Hata baada ya kujua Mgombea wa CCM ni Magufuli, why kuna watu bado wanaleta mizaha? Kunashusha hadhi ya Urais wetu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,

Leo tena nimepata fursa ya kuwaletea makala hii ya "Kwa Maslahi ya Taifa". Hili ni bandiko la wito kwa Watanzania tuache kufanya mizaha kwenye kila kitu kama hali ilivyo sasa ya kufanya mizaha kwenye kugombea Urais wa JMT na Zanzibar, hata watu wasiostahili, wanapeleka majina yao!. Miongoni mwao wamo walevi, wazinzi, waasherati, wadanganyifu wa umri, kuna hadi wabakaji na wauawaji!

Mizaa ya namna hii kwenye kugombea Urais, kunaufanya urais wa JMT na Zanzibar kuwa ni kitu cha kawaida sana, hadi watu wa hovyo hovyo wanaweza kugombea, na ikitokea watu hawa wa hovyo wakapitishwa na vyama wao, then wanaweza kuchaguliwa kuwa rais wa JMT na Zanzibar na hivyo kujikuta tumepata rais wa hovyo kama ambavyo ilivyotaka kutokea 2015, ingekuwa sio JPM kujitokeza kuokoa jahazi, you can just imagine hali ingekuwaje sasa!. (Naomba msiniulize nani mlevi, mzinzi, muasherati, mbakaji na muuaji) wapo na tunawajua!

Hata baada ya kujua kuwa mgombea urais wa CCM kwa uchaguzi Mkuu huu wa 2020 ni JPM na anaendelea tuu kukamilisha ngwe yake ya pili why kuna watu bado wanaleta mizaha kwenye kugombea urais kwa kuletea majina yao?!. Hii mizaha ya every Tom, Dick and Harry kujiona anauweza urais, wa JMT na Zanzibar, kunashusha hadhi ya urais wetu, kuonyeshea mtu yoyote tuu hata akiwa ni mtu wa hovyo vipi, anaweza tuu kuwa rais wa JMT au Zanzibar. Haya mambo ya watu kugombea urais kwa ku beep au kujaribisha tuu, kwa sasa yamepitwa na wakati!, kwanini tuendelee kuruhusu watu kufanya mizaha kwenye urais wa JMT na Zanzibar?

Nimeuliza hivi kufuatia milolongo ya watu kujitokeza kwa wingi kwenye vyama kuutaka urais wa JMT na kule Zanzibar kuutaka urais wa Zanzibar, miongoni mwa waliojitokeza kwenye vyama, kuna watu wa ajabu ajabu!, natamani kufanywe midahalo ya wazi ya wagombea wote wa urais wa vyama kwa kwanza kwa kuanzia midahalo ya ndani ya vyama, halafu midahalo ya kitaifa baada ya kupitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa wagombea urais wa JMT, na Zanzibar, tuwafanyie midahalo ya kitaifa ili kupata rais bora zaidi na ni kwa kupitia midahalo hiyo mtawabaini walevi, wazinzi, waasherati, wabakaji na wauwaji!

Urais wa JMT ndio nafasi muhimu kuliko nafasi zote ndani ya JMT, hivyo kunahitajika umakini wa hali ya juu tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa rais, hakuhitajiki kufanywa mizaha mizaha ya aina yoyote katika kumpata rais wetu wa awamu ya 6, kwa sabubu rais anayetosha tayari tunaye, wanaojitokeza kumpinga, wanapaswa kuwa ni Wapinzania wa ukweli ambao they can make a difference na sio kugombea kwa kutania!

Siasa ni sayansi ya siasa, tunapoelekea kwenye uchaguzi wa rais, baadhi ya Watanzania wenzetu japo wana sifa na vigezo vya kugombea urais wa JMT kwa mujibu wa katiba, lakini wanafanya mizaha.

Mara baada tuu ya uchaguzi Mkuu wa 2015, na dalili zote kuonyesha JPM anachukua ushindi, niliuliza humu
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kisha nikaja kuuliza
In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Jee Kwa 2020, Do We Still Have A Choice?.

Halafu nikauliza tena
Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!.

Sasa 2020 yenyewe ndio hii, michakato ya ndani ya vyama kuteua wagombea urais imeisha anza ila pia kwa kiasi fulani kwa maoni yangu, naona kama kuna watu wanafanya mizaa kutaka kuteuliwa na vyama vyao!.

Naomba kukiri, nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili, baada ya kuisoma hoja ya mwana jf huyu
... japo wananchi na wazee ndani ya chama wamemtaka afanye hivyo, haonyeshi kuwa mgombea na kimsingi hakujiandaa kuwa mgombea kabisa

Ili kuleta ushindani wa kweli na wa haki ni lazima kushindanisha wagombea wanaendana na kufanana. Kushindanisha mlima na kichuguu, au Tembo na sisimizi, ni kufanya mizaha kwenye siasa za urais!

Naomba kwanza nikiri haki kwa wote na usawa wa binaadamu kuwa binaadamu wote ni sawa, na maadam katiba imeweka sifa na vigezo vya kugombea urais, katika Ibara 39 inasema kuwa mtu atachaguliwa kuwa raisi kama ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia. Pia awe ametimiza umri wa miaka arobaini. Awe ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa. Awe na sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi. Na katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali

Pia naomba kukiri tangu ile 2015 kati ya wale wagombea zaidi ya 40 wa CCM waliogombea na JPM kutafuta uteuzi wa CCM, kuna watu mule ni walikuwa ni wazuri kuliko JPM and would have made a better president than JPM lakini JPM aliwashinda kwasababu he was the chosen one, ila baada ya hii miaka 5 ya JPM, mtakubaliana na mimi kuwa kwa mwaka 2020-2025, rais tayari tunaye, hivyo tusifanye mizaha kwenye urais!.

Hata sasa miongoni mwa Watanzania, tuna Watanzania wengi tuu ambao ni wazuri kwenye urais kuliko hata JPM, kwa sifa na vigezo, lakini tunapokuja kwenye ugombea, hatuangalii sifa tuu na vigezo, bali pia tumeangalia mtaji!.

Kwa uchaguzi huu wa 2020, JPM ndie mgombea pekee wa urais wa JMT anaingia kwenye uchaguzi kwa awamu ya pili huku akiwa na mtaji mkubwa, (track record) wa aliyoyafanya na yakuonekanika, hivyo ilitegemewa huko kwenye vyama, waombaji kuteuliwa wawe ni watu waliojitathmini based on JPM kuwa wanaweza kusimama nae na kujipima nae ubavu na sio kuwapandisha ulingoni mabondia wa uzito tofauti, bondia mmoja wa uzito mkubwa, heavy weight na kumpiganisha na bondia wa uzito mwepesi fly weight (uzito wa upepo) or feather weight (uzito wa unyoya), utakuwa ni ushindani usio sawia!

Ilitegemewa baada kujulikana 2020 bondia wa CCM ni JPM, ambaye ni heavy weight, vyama serious vitatafuta wagombea ma heavy weight wa kumkabili JPM na kama hawana ni bora waunganishe nguvu kumsupport mgombea mmoja ambaye angalau, atafanania fanania!, haya ya kushindaisha tembo na sisimizi, sio ushindani wa haki ni kuleta mizaa kwenye urais!

Kwa maoni yangu, kwenye kambi nzima ya upinzani Tanzania, tuna watu wawili tuu ndio wenye uwezo, wa ability na capabilities za kumkabili JPM na aka feel the heat ya uchaguzi. Hawa ni Zitto Zuberi Kabwe na Tundu Lissu.

Kabla ya kushambuliwa, nilipendekeza
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Ila baada ya kushambuliwa nikawa na mashaka kama atarejea nchini
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Hata baada ya kumuandikia barua IGP, kumuomba kuhakikishiwa usalama wake nilishauri
Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Sasa baada ya Tundu Lissu kutangaza nia ya kugombea urais kupitia Chadema, iweje watu wengine ambao ukiwalinganisha na JPM hawajai hata kwenye kiganja lakini wanaomba kuteuliwa?

Hii ni mizaha!, tufanye mizaha kwenye mengine yote ikiwemo kwenye kuposa, lakini tusikubali kabisa kufanya mizaha kwenye urais wa JMT. Mifano hai ya hii mizaha kwenye urais wa JMT ni kama hii
Uchaguzi 2020 - Je, kuna uwezekano kutangaza nia kugombea Urais kupitia CHADEMA kwa baadhi, kunatumika kama kichaka cha kujifichia aibu ya kushindwa ubunge?

Uchaguzi 2020 - Jicho la Tatu: Mgombea Urais CHADEMA ni Freeman Mbowe! Tundu Lissu Pacemaker! Nyalandu ni Serious Contender, Msigwa anatania, Dkt. Mayrose Majinge
Mizaha kama hii ya nini?

Watanzania wenzangu, tuacheni mizaha kwenye urais wa JMT! haya mambo ya mzaha mzaha mwisho wa siku tutakuja kujikuta mizaha hii inatupekea kuja tukajikuta mizaha hii inatutumbukia.
kama ilivyotaka au ilivyotokea ile 2015!

Jee kwa 2020, jee tuendekeze mizaha hii au twende straight?

Nawatakia Jumanne njema.

Paskali.
 
Watanzania wenzangu, tuacheni mizaha kwenye Urais wa JMT!, haya mambo ya mzaha mzaha mwisho wa siku tutakuja kujikuta tunatumbuka...

kama ilivyotokea...



Nawatakia Jumamne njema.

Wewe Pasco wewe....
😂😂😂😂😂
 
Kwani mpaka sasa hivi kuna chama kimeshapata mgombea wa kiti cha Urais ukiacha Chamadola? Wote bado wako kwenye mchakato sasa kwa nini unataka waache michakato yao ndani ya vyama vyao na wafanye kama unavyotaka wewe au na wewe ni Mungu wa kanda yetu pendwa? Wacha udikteta Mami Pasi.
 
Mizaha mizaha mizaha..

Labda ungeelezea kwanza hilo neno umelitumia katika bandiko lako kwa maana ipi?

Kisha uelezee nini maana ya mizaha?

Ila Kama Hilo neno limetumika kwa maana inayoijua mimi basi hakuna mzaha mkubwa uliofanyika kama ule wa kuchapisha fomu moja ya mgombea wa urais, huku tukiaminishwa kuna demokrasia kubwa ndani ya ccm..

Mzaha mwingine ulikuwa ule wa 2015 kujitokeza wagombea urais zaidi 40, Bora hata hao wanaojitokeza huko Zanzibar hawatafikia namba iliyojitokeza 2015.

Mzaha mwingine uliyotia fola ni ule wa Jecha S. Jecha huko visiwani..

Mzaha mwingine ni kwenda kwenye uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi

Hii mizaha mingine uliyoelezea wewe inatokana na katiba ambayo inatoa sifa za nafasi ya ugombea nafasi ya urais ambayo inampa nafasi ya mtu kujitathimini nakuona anatosha Kisha anachukua fomu, wacha twende hivyo hivyo kimzahamzaha tutafika hata mengine yametia kimzaha mhaza.
 
Ndiyo maana ya democracy mkuu af wa hovyo anaweza kuwa Bora sn kuliko anayeonekana mwema tuna mufano mingi mizuri ya viongozi hovyo baada ya kuipata so don judge a book by its cover fungua kisome na zaidi ka amefanya mazuri hofu ya nn Sasa?
 
Back
Top Bottom