Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Bongo hapo nimeshaiona Nissan GT-R na watu wanakimbia nazo fresh tu.

Hopefully anajua GT-R ni nini.
Haya ni maneno tu
Ila unaziendesha vzr tu
Lambo na ferrari ndo gar zilizochini na zisizomufu barabara nyingi
Ila makampuni mengi gar zao zinapiga misere tu kwenye hivi vibarabara vyetu except kwa matoleo machache sana
 
Ifike mahali tubadilike, Barabara zetu % kubwa sio nzuri na zimeharibika...Madereva wengi nao wapo barabarani lakini nao % kubwa hawana maadili ya udereva..unapata wapi ujasiri wa kuanzisha ligi ???ndio maana kuna michezo ya kushindana mwendokasi wa magari na sio humu barabarani kwenye safari za kawaida, huo kwa mtizamo wangu ni USHAMBA sababu unaanzishaje mashindano kama hayo na mtu ambaye huna makubaliano naye kabla kwenye njia inayotumiwa na wengi..?Sometime unakuta Dereva wa gari kubwa au yenye nguvu anapitwa na Gari ndogo anaona kama dharau..how come ?kila mtu ana safari zake na kwa muda wake...Endesha safari yako. Unakuta mwingine ana Gari anapitwa na pikipiki zetu za kichina naye anaamsha kumfukuzia hivi kweli na dereva na akili zako timamu unaadhimia kabisa kushindanisha gari lako na pikpiki zetu za kichina?Tuache hii tunawagharimu wengine kwa ushamba wetu na ulimbukeni na sanasana Watu Tuliojifunzia na Kuvikuta hivi vyombo vya moto ukubwani ndio tumekuwa na hizo mbwembwe. TUBADILIKE LIGI ZA KIPUUZI MABARABARANI SIO UJANJA KILA KITU KINA MAHALI PAKE.
Umesema ukweli mtupu mkuu huu ni utoto ligi kwenye barabara hizi ni kutafuta majanga tu
 
Nimetoka mbeya juzi kupitia songea aiseee barabara ina kona balaa sijawahi ona mkeka ambao naamini unaweza maliza 180km/hr ni ule wa makambako pale umetengenezwa vizuri sana sema una matuta
Ipo mkuu ngoja nitafute ile post
 
Ulikutana na wasiojua kuzitumia gari. Alphard ilikuwa ndiyo saizi yako
Hii gari stamina yake wala sijaikubali kabisa, inaonekana Morano na Mark X hayakua na madereva, ilitakiwa wawaache mbali wewe ubaki na Alphard
 
Nawaza saana juzi niko na subaru nilifika 100 nikaona inavyo chomoka nikawaza sasa 160 ni kifo kabisaaaa manake hata kona hutaiona ..
mkuu subaru ya aina gani hiyo? speed 100 tu? Juzi nimekuja na Escudo tu,ikiwa speed 100km/hr nachat kabisa.
 
Ligi nimestaafu JUZI IJUMAA kwani nimeponea chupuchupu kufa
Wakuu, nimezoea sana kutembea safari ndefu haswa Dar-Kahama-Geita na Dar-Mwanza, mara chache Dar-Bukoba.
Mara nyingi napenda kusafiri jioni au asubuhi sana.

Hizo route nilizozitaja hapo juu hazina Magari madogo mengi usiku, zaidi ya malori na mafuso. So huwa hatujui mambo ya ligi kabisa.

Kuna hii route ya Arusha-Dar na ligi huwa inaanzia pale Njia panda ya Himo, wakuu kuna watu wanapenda kushindana sana, kwenye barabara.

Juzi kati hapa tumetoka Arusha kwenda Dar tulivyofika Pale Njia Panda ya Himo, kulikuwa kuna gari kama tatu ndogo, Mark x nyeupe, Murano moja nyeusi na Alphad ya Silver, plan niliyokuwa nayo nikupoteza muda pale Njia Panda, at least usumbufu upungue barabarani kumbe zile gari zilikuwa zinatafuta abiria wa Dar, mimi kwenye gari ninayoendesha tulikuwa watatu. Sikuwa na wazo la kuchukua abiria.

Ilivyofika saa kumi na mbili kama na nusu hivi yule jamaa wa Alphad akang'oa, baada ya kama dakika kumi, Mark X akang'oa.
Hapo nimepaki upande wa pili wa barabara.

Ukapita tena muda kidogo Murano akang'oa...Tukamaliza mambo yetu tukaanza kuondoka, nilijua nikipiga mashine vizuri nitaenda kuwatoa kabla hata hawajafika Same!!
Tumeanza kutembea sio kwa speed kali hiyo jioni jioni ya saa moja bado watu ni wengi barabarani na mibasi + magari makubwa mengi yakitoka Dar kuja Moshi, Arusha.

Haikuchukua dakika nyingi saana kufika Mwanga, nikaiona ile Murano ndio inaondoka, nikajua labda alikuwa anaongezea abiria, nikawa nimempita mbele kabla ya Kisaranga nikaipita na ile Mark x, Alphad sikuiona. Giza linazidi kuongezeka naona na barabara inapungua jam.

Tumepita Lembeni kwenye Kivuko cha treni jamaa wa Mark X akaovertake kwa speed kali kuianza Tambarare flan hivi kuelekea Same, hapo ndio ikawa shughuli hakuniacha mbali sana, kabla ya sehemu inaitwa mgagao Murano akaniovertake akaenda akaovertake na mark x..

Baada ya Murano kunipita nikagundua Mark X kaongeza speed zaidi kwasababu alianza kuniacha kwa mbali kidogo.

Nikagundua hawa watu kama vile wanafanya ligi hapo road, nikaamua na mimi kujihusisha nao, ule mtiti haukuwa wa kawaida Tukaanza kutembea sasa pita nikupite ikaanza, jamaa wa Mark X tulikuwa tunamuacha sana...

Mpinzani wangu mkubwa alikuwa jamaa wa Murano, hadi tunafika Korogwe, kwenye kona yakuelekea Old Korogwe, kuna beria, tukamkuta jamaa wa Alphad pale na gari nyingine ndogo mbili, zote zinaenda Dar, ebwana eeh kama ni ligi ndio ilikuwa kama vile inaanza piga nikupige,

Jamaa walikuwa wanatoa changamoto sana, hata kusinzia huwezi muda wote unawaza kumtangulia aliyeko mbele yako na kutokukubali aliyeko nyuma yako akupite! Huu mfumo ulifanya tukafika Dar mapema sana! Huu utaratibu wa Ligi kwenye hii barabara sijui kama ni wa kila siku, Kuna mashindano sana.

Ni barabara yenye ligi tena matata sana.
Kuna MwanaJf anayependa ligi barabarani, share na sisi.
 
Chuma hiyo
tapatalk_1554817930145.jpeg
 
Back
Top Bottom