Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 52, leo Juni 21, 2023
Kulaza Shule za Bweni watoto wenye umri chini ya Miaka 5
Naibu waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolijia Mhe. Omary Juma Kipanga (Mb) amesema kuwa kibali cha kulaza wanafunzi wa Bweni hutolewa kwa wanafunzi kuanzia darasa la 5 au kinaweza kutolewa kwa kibali maalumu kwa walio chini ya umri huo.
Kuuza Mazao nje ya Nchi
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali haijazuia uuzwaji wa mazao nje ya nchi bali imezuia watu kufanya biashara bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Hussein Bashe, Waziri wa KilimoAmesema "Haiwezekani mtu unanunua mahindi Songea, unapakia kwenye malori, huna business license ya aina yoyote, hata business name kusajili ambayo ni huduma inayotolewa, huna TIN, huna TAX clearance, huna export permit... halafu unataka nchi ikuruhusu kwenda kuuza nje mazao hayo."
Ameongeza, "Malipo hayaonekani katika mfumo rasmi wa fedha, hatuzipati data katika export statement zetu za nchi. Maelekezo ya Rais yako wazi, Mtanzania yeyote anayetaka kufanya biashara ya mazao kwa ajili ya kuuza nje ama kuuza ndani ya nchi akate leseni ya Biashara"
Amewaambia wafanyabiashara wa mazao kwenda kwenye Halmashauri kukata leseni za biashara na TRA kuchukua TIN certificate ili waingie kwenye mfumo rasmi wa biashara ya mazao ya kilimo. Nia ya Serikali ni kurasimisha shughuli za kilimo na shughuli za biashara za mazao ya biashara.
Kodi ya Tsh. 100 kwenye kila lita ya Mafuta
Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema hakubaliani pendekezo la kuongeza kodi ya Tsh. 100 kwa kila lita ya mafuta ya petroli na dizeli inayotaka kuanzishwa na Serikali kwenye Bajeti mpya ya mwaka 2023/24.
Eneo la mafuta huwagusa wananchi moja kwa moja hivyo serikali inapaswa kuongeza ubunifu kwa kutafuta vyanzo vingine vya mapato badala ya kumuumiza mtanzania wa kawaida.
Amesisitiza pia kuongeza gharama ya simenti ni kuwaumiza wananchi pia inakwenda kinyume na sera ya Serikali inayotaka watu wawe na makazi bora.
Mrisho Gambo: Gharama ya Bando imepanda sana, majibu tunayopewa hayaendani na hali halisi
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amesema gharama za bando zimepanda sana nchini.
"Katika kitu ambacho tunatakiwa tukiangalie vizuri ni gharama za bando zimepanda sana. Majibu tunayopewa hayaendani na hali halisi. Unaambiwa sijui zima app hii, sijui fanya hivi...hicho ni kitu kimoja, kitakupunguzia matumizi" amesema Gambo
Kupanda huku kwa gharama za bando kunapunguza ubunifu, udadisi na kujifunza pamoja na kuongeza gharama ya maisha.
Kulaza Shule za Bweni watoto wenye umri chini ya Miaka 5
Naibu waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolijia Mhe. Omary Juma Kipanga (Mb) amesema kuwa kibali cha kulaza wanafunzi wa Bweni hutolewa kwa wanafunzi kuanzia darasa la 5 au kinaweza kutolewa kwa kibali maalumu kwa walio chini ya umri huo.
Omary Juma Kipanga, Naibu waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolijia
Amebainisha kuwa Serikali itaendelea kudhibiti tatizo la watoto wenye umri chini ya miaka 5 kusoma shule za bweni kwa kuhakikisha inachukua inafanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na shule itakayobainika kukiuka maelezo haya itachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria ikiwemo kufutiwa usajili.Kuuza Mazao nje ya Nchi
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali haijazuia uuzwaji wa mazao nje ya nchi bali imezuia watu kufanya biashara bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo
Ameongeza, "Malipo hayaonekani katika mfumo rasmi wa fedha, hatuzipati data katika export statement zetu za nchi. Maelekezo ya Rais yako wazi, Mtanzania yeyote anayetaka kufanya biashara ya mazao kwa ajili ya kuuza nje ama kuuza ndani ya nchi akate leseni ya Biashara"
Amewaambia wafanyabiashara wa mazao kwenda kwenye Halmashauri kukata leseni za biashara na TRA kuchukua TIN certificate ili waingie kwenye mfumo rasmi wa biashara ya mazao ya kilimo. Nia ya Serikali ni kurasimisha shughuli za kilimo na shughuli za biashara za mazao ya biashara.
Kodi ya Tsh. 100 kwenye kila lita ya Mafuta
Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema hakubaliani pendekezo la kuongeza kodi ya Tsh. 100 kwa kila lita ya mafuta ya petroli na dizeli inayotaka kuanzishwa na Serikali kwenye Bajeti mpya ya mwaka 2023/24.
Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini
Amesema tayari kuna zaidi ya kodi 22 na kuongeza Tsh 100 nyingine ni kuongeza mzigo kwa mwananchi, hivyo kuongeza gharama ya maisha.Eneo la mafuta huwagusa wananchi moja kwa moja hivyo serikali inapaswa kuongeza ubunifu kwa kutafuta vyanzo vingine vya mapato badala ya kumuumiza mtanzania wa kawaida.