The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Ndani ya kipindi kifupi gharama ya bando/bundle ya internet imepanda kwa zaidi ya 45%.
Sisi watumiaji wa Vodacom tulikua tunanunua kifurushi cha Mwezi kwa shilingi elfu 50 na kupata GB 50.
Haikukaa muda kifurushi kikapanda gharama badala ya kupata GB 50 tukapewa GB 37. Mwezi March/April mwaka huu kikapanda tena ama kwa maana nyingine thamani ya shilingi ikashuka tena tukapata GB 32.
Leo nimejaribu kununua kifurushi kile kile kwa Elfu 50 nimepata GB 28.
Hii kiuchumi ni kwamba ndani ya mwaka mmoja thamani ya fedha yetu imeshuka kwa 45% ama gharama za maisha zimepanda kwa 45%. Maana yake ni kua kitu ulichokua unaweza kukinunua kwa elfu 50 leo utakipata kwa elfu 80.
Rais wetu kitu kinachoitwa mfumuko wa bei kimemshinda kabisa kudhibiti. Wafanyabiashara na watoa huduma wanajiamulia bei wanayotaka. Tunaoumia ni sisi walaji.
Tanzania kwa sasa hakuna consumer protection, bei zinapanda kila uchwao. Kufikia December mwaka huu GB 1 itakua elfu 5.
Gharama za bando na maisha kwa ujumla kwa miaka 5 ya Magufuli zilikuwa ni zile zile pamoja na janga la Covid, ila ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya kuupigwa mwingi kila kitu kimepanda bei.
Mama endelea kuupiga mwingi.