Hii Mitandao ya simu inatutakia nini wanateknolojia Tanzania?

Vifurushi vya postpaid ndo vinaweza kuwa na unafuu kwa sasa nadhani japo sijavifuatilia kwa umakini
 
Postpaid hela kubwa ila value pia kubwa 25,000 unapata GB 30 ina maana roughly kwa kila 1000 unapata 1.2GB.
Haswaa na ndio nataka nizifuatilie maana hizi bei mpya za vifurushi value for money haipo kabisa mkuu!
 
Halotel wana 1gb kwa Sh 500 na 5gb kwa sh 1500
Daah! Hiyo 1.5k kwa Airtel ilikua 10GB at least kwa siku nilikua natumia 20GB kwa 3k ndiyo nlkua natumia kwa matumizi ya ku update mashine na kupakua softwares & files zangu za kazi make na nyingi zina ukubwa kuanzia 1GB.

Kimeniuma sana walivyokitoa, heri wafute vyote tu sasa.
 
Nilikuwa nimezoea halotel sh elf5 napewa gb6 kwa wiki moja leo najiunga nakutana na elf5 gb3 hadi nimechoka tunakwenda wapi
Hmm! Ilikua gb6 au 7 mkuu? Mimi nlkua napewa gb7 kwa 5k kwenye vifurushi vya 4G pale! Daah kama na hiki wamekipiga panga basi chip yao wacha iendelee kukaa kwenye droo tu.
 
Haipo
 
Solution ni fibre zisambazwe mitaani na company inayojielewa au kuwe na company ya simu inayotoa bando za internet tu kwa bei nafuu.

Ukiondoa vifurushi vya usiku sina kifurushi kingine ninachonunua ni bora waondoe vyote tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…