FOCAC yanyanyua wakulima wa Afrika kimapato na kuondokana na umasikini

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1638492373516.png

Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), umemalizika hivi karibuni mjini Senegal, Senegal. Mkutano wa mwaka huu ni muhimu sana kwasababu umeonesha hatua kubwa zilizopigwa katika miongo miwili tangu mkutano wa kwanza ufanyike mjini Beijing mwaka 2000.

Wakati ushirikiano huu ukikua na kupasua anga kwa miaka 20 iliyopita, Baraz hili kati ya China na nchi za Afrika, bila shaka limekuwa mwongozo muhimu sana ndani ya bara la Afrika pamoja na mshirika wao wa nje ya Afrika ambaye ni China. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimenufaika sana na baraza hili na hata ushirikiano wake na China kwa ujumla, ambapo hadi sasa imefaidika na miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundo mbinu, teknolojia, biashara, nishati, pamoja na kilimo.

Kupitia ushirikiano wa kilimo kati ya Tanzania na China, Tanzania imeanza taratibu kujinyanyua na kujiondoa kwenye lindi la umasikini. Akieleza kile wanachonufaika nacho kutokana na miradi mbalimbali ya ushirikiano wa China na Afrika katika kilimo, Kaimu Mkurugenzi wa uzalishaji wa mazao katika Wizara ya kilimo, Chakula na Ushirika, Beatus Malema anasema Tanzania inajifunza mambo mengi sana ya kilimo kutoka China, kupitia mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu na hata kupatiwa teknolojia ya uzalishaji wa mazao.

Kilimo ni uti wa mgongo katika kukuza uchumi na kuleta ajira kwa Taifa. Tanzania inajitosheleza kwa chakula kwa kati ya asilimia 112 na 118. Asilimia 75 ya kipato cha Watanzania hutokana na kilimo na husaidia ukuaji wa nchi hiyo. Hivyo ujio wa teknolojia za kilimo kutoka China umeanza kuwakomboa wanyonge ambao hapo awali walilazimika kutumia njia za jadi zilizowachukua muda mrefu na pia kupata mazao machache.

Fikiri Kisairo, ni mkulima wa Kijiji cha Kitete wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, hivi sasa anasema anajivunia sana na shamba lake la mahindi linalostawi kila uchao.

“Zile siku za kurukwa na usingizi usiku nikifiria namna ya kutafuta ada ya shule kwa watoto wangu wawili zimeisha sasa,” anasema Kisairo, ambaye ni mnufaika wa ushirikiano wa kilimo kati ya China na Tanzania ambao unaendelea kwa miaka 10 sasa na kusaidia kuondoa mamia ya wakulima wa Tanzania kwenye umasikini.

Kisairo alijiunga na mradi wa mahindi mwaka 2019 unaosimamiwa na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Tanzania, ambao unashirikia vijiji vingi vya mkoani Morogoro ili kuondoa umasikini kati ya wanakijiji hao.

Mkulima huyo, ambaye alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa kongamano la “Mafanikio ya Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Tanzania: Teknolojia Ndogo, Mradi mkubwa wa Mavuno”, anasema alijiunga na mradi wa mahindi baada ya kutimiza masharti waliyopewa wakulima na baadaye kushiriki kwenye mradi huo kwa miaka mitatu sasa.

“Kuongezeka kwa mavuno ya mahindi kumeniwezesha kujinasua kwenye mtego wa umasikini kwani sasa nina chakula cha kutosha na nauza mahindi ili kuongeza kipato changu.

Kisairo, ambaye ana familia ya watu watano, sasa anajigamba kwamba chini ya mafunzo na ufadhili wa China kwenye kilimo, anaweza kulipia ada ya shule ya watoto wake, na amechimba shimo kubwa la maji ambalo analitumia kumwagilia bustani yake ya mbogamboga yenye ekari 1.21 katika mwaka mzima, ikiwemo misimu isiyokuwa na mvua.

Konsela mkuu wa ubalozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, amesema kwenye masuala ya ushirikiano wa kilimo, China na Tanzania ni washirika wazuri sana. Mradi wa mahindi sio tu umeongeza uzalishaji wa mahindi, lakini pia umeboresha hali ya maisha ya wakulima wengi kwani bidhaa nyingi za Tanzania sasa zinaingia kwenye soko la China.

Lakini ushirikiano huu wa kilimo haupo Tanzania pekee, bali China inatanua mbawe zake na kuzisadia nchi nyingine nyingi tu za Afrika, ikitarajia kupitia ushirikiano huu wa FOCAC, bara la Afrika nalo litaweza kujikwamua na kila nchi kuweza kulisha wananchi wake kama ilivyofanikiwa yenyewe kuondoa tatizo la njaa.
 
Back
Top Bottom