Wanasiasa wana dharau sana. Na utakuta nafasi chache zilizopo serikalini wanawapa watoto wao huku watoto wa masikini wakiendelea kulia na kusaga meno. Inauma sana."Vijana waache uvivu, wajiajiri"
Alisikika mzee mmoja alieajiriwa serikalini tokea mwaka 1965 mpaka sasa hajaacha ajira yake.
Wanasiasa wana dharau sana. Na utakuta nafasi chache zilizopo serikalini wanawapa watoto wao huku watoto wa masikini wakiendelea kulia na kusaga meno. Inauma sana.
Duh! Ukoo mzima unamwangalia akawakomboe! Alafu unaambiwa akajiajiri!Hii picha inaongea mambo mengi sana. Wazungu wanasema a picture speaks louder than words. Nikiiona hii picha nawaza mengi sana, hasa kwa vijana wa kitanzania wanaohitimu vyuoni makumi kwa maelfu kila mwaka.
View attachment 2843100
nilikuwa napasikia tu motoni...ila amini nawaambia Motoni ni hapa Tanganyika...!
Hapo sasa. Sijui atajiajirije wakati mtaji wote ameuacha chuoni. Kuna kijana wetu mmoja tumemsomesha pale UDSM digrii ya BA Kiswahili. Baada ya kuhitimu akapata ajira ya kuolewa na kuzalishwa mtoto. Hadithi ikawa imeishia hapo.Duh! Hukoo mzima unamwangalia akawakomboe! Alafu unaambiwa akajiajiri!
Na hana hata biashara ya pipi"Vijana waache uvivu, wajiajiri"
Alisikika mzee mmoja alieajiriwa serikalini tokea mwaka 1965 mpaka sasa hajaacha ajira yake.
Ila huyu naye alizidi, utasomeaje Shahaha ya Kiswahili hapa Tanzania?? Shahada ya namna hii itakusaidia nini ktk maisha yako kwa hapa Tanzania??? Ni vyema vijana hawa wakatafuta taarifa sahihi mapema ktk safari zao za maisha ya kuisaka elimu, wafanye utafiti wa kina mapema juu ya masomo yanayofaa zaidi kusoma kuanzia wakati wanapokuwa kwenye Shule za Sekondari.Hapo sasa. Sijui atajiajirije wakati mtaji wote ameuacha chuoni. Kuna kijana wetu mmoja tumemsomesha pale UDSM digrii ya BA Kiswahili. Baada ya kuhitimu akapata ajira ya kuolewa na kuzalishwa mtoto. Hadithi ikawa imeishia hapo.
Wewe fikiria familia yenyewe ya kimasikini tumejipinda kumsomesha kwa miaka yote 3 halafu ajira anayopata ni kuolewa kwa mahari ya Tsh laki 8. Na bado anadaiwa mkopo na serikali. Ama kweli jehanamu ni hapa hapa Tanganyika.
Siku hizi umeacha comment za kiingereza 🤣mbona sioni ikiongea ...?
EeeHukoo
😃😃mbona sioni ikiongea ...?
Vijana wengine wanajisomea tu ilmradi wapate digrii wakidhani kitaeleweka mbele kwa mbele. Nawaona vijana wengi waliohitimu Bachelors za Education wapo vijiweni wanaendesha bodaboda.Ila huyu naye alizidi, utasomeaje Shahaha ya Kiswahili hapa Tanzania?? Shahada ya namna hii itakusaidia nini ktk maisha yako kwa hapa Tanzania??? Ni vyema vijana hawa wakatafuta taarifa sahihi mapema ktk safari zao za maisha ya kuisaka elimu, wafanye utafiti wa kina mapema juu ya masomo yanayofaa zaidi kusoma kuanzia wakati wanapokuwa kwenye Shule za Sekondari.
Wafanye uchaguzi sahihi wa masomo ya kusomea tangu wakiwa Sekondari na wakiwa Vyuo Vikuu, wasikurupuke au kufuata mkumbo.
Kwa maoni yangu, ni vyema wakachagua au kupendelea kusoma masomo ya Sayansi zaidi kuliko masomo ya Sanaa ambayo kwa kiasi kikubwa soko lake kwa sasa linaonekana kuwa gumu sana hapa duniani.
Wewe unaongea Kwa kutumia hisia wala sio akiliVijana wengine wanajisomea tu ilmradi wapate digrii wakidhani kitaeleweka mbele kwa mbele. Nawaona vijana wengi waliohitimu Bachelors za Education wapo vijiweni wanaendesha bodaboda.
Kusema kweli kuna haja ya serikali kubadili mtaala wa elimu na kuondoa masomo ya kipumbavu kama vile Kiswahili, Civics, History na masome mengine ya kipuuzi ili kuwapa wanafunzi nafasi ya kujikita kwenye masomo ya maana.
Kiswahili kinafundishwa sehemu nyingi huko duniani ni swala la kupata exposure tu huyo utamuonea wivu.Ila huyu naye alizidi, utasomeaje Shahaha ya Kiswahili hapa Tanzania?? Shahada ya namna hii itakusaidia nini ktk maisha yako kwa hapa Tanzania??? Ni vyema vijana hawa wakatafuta taarifa sahihi mapema ktk safari zao za maisha ya kuisaka elimu, wafanye utafiti wa kina mapema juu ya masomo yanayofaa zaidi kusoma kuanzia wakati wanapokuwa kwenye Shule za Sekondari.
Wafanye uchaguzi sahihi wa masomo ya kusomea tangu wakiwa Sekondari na wakiwa Vyuo Vikuu, wasikurupuke au kufuata mkumbo.
Kwa maoni yangu, ni vyema wakachagua au kupendelea kusoma masomo ya Sayansi zaidi kuliko masomo ya Sanaa ambayo kwa kiasi kikubwa soko lake kwa sasa linaonekana kuwa gumu sana hapa duniani.
Sayansi asili (yaàni Sayansi na Teknolojia) ndio inayotawala dunia kwa sasa, whether you like it or not.