Hii nchi tunaipeleka wapi iwapo haya ni ya kweli?

Hii nchi tunaipeleka wapi iwapo haya ni ya kweli?

Kwa hivyo Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa ni kama hawana Kazi !?.Yani unajifanya kuondoa Tatizo kwa kuongeza Tatizo kubwa zaidi !?.Huku ni kuwaza kizamani kabisa na hiyo Sheria ni kandamizi kabisa na haifai.

Haujajibu Swali langu nililo kuuliza Mkuu.
Kwa imani yako takukuru peke yake inaweza kumaliza rushwa bila kushirikisha kila mtu au kila taasisi kuweka mikakati ya kuzuia rushwa? Hili sio swala la Takukuru pekee yao, hata wewe pambana bagosha.
 
Umeulizwa huko hivi,; Wabunge na madiwani wote mliowanunua baada ya wiki moja mkawapa ugombea walitimiza miaka miwili ccm ?

Angalia unavyong'aang'aa macho na kutukenulia mimeno!
Ukipita huu uzi vizuri utaona hoja yako imeshajibuwa.
 
MN
Unaelezeaje wabunge na madiwani lukuki waliohamia CCM kutoka vyama vya upinzani,na kisha wakateuliwa na CCM kupeperusha bendera ya chama kwenye majimbo na kata walizokuwa wakiziongoza kabla?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ndugu yangu, hiyo watu kuhamia CCM wakapewa ubunge ilikuwa zamani. Hii hoja ya kuzuia watu miaka 2 kama ikipita itawahusu hata CCM hawawezi kuikwepa.
 
Mtu anakuja kwenye chama dakika mbili mara pap, yeye ndio mshika kibendera. Waliohagaikia chama kama kina Mzee Slaa wanatupwa nje, tena kwa kejeli. That not a level playing field.
Wee mushumbuz ya 2015 bado yanakuuma?
 
...yaani tena huko ZNZ ndio wawe makini sana, ni vigumu sana kwa chama chenye mrengo wa CUF au ACT kushinda au kupewa nchi, ni bora hata CHADEMA inaweza kupewa nchi kule kuliko hivyo vingine, hilo ni tatizo la kihistoria la kutoaminiana, kuna kale kamsemo ka "Mapinduzi Daima"....
Mkuu,
Samahani, tatizo la Zanzibar sio kutoaminiana. Tatizo Zanzibar si tofauti na Bara. Tatizo kubwa ni CCM kung'ang'ania madaraka yasiokuwa yao!
 
Zanzibar inajiendesha yenyewe kwenye siasa za ndani ambazo hazingiliani mambo ya muungano. Kama bara watapenda na wao wanaweza kupendekeza.
Na wala hamtaishia hapa! mtaendelea kujitungia sheria za ajabu ajabu ili mradi muendelee na njama zenu za kubaki madarakani. Ila mjue mwisho wa siku sheria hizi zitawageukia wenyewe, tena siku yenyewe haiko mbali.
 
Mimi huwa sielewi why tunawategemea marekani na mataifa mengine,watanzania tupo milioni 58 hivi,ccm wapo chini ya milioni 14.hivi watu milioni 44 kuburuzwa na watu chini ya milioni 14 ni ujinga,uzembe au ubwege?

Kusema ukweli ni ubwege. Shida mabwege ni wengi mno na wengi wao wanaimba mapambio.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom