Niseme kuwa katika wagombea wa CCM angalau January katoa 'picha' atakuwa Rais wa namna gani akiweza kufika.....wengine wengi hatujui misimamo yao ya mambo mengi.
Sasa leo katika hotuba yake ya kutangaza nia January kazungumzia 'ufa wa kidini'na kwa mawazo yake akipewa Urais basi ataunda 'baraza maalum la viongozi wa dini'eti kazi yao iwe kukutana kila baada ya miezi miwili na kujadili namna 'ya kutunza amani'na kuondoa huo mgawanyiko wa kidini.
Binafsi naona likifanyika hilo ndio nchi itaingia kwenye mgawanyiko mkubwa zaidi wa kidini umoja wa watanzania, amani upendo na mshikamano haupo sababu ya viongozi wa kidini.
Watanzania wengi wamechanganya dini kwenye familia zao na wanashirikiana vizuri tu kuanzisha Taasisi zitakazo wapa sauti viongozi wa kidini ndio itakuwa 'platform' ya wao ku manipulate 'their influences' na ku gain more voice za kuwagawa wananchi.
Kinachohitajika ni kuwaacha na kuwa na serikali ambayo haiwapi sauti yoyote ile kwenye masuala ya kitaiifa.....'Dini ibaki kuwa ni jambo la mtu binafsi' na viongozi wa dini waondolewe kwenye 'National Affairs' completely.
Tuache kabisa kushirikisha shughuli za kidini na za viongozi wa kitaifa...Sherehe zote za kidini zibaki kuwa za kidini na viongozi wa kitaifa hasa wa serikali.
Wasihusike na wala wasiende kwenda kuhutubbia masuala ya kitaifa ndani ya misikiti na makanisa.
Kama tuko serious na kutenganisha dini na siasa....basi tusiruhusu hizi idea za January kupewa nafasi.
Mawazo ya January kwa juu yanaonekana mazuri sana lakini kiukweli ni mawazo hatari sana sababu yatazidi kuwapa nguvu isiyo ya lazima viongozi wa kidini.
Watu kama Gwajima watajikuta wanapewa 'umuhimu wa kitaifa' usio na lazima kwa kupitia vyombo kama hivyo ambavyo January anataka kushawishi viwepo.
Dini ibaki kuwa ni jambo la mtu binafsi na viongozi wa dini waachwe huko huko kwenye mimbari za dini zao.
Imenishangaza hiyo kauli....
Naomba nami kupata update, je baba Mtu (Mzee Makamba) alikuwepo? Je dada mtu (Mwanvita) alikuwepo?
Mkuu you have a point lakini tusijilinganishe sisi na wajerumani. Wewe fikiria tu zile propaganda za kuwa CUF au CDM ni vyama vya kidini zilivyokuwa na negative impact kwenye jamii yetu sasa ndio imagine tungekuwa na chama kabisa chenye mrengo wa kidini sasa hivi Tanzania si ingelishakuwa vipandevipande?
Naungana na The Boss somehow viongozi wa kidini wasiwe wa matamko bali wawe washauri wa serikali maana serikali nayo ina ubabe sana hivyo kunapokuwa na organization zenye influence katika jamii kama hizi serikali inakuwa inafanya maamuzi yake kwa tahadhali
Hii ni mada bora kwa uhai na ustawi wa Taifa la Tanzania na watu wake.
Kuwaweka viongozi wadin kwenye attention nikulipeleka Taifa kuzimu. Madai kadhaa yatazua migogoro hatimae machafuko na mwisho vita kamili.
1. Madai ya migawanyo ya madaraka kwa kuzingatia uwiano wa kidin badala ya taaluma za wahusika yatazuka huko.
2. Madai ya haki za kuchinja yataibukia hukohuko
3. Madai ya usawa wakumiliki resources kwa mitazamo ya din yataibuliwa mf. Mahospital, mashule, miradi nk
4. Madai ya migawanyo ya ruzuku bila kufuata utaratibu wala vigezo yataibuliwa ilmradi kila din ipate.
5. Madai ya kutofuga au kufuga baadhi ya wanyama yataibuliwa hatakama katiba inaruhusu.
6. Madai ya zamu yetu kupata urais siyo din yenu yatazuka nk
Kunamigogoro mingi itaibuka nakulitetemesha Taifa na kufarakanisha mtu na mtu, jiran na jiran, mkowa na mkowa nk.
Hili jambo nilakuliogopa kama ukimwi maana unapoingilia nipatamu sana kwa maambukizi mengi ukiachiambali ajali nk lakin UKIMWI UKIINGIA BALAA, KUTOKA NI MATANGA yaan vilio nakusaga meno.
Tusishabikie na kushangilia kifo tujiweke mbali na madhila balaa na hila za ibilisi. Viongozi wadin waache mbali kabisa na serikali isijingize kubeba gunia lililojaa na lijivuja tindikali aina ya cynide (udin) itatuangamizia Taifa letu.
Hongera The Boss hii ni mada bora na muhim sana kwetu na uhai Taifa kwa ujumla.
Mkuu kuna mengine tunayachukua kama yalivyo maana ukiingia kwa undani zaidi ya imani za dini utagundua kwamba Yesu hakuwa Mkatoliki wala Mrutheri na hata Muhammad hakuwa Sunni wala Shia bali mcha Mungu, haya madhehebu ya dini tumeanzisha wenyewe na hatari yake ni kubwa toka kuanzishwa kwake hivyo bora kuwepo mawasiliano mazuri baina ya vyombo hivi na serikali kama mshauri. Tunachopinga ni serikali kushirikiana na imani hizi ila huwezi kataza mtu na imani yake utakuwa unaondoa uhuru na haki yake.
Uingereza wameweza tu kukomesha Ugaidi wa IRA kwa kuanzisha mawasiliano bora baina ya vyombo vya dini na serikali. leo wameshindwa kuleta salama huko Mahsariki ya kati kwa sababu serikali zinajaribu kuwasiliana zenyewe dhidi ya dini pasipo kufahamu kwamba chimbuko la misukosuko yote hiyo yote ni mawasiliano mabaya yaliyopo baina ya madhehebu na nasaba zao.
Mahala popote pakisha anza ubaguzi wa aina yoyote iwe dini, Ukabila ama rangi basi ni vizuri sana serikali kuwa karibu na vyombo hivyo, kuwasilikiza na hata kuwashauri juu ya sheria na misngi ilojenga Utaifa wao sio dini zao.
Viongozi wa dini ni wa dini wakideka kwa sababu wanakutana na viongozi wa serikali basi hao sii viongozi wa dini maana wanachaguliwa na waumini wenyewe kuwasilisha hoja zao inapobidi.Kuanzisha mawasiliano na viongozi wa dini au kujadili lolote na viongozi wa dini
linaweza kufanyika bila kuunda chombo maalum na kuwapa 'platform'
ya wao kuongeza 'influence' ...katika jamii ambayo hiyo influence inaweza kuwafanya waligawe Taifa
au wengine waanze kudeka.......