Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Shetani anapoona mnakimbizana kibwege anatabasamu akiwa na glass lake la mvinyo wa damu ambao aliupata katika ajali iliyopita

Na ukifika speed 160km/h unaanza kusikia wimbo wa Jimmy Reeves kichwani ukiimba

‘This world is not my home I'm just passing through,My treasures are laid up somewhere beyond the blue...............’
 
Gari yangu ya kwanza kabisa ya kichovu toyota caldina, hapo natoka Moshi kuja dar na sina uzoefu sana na route za mbali, jamaa wa vits naye akaamua eti kunianzishia ligi, mimi niko 110 kph ananipita speed then mbele anaenda anapaki, nikipita tu huyu tena. Ama kweli ukiwa mchovu hata wachovu watataka ligi na wewe. Sasa hivi hata BMW akileta ligi na mimi ajipange kweli kweli, japo sita sahau kamwe dharau nilizoonyeshwa na vits kipindi nina gari la kichovu

Hata hio Caldina uliyokua nayo hukuamua tu kumnyoosha huyo wa Vitz,ungepata caldina yenye 3s-Gte nyang’au wasingekusogelea kizembe.
 
Ligi za Moshi - Arusha - Mto wa Mmbu tuachie hizo ligi mkuu nina kitu cha BMW hakijawahi kuniangusha, wajapan wanapata tabu sana. Wengine wanahisigi wanafukuzwa na majambazi.

Gari za kijapan naziitaga Prey namfukuza hapo nyuma huku naangalia dash board nitamani nikiona yupo 170 mbishi 180 basi hapo gear box naitupia kwenye sport mode kitu kinashtuka, nawasha indicator ya kuovertake napita kwa kasi ya ajabu naitafuta 200 nahakikisha mpumbavu haoni taa za breki.

Naenda mbele napark namsubiri apite tena . Wengine wakiona nimesimama hahahaha wanaogopa wanapark pembeni wanasikilizia.

Wabongo waoga sana

Tutajie bmw model yako unayomiliki na utuambie ni gari gani hizo za kijapan unazozionea ili tusawazishe uwanja hapa.
 
IT hawafai ndiyo maana wanakula mbanga sana. Juzi kuna polisi walikuwa na Nissan xtrail wanafukuza Honda IT, polisi walitembezwa mwendo mbaya sana na hawakuona hata taa za nyuma za IT zinawakia wapi. Badae wakarudi eti wanakagua maeneo huenda yule mwamba kajificha.. natamani polisi wapewe powerful cars
Ligi za IT hatari sana, gari mpya na jamaa anataka asubuhi yupo mwanza ni balaa
 
Ligi tamu kuanzia saa 10 jioni kutafuta kale kagiza cha saa 1 kasoro baba unakutana na V8 flani STK dereva anayejitambua, ligi inakuwa tamu sana. Yeye anaamini v8 inachanja mbuga na 220 yake mnyama BMW unasoma 240 halafu boss wake amelala hahahaha au na yeye anapenda ligi dereva anamwambia kuna mshezi anakuja kasi hapo nyuma unaona boss anachungulia kwenye mirror unaona v8 inaanza kuchanganya 180- 190 anachezea hapo kijana namuashia indicator napita anapagawa.

Mara mbele mteremko sipiti asije akasema nimetumia advantage ya mteremko nasubiria muinuko tunavyoanza kukamata tambarare basi napita.

Mjerumani nyoko sana BMW forever

Inaonekana mkuu ukiona hizo 220km/h sijui 240km/h zinakupagawisha balaa,ukikutana na ki golf-gti polo kana 300km/h kuna uwezekano ukaogopa kwenda nako ligi kisa umeona dashboard yake kana speed 300.
 
IT hawafai ndiyo maana wanakula mbanga sana. Juzi kuna polisi walikuwa na Nissan xtrail wanafukuza Honda IT, polisi walitembezwa mwendo mbaya sana na hawakuona hata taa za nyuma za IT zinawakia wapi. Badae wakarudi eti wanakagua maeneo huenda yule mwamba kajificha.. natamani polisi wapewe powerful cars

Hahah daah nimecheka sana,kuna polisi na cruiser yao waliikimbiza Subaru wrx sti hahah aisee walienda kusimulia.
 
Usiku sio salama kwa ligi.

Si rahisi kuona zaidi ya 200M, ukiwa speed zaidi ya 100kph, ni ngumu kukwepa hatari ya ghafla.

Usishindane na watu wa magazeti, hao wanapita hiyo njia kila siku tena usiku. Wanaifahamu vizuri sana.

Na usiku kuna ajali nyingi sana za uzembe na kutokosa umakini.

Kuwa makini, usishindane na usiemjua.

Mwezi uliopita kuna noah iliingia nyuma ya trela la trekta ambalo halikuwa na taa wala reflector maeneo ya vijiji flani kabla ya Kabuku! Ilikuwa ligi hivyo hivyo, usiku ni mbaya sana kukimbia speed kubwa
 
Gari yangu ya kwanza kabisa ya kichovu toyota caldina, hapo natoka Moshi kuja dar na sina uzoefu sana na route za mbali, jamaa wa vits naye akaamua eti kunianzishia ligi, mimi niko 110 kph ananipita speed then mbele anaenda anapaki, nikipita tu huyu tena. Ama kweli ukiwa mchovu hata wachovu watataka ligi na wewe. Sasa hivi hata BMW akileta ligi na mimi ajipange kweli kweli, japo sita sahau kamwe dharau nilizoonyeshwa na vits kipindi nina gari la kichovu
[emoji3][emoji3][emoji3] ligi inapendwa na wengi...
 
Back
Top Bottom