Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,328
- 8,243
Kwanza kabla ya yote naomba kusema kwamba nchi ya Tanzania ndio yenye bei ya chini zaidi ya bando za internet katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Pili ukichukua wastani wa mshahara wa kila mwezi, inaonekana watanzania ndio wanalipa asilimia kubwa zaidi ya mapato yao katika kununua bando la internet.
Bei za data kwa Tanzania ni dolla za kimarekani 0.75 ($0.75), Uganda ni dolla 1.56 ($1.56) na Kenya ni dolla 2.25.
Wastani wa mapato ya kila mwezi ya kila mtanzania ni dolla 174 ($174), Uganda ni $1291 na Kenya ni $738.
Kikawaida gharama ya bando la GB 5 haipaswi kuzidi asilimia mbili (2%) ya wastani wa mapato ya kila mwezi ya mtanzania, ambayo inapaswa kufikiwa kabla ya 2026.
Kwasasa gharama ya internet bando ni kubwa zaidi kuliko ya asilimia mbili (2%) ya wastani wa kipato cha kila mwezi kwa GB 5.
Bei ya wastani ya GB5 ni Shilingi za Kitanzania 40,960 (USD17.57), ambayo ni asilimia 10 ya mapato ya wastani ya Shilingi za kitanzania 410,147 (USD176).
Ukipiga hesabu bei hiyo ni mara tano zaidi ya bei ya asilimia mbili (2%) ya wastani wa mapato ya kila mwezi.
Na kitakwimu hii bei inawaumiza zaidi wanawake na wakulima.
Ukijaribu kuchambua taarifa zilizowekwa katika jedwali linaonyesha wastani wa mapato na bei za bando la internet kulingana na sekta.
Jedwali linaonyesha gharama za bando ni kubwa zaidi kwa watu wakulima wadogo, ambapo ni asilimia ya ishirini na moja (21%) ya mapato yao.
Bei zilizoorodheshwa zinatokana na takwimu za Septemba 2022. Mwaka 2020, mtu angeweza kununua bando la data la GB 10 kwa Shilingi 10,000 za kitanzania ambayo ni sawa na dolla za kimarekani 4.3 (USD4.3).
Lakini kwa sasa, 9.8GB inauzwa kwa Shilingi za Kitanzania 20,000 (USD8.6), ambayo ni bei mara mbili ndani ya miaka miwili tu.
Kumbe tukifanya bei za bando ziwe nafuu kulingana na kiwango cha maisha cha mtanzania kutaongeza kushiriki na ufikiaji wa habari kwa urahisi.
Imeandikwa na: bandg.editors@gmail.com