwa sisi wenyewe tunatambulishana juu ya Waislaam/Wakristu kama kwamba ni wafuasi wa ama society fulani. And for that needs to be controlled maana Wayahudi wameweza kudai nchi ni yao kwa kutumia dini na ikahalalishwa dunai nzima na sasa tumeona ISIS wakianza kudai nchi... ni mwanzo wa marudio ya kuhalalisha dini kumiliki nchi - Tujihadhari.

Mkandara mawazo yako ni mazuri ila umechanganya mada, Wayahudi nchi waliyoidai ni yao bila kutumia dini au kutumia dini hiyo ni FACT, wakati ISIS Hawana mahali pao hivyo ni vitu viwili tofauti.
 
Hivi unafahamu kuwa Chama cha kiongozi wa Ujerumani, Angela Markel ni kinaitwa Christian Democratic Union (CDU) na chama dada ni Christian Social Union? Ideology ya chama ni Social Conservatism, Christian Democtacy an European Unionism. Na hata siku moja hujasikia Wajerumani wamechapana sababu ya udini.

La msingi hapa ni kuepuka ubaguzi wa aina yoyote ile nchini, na kujua Functions of Religion in Society. Dini inasehemu kubwa sana ktk jamii yoyote.

Mwisho, labda ukipata muda jifunze hizi terms mbili: Social Cohesion na Social Stability. Nadhani zitakupa muangaza kidogo wa kujua umuhimu wa dini ktk jamii.

Mkuu you have a point lakini tusijilinganishe sisi na wajerumani. Wewe fikiria tu zile propaganda za kuwa CUF au CDM ni vyama vya kidini zilivyokuwa na negative impact kwenye jamii yetu sasa ndio imagine tungekuwa na chama kabisa chenye mrengo wa kidini sasa hivi Tanzania si ingelishakuwa vipandevipande?

Naungana na The Boss somehow viongozi wa kidini wasiwe wa matamko bali wawe washauri wa serikali maana serikali nayo ina ubabe sana hivyo kunapokuwa na organization zenye influence katika jamii kama hizi serikali inakuwa inafanya maamuzi yake kwa tahadhali
 
Last edited by a moderator:
makamba kuna mambo kayasema vizuri lakini kuna baadhi kayaharibu. mojawapo ni hili la dini. ni jambo la hatari sana. hilo baraza atakaloliunda litalipwaje? kama ni hela ya serikali ni muendelezo uleule wa kuvunja katiba. any way hakuna wa kuweza kubadilisha mfumo wa ndani ya ccm kama ni mwanaccm.
 
Yeye kachanganya so hii kwake ni kama kete ati hatopendelea upande wowote. . . . .,. To say naye anaona kuna upande unapendelewa!!!

Kila mtu akitumia personal attributes zake kugeuka kuwa sifa dhidi ya wengine tutaishia wapi sijui. . . . . .
 
Only in JAMIIFORUMS

Whats wrong with kiongozi wa kitaifa kukutanisha viongozi wa dini mbali mbali kuangalia namna ya kuboresha amani na utulivu au ku address any issues walizo nazo?

Hivi inamaana hupendi JK au Mkapa au Nyerere alivyokuwa anakutana na viongozi wa dini?

acha hizo

mkuu mtoa mada yuko sahihi. hivi hilo baraza litakaloundwa litatumia fedha kutoka wapi? unatambua katiba yetu inasemaje kuhusiana na mambo ya dini? jambo hili ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu.
 
Back
Top Bottom