Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii style naipendaga sana pia, unafata nyuma tu. Niliwahi fata Land Cruiser VX flani toka HiMo jamaa alikuwa relaxed ni 80-120 sema nilipofika Mombo nikaingia hotelini tukapotezana.
Kabisa mkuu.. Na unakuta jamaa alivyogeuka alafu hakuoni alihuzunika sana..
 
120km/h is enough boss kwa sehemu nyingi za barabara zetu..

Kuna sehemu ni mzuri yes unaweza kanyaga mpaka 140km/h lakini hii isiwe ndio average speed yako..

Alafu mi naona watu wanaokimbia ovyo barabarani akikutangulia sana ni dakika kadhaa tu.. Unakuta labda sehemu ya kula au mbele kuna traffic check unamkuta ndio kwanza na yeye kafika muda huo huo..
Kama wale Dar wanaohama lane kila wakati lakini mwisho wa siku mnakutana kwenye mataa.

Na hii pia ipo kwenye mabasi, kipindi kile hakuna udhibiti mkubwa utakuta basi imejaa siti lakini inakimbia balaa, lakini ile ya nyuma yake zote zinakutana sehemu ya kula. Basi zinatoka Mbeya na spidi za ajabu ila zikifika karib na Moro zinapaki kuogopa faini kituo cha Msamvu, ajabu zinafika muda mmoja Dar!! Ujinga kabisa
 
Hivi barabara zetu unaweza endeesha mpaka 160++ sijui kwa kweli au [emoji856] wazoefu tafadhali aliewahi kupepeta Mashine mpaka 160++ navyo amini kutoka na malori, barabara na kona nyingi labda 140[emoji1]
 
Ni jambo linawezekana hata nilipoenda songea niliwahi sikia kuna mwamba aliitwa Giriki aliwahi fika songea saa 10 jioni...na ailiwekwa ndani wiki nzima.Kipindi hiko hakuna tochi kama sasa sheria hazibani kama sasa kwahiyo usibishe mkuu inawezekana.
Kiswele
 
Guriki hakuwa Tawaqal ya Mbeya?
 
Mimi 2017 sitaisahau natoka Gairo - Dar kufika Moro ukiwa unaiacha morogoro mjini kuna njia imenyooka sana aisee nikaanza ligi lori mimi na IST mimi mdogo wangu, shemeji yangu na bi mkubwa aisee lori la mafuta BIL aisee niliiga kulifata nyuma aisee jamaa aliwahi kurudi kulia baada ya ku overtake aisee ile siku sitaisahau jamaa aliekua anakuja kwa mbele yangu na fuso hakupunguza mwendo lori nalo liovertake halikupunguza mwendo unakanyaga accelerator hadi chini gari ipo pale pale sijui ilikuaje lakini niliwahi kurudi kushoto nikalichomekea hilo lori nililokua nalipita baada ya jambo lile ilibidi nipaki pembeni nikojoe niliapa sitaanzisha ligi tena...barabarani wala kumfata mtu nyuma akihama na wewe unahama ni hatari sana
Hii hatari sana. Mie huwa ninasubiri wa mbele akimaliza ku overtake, nami niangalie mazingira. Kuna siku nilisafiri na Abood, Moro - Dar, mbele kulikuwa na basi nyingine 2, sisi wa tatu. Basi la mbele lika overtake Lori la mbao, wa kwanza na wa pili wakapita, sisi tupo katikati, mbele si ikatokea tanker..... Dereva wa lori akatoa mkono nje anamwambia Abood arudi nyuma. Humo ndani tulipigana vikumbo hatari kwa hizo brekk zilizofungwa.
 
Wewe ulikua na gari gani? Mkuu
 
IT hawafai ndiyo maana wanakula mbanga sana. Juzi kuna polisi walikuwa na Nissan xtrail wanafukuza Honda IT, polisi walitembezwa mwendo mbaya sana na hawakuona hata taa za nyuma za IT zinawakia wapi. Badae wakarudi eti wanakagua maeneo huenda yule mwamba kajificha.. natamani polisi wapewe powerful cars
Ndiyo maana south Africa polisi wana gari aina zote
 
Hivi barabara zetu unaweza endeesha mpaka 160++ sijui kwa kweli au [emoji856] wazoefu tafadhali aliewahi kupepeta Mashine mpaka 160++ navyo amini kutoka na malori, barabara na kona nyingi labda 140[emoji1]
Inategemea na barabara za wapi au kipande kipi cha barabara.

Jumapili iliopita nilikuwa natoka Arusha kwenda Dar.

Kipande cha Mwanga mpaka Mombo nilikuwa nafukia hadi 180kph. Ni mara chache sana nilifika 220kph.
 
Katika hizi gari ulizotaja sijui M5/Subaru wild/Porsche 911 gt3 wewe unamiliki ipi kati ya hizo?
Similiki hata moja kwasababu Tz hakuna barabara ya kuendesha hizo gari.

Ni kujipa mateso tu.
 
Nimetoka mbeya juzi kupitia songea aiseee barabara ina kona balaa sijawahi ona mkeka ambao naamini unaweza maliza 180km/hr ni ule wa makambako pale umetengenezwa vizuri sana sema una matuta
 
Namshangaa barabara hiyo nimepita juzi ukimaliza makambako tu inamashimo kweli kuelekea mbeya afu usiku uwe 140kph sidhani
Sijakuelewa mkuu..una km 170 alaf ukitembea kwa speed ya 160kph itatumika muda gani?
 
Hivi barabara zetu unaweza endeesha mpaka 160++ sijui kwa kweli au [emoji856] wazoefu tafadhali aliewahi kupepeta Mashine mpaka 160++ navyo amini kutoka na malori, barabara na kona nyingi labda 140[emoji1]

Inatokana na kuchanganya kwa gar mkubwa
Nyingine zinahitaj kilometer 6 ndo ifike 180 nyingine kilometer 1
Nyingine ndo kufika 180 adi malaika washuke
 
Similiki hata moja kwasababu Tz hakuna barabara ya kuendesha hizo gari.

Ni kujipa mateso tu.

Haya ni maneno tu
Ila unaziendesha vzr tu
Lambo na ferrari ndo gar zilizochini na zisizomufu barabara nyingi
Ila makampuni mengi gar zao zinapiga misere tu kwenye hivi vibarabara vyetu except kwa matoleo machache sana
 
Back
Top Bottom