kimpe
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 911
- 861
Jana niliona kwenye mitandao ya kijamii wananchi wakilalamika kuchukuliwa eneo lao na Taasisi ya Kilimo Uyole. nilipofuatilia hili suala ni kwamba lilishafanyiwa maamuzi miaka mitatu iliyopita na waziri wa Ardhi wa kipindi hicho Mh Lukuvi kwa kuwarudishia wananchi hekari zao 67 ambazo kilimo walizihitaji lakini wakashindwa kuzilipia fidia kwa miaka takribani ishirini.
Mbele ya Mbunge wa Mbeya ambaye ni spika wa Bunge ambaye aliwaombea wananchi hao na mgogoro huo ukatatuliwa lakini siku tatu zilizopita Mkurugenzi wa Kilimo kawapa tenda Suma JKT Uyole wajenge ukuta ndani ya makazi ya watu ambao wameshahamia kwa nia ya kutaka kulitwaa upya
Taharuki hii anaypianzisha mkurugenzi haijulikani ni nani yupo nyuma yake lakini kwa anayoyafanya ndo yale Miaka ya unanijua mimi nani wapeni haki zao wananchi kuwafidia hamuwezi