Hii nchi tunaipeleka wapi iwapo haya ni ya kweli?

Hueleweki unaongea nini! Ebu tuliza kalio ma akili kwanza wewe bavicha. Baba na mama yako wamekusomesha kwa hela za sisiemu. Usiwapangie wakufuate huko upuuzini.
Una uwezo mdogo sana wa fikra. Kudhani mzazi kujinyima na kumsomesha mtoto ni hisani ya ccm !!. Kwa akili hii utaongozaJe family ?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhh hivi ilichukua muda gani tangu Lowasa alipoacha CCM na kujiunga na CHADEMA na kupewa kugombea Urais?..

Tukumbushane ili kuweka kumbukumbu vizuri
Akchuale ni muda uleule alotumia Mwikwabe kuhamia CCM na kuchukuwa jimbo.lake mwenyewe.
 
Maria Sarungi:
Serious trouble is brewing in Zanzibar! Mark this tweet!
@ccm_tanzania is set to pass an amendment to bar all @ACTwazalendo
opposition candidates with the excuse that you have to be a member of a party for at least 2 years to qualify. This will not end well! #Tanzania

Zitto MwamiRuyagwa Kabwe:
Tuliposema kuwa CCM wana mpango wa kuzuia mamia ya wanachama wa @ACTwazalendo kugombea Urais, Ubunge na Udiwani ktk Uchaguzi 2020, CCM walikanusha. Ndg. @omarshaaban80 juzi alikazia maneno ya Maalim @SeifSharifHamad CCM wakakanusha tena, wakakataa taarifa yao rasmi. Hapa je?

Hapo mwishoni Zitto katika tweet yake kahoji hivyo baada ya mjumbe mmoja wa Baraza la Wawakilishi kusikika katika clip iliyoko mtandaoni akisema anakusudia kupeleka hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi kutaka kuwe na sheria itayozuia waliojiunga na vyama kutogombea nafasi ya uraisi,uwakilishi na udiwani mpaka kwanza wawe wametimiza miaka miwili katika vyama walivyojiunga.
Katika falsafa za sheria, kutunga sheria inayokuwa retroactive (sheria mpya inayorudi nyuma kuhukumu yaliyotokea kabla haijatungwa) ni kitu ambacho hakipendwi sana.

Nina maana gani?

Ngoja nitoe mfano.

Tunaweza kutunga sheria leo. Tukasema, kuanzia kesho, kuvaa shati jekundu ni kosa, ukikutwa umevaa shati jekundu utafungwa au kupigwa faini.

Hiyo sheria itakuwa haina tatizo la kuwa retroactive.

Lakini, tukitunga sheria leo, halafu tukasema mtu yeyote aliyevaa shati jekundu kuanzia January 1 2020 amefanya makosa, wakati sheria tumeitunga February 9 2020, na kabla ya kutunga hiyo sheria watu hawakujua kwamba kuvaa shati jekundu ni makosa, basi sheria hiyo ina tatizo la kuwa retroactive.

Kwa nini falsafa nyingi za sheria zinakataza sheria kuwa retroactive?

Mosi, ni kwa sababu, sheria ikiwa retroactive haimpi mtu haki ya kujua nini ni kinyume cha sheria, mtu hawezi kujilinda ili asivunje sheria kama anatakiwa aifuate sheria ambayo bado haijatungwa. Kwa mfano wetu, mtu hawezi kujizuia kuvaa shati Jekundu January 1 2020, kwa minajili ya kutotaka kuvunja sheria, kama sheria yenyewe inetungwa February 9 2020.

Pili, hizi habari za kutunga sheria na kuzipa nguvu za kurudi nyuma, zinatoa mwanya wa kutegeana. Watu wataanza kutungiana sheria kubana watu au makundi fulani maalum. Hapa gunaona kama CCM wanawaogooa ACT, wamewatungia shwria maalum kuwabana. Kama Kikwete hamtaki Sitta kuwa Spika, anamtungia sheria maalum kwamba sasa tunataka Spika mwanamke. Kama CCM haimtaki Lowassa kuwa mgombea urais, inamtungua sheria maalum ya umri kumkata.

Mwishowe sheria inakuwa ni silaha ya kudhibiti wapinzani wa kisiasa. Si namna ya kupata haki.

Zaidi, kuwanyima watu haki ya kuchaguliwa uongozi kwa minajiki ya umri wa chama ni kuwanyima haki ya kikatiba.

Inawezekana chama chenye mwezi mmoja kikawa kizuri kuliko cha miaka sabini.

Tuache ujinga wa kutumia sheria kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu nakuja kwenye chama dakika mbili mara pap, yeye ndio mshika kibendera. Waliohagaikia chama kama kina Mzee Slaa wanatupwa nje, tena kwa kejeli. That not a level playing field.
mfano mwengine mzuri ni kama kina Waitara vile...
 
Je kama ni star mchezaji wa kulipwa kwa nn asicheze?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui kama umefuatilia ukaona vyama vingi vinashidwa kujenga viongozi wa kesho. Vingi vimebaki kudakia viongozi wa vyama jirani kuliko kutengeneza mazingira ya vijana kustawi. Mifano iko mingi tu tokea vyama vingi vianzishe.
 
Maria Sarungi:
Serious trouble is brewing in Zanzibar! Mark this tweet!
@ccm_tanzania is set to pass an amendment to bar all @ACTwazalendo
opposition candidates with the excuse that you have to be a member of a party for at least 2 years to qualify. This will not end well! #Tanzania

Zitto MwamiRuyagwa Kabwe:
Tuliposema kuwa CCM wana mpango wa kuzuia mamia ya wanachama wa @ACTwazalendo kugombea Urais, Ubunge na Udiwani ktk Uchaguzi 2020, CCM walikanusha. Ndg. @omarshaaban80 juzi alikazia maneno ya Maalim @SeifSharifHamad CCM wakakanusha tena, wakakataa taarifa yao rasmi. Hapa je?

Hapo mwishoni Zitto katika tweet yake kahoji hivyo baada ya mjumbe mmoja wa Baraza la Wawakilishi kusikika katika clip iliyoko mtandaoni akisema anakusudia kupeleka hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi kutaka kuwe na sheria itayozuia waliojiunga na vyama kutogombea nafasi ya uraisi,uwakilishi na udiwani mpaka kwanza wawe wametimiza miaka miwili katika vyama walivyojiunga.
Nosense
 
Lazima tupitie kwenye joto kali sana ili tuweze kujitambua kama binadamu wengine duniani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom