SoC03 Bima ya bando nchini Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Aidarus Ally

Member
Aug 18, 2022
8
7
Kulingana na kuwepo kwa changamoto nyingi sana zinazoikumba jamii ya kitanzania kuhusu gharama za bando na kuwepo kwa kutoeleweka namna ipi itumike ili kuwezesha upatikanaji wa gharama nafuu za bando kwa watumiaji wa mitandao, kwa maoni yangu naona namna sahihi itakayotatua changamoto hii ni kwamba serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inatakiwa kuanzisha mfumo unaoitwa "Bima ya bando" ambao utarahisha gharama za bando pia na matumizi yake.

GHARAMA ZA BANDO WAKATI WA ZAMANI

Hapo mwanzo kulikuwa na gharama nafuu kwa watumiaji wa mitandao kama Tigo, Vodacom, Airtel, Halotel na Ttcl. Mfano mzuri watumiaji wa mtandao wa Halotel walikuwa wanapata Mega bytes (mb) 500 kwa shilingi 500, Giga byte(gb)1 kwa shilingi 1000, ambayo kwa kawaida gharama hizi ni nafuu ukilinganisha na gharama zilizoko wakati wa sasa.

GHARAMA ZA BANDO WAKATI WA SASA

Kwa wakati huu ambao Sayansi na teknolojia imekuwa kwa kasi kumekuwa na sura mpya juu ya gharama kubwa za upatikanaji wa bando kwa watumiaji wake, mfano mzuri mtandao wa Vodacom ili uweze kupata Giga byte (Gb) 1 lazima uwe na shilingi 3000 na shilingi elfu moja unapata Mega bytes (mb) 450, Sura hii inaonesha uwepo ughali wa bando.

"BIMA YA BANDO"

Bima hii ni kama bima zingine zinazopatikana nchini tanzania, lakini bima inatakiwa igawanyike sehemu kuu mbili (2) kwa sababu matumizi ya bando yanatofautiana kulingana na kasi ya mtandao.

KASI YA MTANDAO 4G

Matumizi ya bando kwa mtandao wenye kasi ya 4G yanatofautiana na matumizi ya mtandao wenye kasi nyingine, Mfano Mega byte (mb) 500 kwa matumizi ya mtandao wa kasi 4G hazichelewi kuisha tofauti na 3G au 2G.

KASI YA MTANDAO 5G

Matumizi ya bando kwa mtandao wenye kasi ya 5G vile vile yanatofautiana na matumizi ya mtandao wenye kasi kama ya 4G, 3G na 2G. Mfano Giga byte (gb) 1 kwenye mtandao wa kasi ya 5G inachukua muda mchache kuisha kulinganisha na kasi ya 4G, 3G au 2G.

Hivyo basi bima hii igawanyike sehemu kuu tatu(3).

Kuwepo na (1)bima ya bando kwa kasi ya 3G

(2)bima ya bando kwa kasi ya 4G

(3)bima ya bando kwa kasi ya 5G

"BIMA YA BANDO KWA KASI YA 3G"

Watumiaji wote watakaojiunga na bima hii wataweza kutumia huduma ya intaneti kwa kasi ya 3G tu. Hivyo watumiaji wa bima hii watalipia gharama tofauti na watumiaji wa bima zingine za bando. Mfano kwa miezi sita iwe shilingi 37,800/= kwa watumiaji wa mtandao wa kasi ya 3G ndani ya miezi sita(6), hivyo kwa mwaka itakuwa shilingi 75600/=

"BIMA YA BANDO KWA KASI YA 4G"

Watumiaji wote watakaojiunga na bima hii wataweza kutumia huduma ya intaneti kwa kasi ya 4G tu. Hivyo watumiaji wa bima hii watalipia gharama tofauti na watumiaji wa bima zingine za bando. Mfano kwa miezi sita iwe shilingi 42400/= kwa watumiaji wa mtandao kasi 4G hivyo sawa na shilingi 84800/=.

"BIMA YA BANDO KWA KASI YA 5G"

Watumiaji wote watakaojiunga na bima hii watalipia gharama tofauti na watumiaji wengine, mfano watumiaji wa bima hii kwa miezi sita(6) watalipia shilingi 49300 sawa na shilingi 98600/= kwa mwaka mzima.

"KWA NINI BIMA IWE YA MIEZI SITA(6) NA YA MWAKA"

Bima ya bando miezi sita(6)

- bima hii itajumuisha kuwa ni bima ndogo, ambayo itakayo mwezesha mtumiaji kulipia gharama za bando kila baada ya miezi sita(6).

Bima ya bando mwaka mzima

- bima hii itajumuishwa kuwa ni bima kubwa, ambayo itakayo mwezesha mtumiaji kulipia gharama za bando kila baada ya mwaka mmoja.

FAIDA ZA BIMA YA BANDO KWA WATUMIAJI

(1) Gharama nafuu kwa watumiaji

- Bima itawezesha gharama nafuu kwa watumiaji wa mtandao. Mfano kwa miezi sita(6) kwa mtandao wa kasi ya 4G ni shilingi 42400 sawa na shilingi 84800 kwa mwaka, ambayo gharama hizi ni nafuu sana ukilinganisha na gharama zilizopo wakati wa sasa ambao hakuna bima, pasi na kuwepo kwa bima, mtumiaji anaweza kutumia zaidi ya shilingi laki mbili kwa mwaka kwa ajili ya kupata bando ili kuweza kupata huduma ya intaneti.

(2) Kuwepo kwa matumizi halisi ya bando

- Kumekuwa na mwenendo wa baadhi ya watumiaji wa mitandao kutumia hovyo bando kisha kuanza kulalamikia makampuni ya simu na serikali ya kuwa bando zinazowekwa si halisi kwa zinawahi kuisha, na kusahau kuwa kila kasi ya mtandao inavyokuwa kubwa na ndivyo bando linavyowahi kuisha.

FAIDA ZA BIMA YA BANDO KWA SERIKALI NA KAMPUNI ZA MITANDAO

(1) Chanzo cha mapato

- Watumiaji watakapolipa huduma hii ya bima ya bando kampuni zitapata faida kupitia pesa watakazo pokea, pia vile vile serikali itapata mapato kulipia kodi.

(2) Kutatua changamoto za watumiaji wa mitandao ya simu

- Uwepo wa bima ya bando utawezesha kampuni za simu kwa kushirikiana na serikali kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watumiaji wa mitandao hiyo kama vile Tigo, Vodacom, Airtel, Halotel na Ttcl kuhusiana na suala zima la bando.

KWA UJUMLA; Mfumo huu wa bima ya bando ukizingatiwa kwa usahihi unaweza ukatatua changamoto nyingi katika jamii ya Tanzania, na kuwezesha wananchi kupata bando kwa gharama nafuu.

IMG_20230727_061057_228~2.jpg
IMG_20230727_062436_897~2.jpg
 
Back
Top Bottom