Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583




Wanabodi,

Nimemsikiliza, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe akihojiwa kwenye kipindi cha Mikasi!, (japo kipindi hakikuwa na maswali magumu kivile!, ile hiki ndicho Watanzania wanachokihitaji, vipindi vya maswali magumu type ya "kiti moto" havihitajiki sana kwa audience yetu!.

Kiukweli, tukubali, tukatae, ZZK ni Mzalendo wa kweli wa nchi hii, yuko very patriotic katika suala la Muundo wa Muungano, ZZK ni kama Nyerere, anaamini katika muungano wa serikali Moja!, yenye rais mmoja na mawaziri wakuu wawili!. Huu ndio ulikuwa msimamo wa Baba wa Taifa katika muungano wa serikali mbili kuelekea moja!.

Kwenye hii interview ya ZZK nimempa baadhi ya alama zifuataza kwenye pros and cons.

Tukianza na pros

  1. Uwezo wa Ubongo, akili, mzuri kichwani (Brain Power), Bright, Brilliant, with High I.Q. nampa 100%
  2. Uwezo wa kujieleza ( expressing himself) nampa 100%
  3. Uwezo wa ushawishi ( convincing power) nampa 100%
  4. Ni kiongozi Mtendaji na sio tuu msemaji (action oriented) 100%
  5. Kuaminika (trustworthness) 75%
  6. Uaminifu (Honesty) 75%
  7. Kujijengea heshima (Integrity) 100%
  8. Uwajibikaji (responsibility) 75%
  9. Kujiamini (confidence) 150% (imrekuwa over and above-over confidence)
  10. Kuthamini kazi yake (enthusiasm) 100%
  11. Kijitoa kutumikia watu (dedication) 100%
  12. Kuipenda kazi yake (passion) 100%
  13. Kuingwa mfano (Inspiration) 100%
  14. Muonyesha njia (trend setter) 150% (over and obove lazima awe yeye)
  15. Kupigiwa mfano (role model) 100%
  16. Muhamasishaji (motivator) 100%
  17. Mpanga mikakati (organiser) 100%
  18. Ushirikiano (team player) 50%
  19. Ustahimilivu (endurance) 50%
  20. Uvumilivu (tolerance) 50%
  21. Uchambuzi (analytical) 100%
  22. Kusimamia malengo (keeping focus) 75%.
  23. Kujitoa (commitment) 100%
  24. Uono (visionary leader) 100%
  25. Kazaliwa kuongoza (born leader) 100%
  26. Kajengwa Kuongoza (made leader) 100%
  27. Ukomavu (maturity) 50%
  28. Unyenyekevu () 50%
  29. Uhuru wa kufikiri (independence in thinking) 100%
  30. Urahisi wa kupelekwa pelekwa (follower) 25%
  31. Msimamo usioyumba (Strength of a character ) 100%
  32. Nguvu ya kufanya maamuzi (decisiveness) 100%
  33. Uwezo wa kushikilia maamuzi (firmness) 100%
  34. Uwezo wa kusimama kwenye malengo (objectivity) 100%
  35. Uwezo wa kuhimili vishindo, moyo wa chuma (perseverance) 100%
  36. Mtu mwenye Huruma 100%
  37. Ni Mwenye kujitoa kwa ajili ya Watu.100%
  38. Ni Mtu wa Kusaidia sana "the needy" 100%
  39. Ni Mtu mwenye Uchungu na Maendeleo 100%
  40. Ni Miganaji wa Kweli, hadi risasi ya mwisho, na tone la mwisho la damu 100%

Cons
  1. Kuaminika kwa mashaka
  2. Not a good team player
  3. Not settled emotionally
  4. No stable in love (player)
  5. Umimi egotism.
  6. Kujiamini kupitiliza (over confidence)
  7. Kujikweza (superiority complex)
  8. Kujifagilia kwa sana (boastfulness)
  9. Kuambilika haambiliki
  10. Fault finder hivyo ni perfectionist!.
  11. Immaturity
  12. Kiburi, jeuri
  13. Sio mnyenyekevu kukubali kupelekwa palekwa tuu. (not easily to be pushed around)
  14. Misimamo mikali isiyoyumba (extrimist)
  15. Kinganganizi (persistance)
  16. Mgomvi fulani asiyekubali maonevu, manyanyaso (fighter)
  17. Ana papara (impulsiveness)
  18. Muoteaji (dreamer)
  19. Hajali sana (dare devil) akishaamua ameamua hajali consequences
  20. Kiasi (considerate) not considerate of the consequences or of others
  21. Arrogant,
  22. Power maniach,
  23. Stubborn politician.
  24. Inconsistance, (Sitagombea tena Ubunge, Nitagombea Urais, Natafuta Jimbo, Nitaend kufundisha ...)
  25. Mropokaji

Maeneo yote hayo nimeya observe kwenye mahojiano yake!.

Chama chake kina viongozi wengi wenye uwezo, ila kwa calibre yake, he is the one and only ndani ya chama chake akifuatiwa na JJ Mnyika kwa karibu, wengine karibo wote wako mbali sana!.

Amethibitisha kizingiti za umri kikiondolewa, na sifa za rais tunayemtaka zikikosekana, ataingia kwenye kinyang'anyiro hicho, hivyo na mimi namuweka ZZK kuwa ni number 2 baada ya "yule jamaa yetu!" .

Asante.

Pasco
============================== ===

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amesema atajiunga na chama kipya cha siasa.

Hata hivyo, amesema uamuzi wa kuanzisha chama chake kipya cha siasa utasubiri kwanza uamuzi utakatolewa na mahakama katika kesi yake iliyopo mahakamani inayohusiana na uanachama wake ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Novemba 22 mwaka jana, Zitto alisimamishwa unaibu Katibu Mkuu wa Chadema na unaibu kiongozi wa upinzani bungeni baada ya kutuhumiwa kuhusika na njama za kukihujumu chama hicho.

Zitto alisema hayo juzi wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na kituo cha televisheni cha EATV baada ya kuulizwa kuwa kuna fununu kwamba ana mpango wa kuanzisha chama chake kipya cha siasa.

"Kwa hivi sasa nina kesi mahakamani inayohusiana na uanachama wangu kwenye chama cha Chadema, kwa hiyo siwezi kusema lolote kuhusiana na kuanzisha chama kipya au hapana kwa sababu nasubiri maamuzi yatakayotolewa na mahakama," alisema.
Alisema kwa jinsi ambavyo maamuzi ya kesi hiyo yatakuwa, kwa kuwa ni mwanasiasa na anataka aendelee kubaki kwenye jukwaa la siasa, nia yake ni kubaki kwenye siasa, lakini siyo katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) au katika vyama mojawapo vya siasa vilivyopo.

Hata hivyo, wakati Zitto akisema hayo kumekuwapo na taarifa za kumhusisha Zitto na chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT)-Tanzania kutokana na viongozi wake kuwa ni waliotimuliwa ndani ya Chadema.

Miongoni mwa viongozi wa sasa wa chama hicho ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, ambaye alisimamishwa uongozi sambamba na Zitto, lakini baadaye Chadema kilimfuta uanachama kutokana na tuhuma za uasi.

Mwingine aliyesimamishwa uongozi sambamba na Zitto na Mwigamba ni Profesa Mshiriki Kitila Mkumbo ambaye alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema.

URAIS 2015
Kadhalika Zitto alisema ingawa angelipenda kugombea urais mwakaji, kikwazo ni katiba ya sasa na Rasimu ya Katiba mpya ambayo inaeleza sifa za mtu anayetaka kugombea urais ni lazima awe na umri wa kuanzia miaka 40 wakati katika nchi kama Kenya, Malawi, Marekani, Rwanda, Burundi, Msumbiji na Afrika Kusini ni miaka 35.

Zitto alisema kama hali itabaki hivyo, atamuunga mkono mgombea anayeijua nchi vizuri kwa sababu Tanzania inahitaji rais atakayewaunganisha Watanzania na siyo anayewagawa.

"Tunahitaji rais ambaye haya anayajua na ameonyesha ni namna gani atayatekeleza na siyo blabla," alisema.

KUTUMIWA NA CCM
Zitto alisema amekuwa akisikia baadhi ya watu wakisema kuwa anatumiwa na CCM, lakini bahati mbaya wanaodai hivyo hawaelezi kwa undani anatumiwa vipi na chama hicho tawala.

"Hivi mbunge anayetumiwa na CCM anaweza akapeleka hoja bungeni kutaka kumuondoa madarakani Waziri Mkuu, anaweza akapeleka hoja bungeni ya kuhakikisha mikataba yote inakuwa wazi ikiwamo ya gesi?" alihoji.

Alisema wanaotoa madai hayo wajitokeze waseme wamefanya nini kwa ajili ya taifa lao na kwamba anachofahamu hizo ni propaganda tu za kisiasa na siasa nyepesi za Tanzania ambazo hazina mashiko.

ATOFAUTIANA NA UKAWA
Katika mahojiano hayo Zitto alisema si sehemu ya Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa sababu vyama vinavyounda umoja huo ni pamoja na Chadema ambacho ana mgogoro nacho kutokana na kukifungulia kesi mahakamani akipinga kumvua madaraka.

Alisema ana msimamo tofauti na CCM na Ukawa kuhusu muundo wa Muungano kwani kwa mtazamo wake ni kuwa na Rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar na Tanganyika ziongozwe na mawaziri wakuu.

Alifafanua kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuwa na Muungano imara kwani Muungano wa sasa hautendi haki kwa upande mmoja ambao hata hivyo, hakuutaja.

Chanzo: Nipashe

Watu hawalali mpaka kieleweke!..
semeni mtayoweza lakini Zitto ni miongoni mwa viongozi adimu nchini na hasa ukimsoma tweet zake, mitazamo yake ni ya kipekee ambayo sijawaona viongozi wetu wakitazama mambo muhimu zaidi ktk jamii kama yeye. Leo hii hakuna ni siasa tu za kutafuta kura za wananchi.


Porojo nyingi sana kutoka kwa wanasiasa ni kuchafuana wao, kuchafuana vyama, huyu kafanya hivi yule kalala na nani.. lakini ukiyapima hakuna hata moja linamlenga wala linamhusu mwananchi malalahoi, wanapunguziana mashuzi tu..Wakija kwetu ndio utasikia nitafanya hivi, tutafanya hivi lakini undani wa maswala mazito ya kiuchumi hawajui kitu. Zitto ni jembe ambalo Chadema inalijutia na itaendelea kulijutia ndio maana mawe mengi yanarushwa ktk mwembe huo.
- Kila shetani na mbuyu wake!
Mkuu Mkandara , tulia kidogo tuweke rekodi sawa.


Mwaka 2011 kama si 2012 Zitto aliandika makala gazeti la Raia mwema akitaka muundo wa serikali 3.
Mimi niliandika na kusema hata kama aina ya muundo alioutaka ilikuwa tofauti na nilivyofikiri, bado namsifu kwasababu ni kiongozi pekee aliyejitokeza kusema neno kuhusu muungano.


Wakati huo niliandika(rekodi zipo) kuwa hata CDM kilikuwa hakina msimamo kuhusu serikali 3.
Majadiliano mengi yalifuata baada ya hapo nikiwa namtetea vema kuhusu S3 na kusimama kama kiongozi kueleza kile kilicho wazi. Rekodi zinaonyesha Zitto ni muumini wa S3 bila shaka.


Leo anapozungumzia serikali moja si kutokana na maono au mtizamo wa kijamii kama Mkandara anavyoamini na kutaka kuaminisha umma. Anachokifanya ni kuwa ''opportunist'' ili aonekane ana mtazamo tofauti.
Maoni yake hayana tofauti na ya kile chama kipya, hivyo anachokifanya ni publicity wala si uzalendo.
Hilo tumeliweka sawa na upotoshaji hauna nafasi.


Pili, Zitto anapokataa UKAWA ni mnafiki. Kama ni hivyo angebaki bungeni kutetea hoja yake na CCM kama walivyobaki akina Hamad Rashid, Mrema n.k.


Kitendo cha kujitoa kwa kutumia UKAWA huku akikataa ukawa nje ni tabia ya ''oppotunist''
Pasco
Sifa kubwa sana ya kiongozi ni busara. Leo unaona Pandu akisifiwa katika hatua za mwanzo za BMK si kwasababu ya elimu au mitazamo, ni kwasababu ya busara, hekima na usikivu.
Kiongozi ni mtu anayeweza kusadia kuunganisha vipande vya puzzle na kuelekeza namna ya kupata vipande husika.


Tatizo la Zitto ni ukosefu wa Busara ambao huzaa papara, hamaki, majigambo na vitu vya namna hiyo.
Katika jamii mtu mwenye busara huonekana zaidi kuliko mwenye akili.
Akili si busara, na mara nyingi viongozi wenye busara huweza kuongoza akili, si viongozi wenye akili huwaongoza wenye busara.


Katika mifano yako ya akina Nasser, Nkrumah, Nyerere, Tito, Mandela n.k. ukitazama kwa undani sifa yao kubwa ya viongozi hao ni busara. Angalia mifano na kauli zao, si akili bali busara zao.
 
Last edited by a moderator:
Unaposema chama chake na kumtaja JJ Mnyika una maana Kamanda JJ Mnyika nae ni wa Mahakama au ACT. Pasco kuwa Serious na umshukuru Mungu kwa kukuumba mtoto wa Kiume otherwise ungekuwa unawakubalia wanaume wote Laghai walah vile....
 
Last edited by a moderator:
Wewe pasco kweli gongo ishakulevya vya kutosha, mara useme TeamLowasa mara TeamMatunguli, sasa upo upande gani?
 
Mbona Pasco huu ni msimamo wako wa tangu mwanzo?

Kuna kipya gani kimeongezeka baada ya kumsikia?

Kuna kipengele cha muhimu - Maturity - hiyo unamweka wapi?
 
Last edited by a moderator:
Unatoa 150% umewaunganisha wangapi? Mwanadamu akiwa nazo nyingi sana ni 100 na sio rahisi.

Binafsi namkubali sana Zitto na Asset ya Tanzania. Kweli ndio alikuwa tegemeo langu kwenye Chadema hai. Na namkubali kwa siasa zake na uzalendo. Muungano ndio akigonga palee ninapopatamani kwa 2nd choice, serikali 1 na mawaziri wakuu wa Tanganyika na Zanzibar. ila 1st choice ni serikali moja isiyo na mashart. Vile wanzanzibar wanalivyo hii mhh!

Kabla ya zito ni Mzee wa nchi ya ahadi EL.. sijui ndiyo uliyemrefaa kama jamaa yetu?. Atupeleke waajiriwa kwenye utekelezaji. awapeleke makampuni binadsi waliokuja kuwekeza kwa ajili ya watanzania na ndipo wao.
 
unaposema serikali maana yake ni waziri mkuu na baraza lake la mawaziri katika nchi zenye parliamentary system of government (UK, germany, france etc) au rais na mawaziri wake kwenye presidential system of government (USA, Kenya etc).

Unaposema kuatakuwa na mawaziri wakuu wawili already unaimply uwepo wa serikali mbili. huyo rais atakuwa very ceremonial and weak na atakuwa anaendesha confederation (hata sio federation kama tulivyodanganywa na kina warioba. mfumo huo waliosuggest unaitwa confederation na sio federation) of two governments. hamna tofauti na alichokiandika warioba!

ukitaka kujua tofauti kwenye mfumo wa federation serikali ya shirikisho ndiyo yenye nguvu na mamlaka over serikali za washirika. kwenye confederation, serikali za washirika ndizo zenye nguvu na mamlaka over hiyo ya shirikisho.
 
Zitto Kabwe anatofauti sana na wanasiasa wengi sana wa Tanzania!

Zitto ana nidhamu fulani ya kutowasema vibaya wanasiasa wenzake! kwa hili namfananisha na Lowassa!

Aina ya wabunge vichaa kama LEMA, Hawatakaa wafikie upeo wa Zitto hata robo siku zote za maisha yao!

mkuu itabidi nikushangae,unamtaja godii ?
 
Zitto Kabwe anatofauti sana na wanasiasa wengi sana wa Tanzania!

Zitto ana nidhamu fulani ya kutowasema vibaya wanasiasa wenzake! kwa hili namfananisha na Lowassa!

Aina ya wabunge vichaa kama LEMA, Hawatakaa wafikie upeo wa Zitto hata robo siku zote za maisha yao!

Mimi nawashangaa hawa wanaotaka kumlinganisha zitto PhD holder na mbowe zero form six.
 
Bill Gates aliacha kuisaka digrii kwa sababu akili alizokuwa nazo zilikuwa zaidi ya digrii. Mbowe hana digrii kwa sababu akili zake ni ndogo sana kuweza kuhimili mikiki mikiki ya digrii,

Bill Gates ni one of the best managers and the richest person on earth. Na hana degree!
Mbowe ana manage multi-millions businesses in the country (Zitto anategemea rushwa akitegemea kuwepo kwake PAC)!
 
Bill Gates aliacha kuisaka digrii kwa sababu akili alizokuwa nazo zilikuwa zaidi ya digrii. Mbowe hana digrii kwa sababu akili zake ni ndogo sana kuweza kuhimili mikiki mikiki ya digrii,

Asingekuwa anaendesha biashara ambazo ni worth millions of dollars then kama ni mjinga hivyo! Nape ana masters degree nasikia, muulize kama anamiliki japo glocery yenye mtaji wa shilling milion moja na ikawa na faida!
 
shemeji yangu acha kudanganya watu, Zitto yuko kwenye project ya mtu wetu tunayemtaka magogoni.

Yeye anatakiwa agombea kupitia ACT ili kugawa kura za wapinzani ili mtu wetu apite. Hata fedha tunamchangia na ACT haijakosa pesa ila kuaminika kwa wananchi.

Zitto ni muhumu sana kwa project ya mamvi kutinga ikulu. Maana mpaka sasa mtu wetu ndani ya chichiemu hana mpinzani. Tatizo lake ni CDM na dawa ya Chadema ni project zitto ili agawe kura na mtu wetu apenye. Haya yanajulikana mpaka mtaa wa ufipa ni suala muda tu hili dili nalo litalipuliwa na kupotezwa kabisa shemeji yangu.

You should go back to your drawing Board other wise there is no hope here. Zitto is finish. Chezea Makamanda uone
 
Pasco,
Cons

  1. Kuaminika kwa mashaka
  2. Not a good team player
  3. Not settled emotionally
  4. No stable in love
  5. Umimi egotism.
  6. Kujiamini kupitiliza (over confidence)
  7. Kujikweza (superiority complex)
  8. Kujifagilia kwa sana (boastfulness)
  9. Kuambilika haambiliki
  10. Fault finder hivyo ni parfectionist!.
Katika hizo Cons unajua kwamba hizi huwa pia ni sifa za Kiongozi bora ktk vitendo, kosa kubwa la Zitto ni kutumia sifa hizi kabla hajapanda uongozi na hii huleta fikra za watu kutokukuamini. Nitakwambai kwamba hata Nyerere, Nkurumah, Nasser na hata Gadaffi na wengine kina Lincorn, Reagan wote hawa walikuwa na sifa hizi baada ya kuchukua madaraka.

Mfano mzuri Mwl. Nyerere, alijifanya sana mtu wa west akakubaliwa na kupewa misaada Kibao na CIA aliongia Ikulu tu akawageuka. Wazee wa dar walimuamini wakifikiri akiingia Ikulu watakula naye sahani moja pale alipotoka Muingereza kumbe mjamaa alipoingia akawaambia hizini mali za Umma sii zenu. Kina Reagan na wengine wote walijua mchezo wa Kisiasa unakwenda vipi mna walipoingia madarakani wakawa watu tofauti kabisa wenye misimamo yao.

Zitto anajionyesha sura yake mapema sana kiasi kwamba achokiamini ndicho anachokitoa hata kwa wanasiasa wenzake, kumbe ni makosa makubwa kisiasa, the guy is good ana makosa ya kibinadamu tu kila mtu kisha ingizwa mkenge akidhani kapata kumbe amepatikana.
 
Back
Top Bottom